Hii taasisi iwe na weledi wa hali ya juu.
Wajiepushe na majungu kabisa,hili nalo linawavunjia heshima,nadhani uwepo mfumo wa udhibiti wa intelligence analysis,asiachiwe mtu mmoja hasa huko mawilayani,kwa sasa taasisi inakosa heshima nadhani kwa kuwa pengine hakuna guidelines za kufatwa kabla intelligence information haijawa acted upon.
Lazima mabosi wa hawa maafisa wawe wanawabana vijana wao waje na hard facts,ambazo zimekuwa analysed sawasawa,akileta jungu kisa tu amegombania demu na mwananchi,piga chini taarifa yake.
Pia ziwepo rules of engagement kati ya taasisi na wanasiasa,inawezekana taasisi ikawa nzuri kila hakuna rules of engaging with politicians,ni wazi wanasiasa ni watu wa visasi,na visasi vyao vinaanzia jinsi wanavyopata madaraka,ni vizuri taasisi ikaweka taratibu detailed ambazo zitawafanya wanasiasa kama wakuu wa mikoa,wilaya,wasiwatumie vibaya,na afisa akikubali kutumika vibaya,ajue kuna adhabu,hii itawapa Uhuru na utashi wa kuwashauri wanasiasa kwamba mzee hoja yako tumeisikia,tumeichambua,tunakushauri acha,suala hilo litavunja heshima yako,ya serikali,na hata wananchi wataitilia shaka serikali.
Ila kimsingi hawa jamaa mpaka sasa,naona kama wana mzuka,wanabebwa na kushawishiwa na wanasiasa kutumika vibaya,ni hawa hawa juzi awamu ya nne,ya tatu,wengine ya pili walikuwepo kama watu wazuri tu,wanasiasa wanapowapa kiburi shida inaanza
Hata polisi walitaka kubadilika,lakini nadhani wamekumbushana kurudi kwenye msitari
Tatizo la nchi hii ni wanasiasa.....tukishaweka miongozo ya wazi ya mahusiano kati ya wataalam na wanasiasa,nchi hii itakuwa kama China ndani ya miaka 50!
Sehemu zote wanazolaumiwa,ni kwa sababu mwanasiasa aliwaharibu(ishu ya nape,press conference ya Roma na harmomwakye)
Japo sipingi mabadiliko