Pascal pole sana,najua JKN alikuwa anashida lakini hili la kuua na kutesa kwa sababu ya kutukana,kuhojiwa sidhani kama lingekuwepo kwa JKN.
Kiongozi yeyote akishashindwa kuongoza basi matokeo yake ni kutumia idara hii kunyamazisha watu.
Uko sahihi sana Mkuu
Uwezo Wa kiuongozi uko chini na mbaya zaidi kuna ukimbukeni Wa MTU kuwa Amiri Jeshi Mkuu kiasikujiona yeye yuko juu ya kila MTU na kila kitu
Kuongoza pasipo rejea ya mipaka yake kisheria ndiko kunaleta yote haya
Polisi kufanya kazi pasipo kujitambua wajibu wao kadri ya sheria iliyofanya wawepo huku wakiishi na kusubiri amri za wenyeviti Wa kamati za ulinzi na usalama ndipo watende kumewapanya wawe wanawayawaya na kutenda mambo ya ajabu ambayo yanawafanya waonekane kero mbele ya jamii inayowazunguka
Polisi wamegeuka miungu watu kwenye vituo vyao vya kazi
Wamepewa ruhusa ya kutenda yhalifu dhidi ya RAIA na kufanyika kuwa moja ya sehemu hatari kwa uchumi na ustawi Wa RAIA
Polisi wanajituma sana kufanya kazi zile ambaxo zinawafanya waweze kuteka fedha ya wananchi
Mimi niliibiwa simu yangu janja nikaenda kuripoti
Kuna jamaa muungwana aliniambia bro. Simu yako inaweza kupatikana tena kwa muda mfupi, lakini hao Wa kitengo hawawezi kuitafuta kwa ajili ya wewe kuipata Bali wataitafuta na kumkamata aliyeinunua na kumbandikia mashtaka maxito labda kuwa simu hiyo iliibwa kwenye tukio LA ujambazi na kuna mauwaji yalifanyika ili kuongoze dau kwa jamaa kuweza kuachiwa
Hivyo dau huwa ni kati ya Tsh 1m hadi 3m kutegemea nafasi au tathmini ya aliyekamatwa na simu kiuchumi.
Hivyo kupata simu yako labda uwape fedha kubwa kuliko watakayodai kwa watae mkuta nayo
Huo ndio mchezo
Sasa ni kwa jinsi gani polisi ambayo wamegeuka Mali binafsi Wa mkulu kwa kuwa anawatumia apendavyo ili kumsaidia kutimiza makengo yake kisiasa wawezaje kurudishwa kwenye mstari wakawatumikia watz ?
Hizi special tasks zinatumika vibaya sana hasa kwa kuwa chini ya komandi za non combatants