TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Hii taasisi iwe na weledi wa hali ya juu.

Wajiepushe na majungu kabisa,hili nalo linawavunjia heshima,nadhani uwepo mfumo wa udhibiti wa intelligence analysis,asiachiwe mtu mmoja hasa huko mawilayani,kwa sasa taasisi inakosa heshima nadhani kwa kuwa pengine hakuna guidelines za kufatwa kabla intelligence information haijawa acted upon.

Lazima mabosi wa hawa maafisa wawe wanawabana vijana wao waje na hard facts,ambazo zimekuwa analysed sawasawa,akileta jungu kisa tu amegombania demu na mwananchi,piga chini taarifa yake.

Pia ziwepo rules of engagement kati ya taasisi na wanasiasa,inawezekana taasisi ikawa nzuri kila hakuna rules of engaging with politicians,ni wazi wanasiasa ni watu wa visasi,na visasi vyao vinaanzia jinsi wanavyopata madaraka,ni vizuri taasisi ikaweka taratibu detailed ambazo zitawafanya wanasiasa kama wakuu wa mikoa,wilaya,wasiwatumie vibaya,na afisa akikubali kutumika vibaya,ajue kuna adhabu,hii itawapa Uhuru na utashi wa kuwashauri wanasiasa kwamba mzee hoja yako tumeisikia,tumeichambua,tunakushauri acha,suala hilo litavunja heshima yako,ya serikali,na hata wananchi wataitilia shaka serikali.

Ila kimsingi hawa jamaa mpaka sasa,naona kama wana mzuka,wanabebwa na kushawishiwa na wanasiasa kutumika vibaya,ni hawa hawa juzi awamu ya nne,ya tatu,wengine ya pili walikuwepo kama watu wazuri tu,wanasiasa wanapowapa kiburi shida inaanza

Hata polisi walitaka kubadilika,lakini nadhani wamekumbushana kurudi kwenye msitari

Tatizo la nchi hii ni wanasiasa.....tukishaweka miongozo ya wazi ya mahusiano kati ya wataalam na wanasiasa,nchi hii itakuwa kama China ndani ya miaka 50!

Sehemu zote wanazolaumiwa,ni kwa sababu mwanasiasa aliwaharibu(ishu ya nape,press conference ya Roma na harmomwakye)

Japo sipingi mabadiliko
 
Kama TISS kisheria hairuhusiwa kukamata.kutesa na kuua,je ni nani huyo aliye juu ya sheria ama ananyamazia au anawapa jeuri kuvunja sheria with impunity?
umeona eh........ kama kisheria (yao ya kazi) wanaruhusiwa hata kumbana mtu korodani kwa praizi.... ili mradi wapate wanachokitaka..............how comes tunawahukumu??
 
Haya mambo yanaumiza sana na yanatengeneza hasira kwenye nafsi za wananchi!!!Sometime una umia mpaka basi,hivi hao huenda wanalindwa ndiyo maana hawaogopi,je watoto wao wanalindwa?Ndugu zao na marafiki zao wanalindwa?Serikali iondoe huu ukakasi.....
 
umeona eh........ kama kisheria (yao ya kazi) wanaruhusiwa hata kumbana mtu korodani kwa praizi.... ili mradi wapate wanachokitaka..............how comes tunawahukumu??

Hata Sheria yao hairuhusu wanafanya tu kwa kulifanya wako juu ya Sheria. Na inafanyika kwa Kiongozi asiye na uwezo wa kuongoza anatumia mabavu ili watu waogope kukosoa.
 
Huko CCM ndiyo mbinu ya kipepeezi.Kwa Tanzania inakiuka Katiba,Sheria na haki za binadamu.
....Mheshimiwa rais kazi kubwa ni kulinda amani na usalama wa raia na ukishindwa hiyo basi tunaelekea kubaya.....I trust you president watekaji wanakuchafua na naimani hukuwapa hiyo kazi.
 
TISS ya leo imekaa kindugu ndugu, ukabila, yani inatia hata kichefuchefu kuzungumzia TISS ya leo...
Ule usiri wa ajira wanautumia kupandikiza ndugu zao kimya kimya,sijui kama wana mechanism ya kuondoa possibility ya kukuta taasisi yao ni mzunguko wa wanaukoo wa watumishi waliowahi kufanya kazi humo
 
Back
Top Bottom