TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Saa hizi mpaka vijijini eti wanahadithiana hizi habari za kutekwa watu,
yaani hii mitandao hii,

hivi kweli baba mchungaji kapilimba anaweza ruhusu hili jambo kweli halafu asubuhi akaamka kuendesha misa kweli?
 
Kumruhusu MTU aliyefeli darasa la saba na akafeli form four Ku interact na idara nyeti ya USALAMA unategemea nini??

Kama sio kufeli kwa idara??
 
Wanabodi
TISS ni idara nyeti, uadilifu wake unapaswa kuwa ni wa kiwango cha mke wa Kaisari, ile kutuhumiwa tuu ni kosa tosha hata bila kuthibitishwa!.

Huu mjadala unaoendelea kuhusu utekaji, utesaji na mauaji ambavyo vinahusishwa na idara yetu nyeti ya Usalama wa Taifa, TISS ni uthibitisho tosha kuwa TISS imechafuka inahitaji kusafishwa!.

...Paskali
Paskali kwanza pole kwa masahibu yaliyompata A. Mayala (RIP).

Nakubaliana na wewe TISS "inahitaji kusafishwa" kulingana na hali ya sasa kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiteknolojia. Mazingira ya kisa ulichokisimulia ni tofauti kabisa na ya leo.

Sikubaliana nawe kuwa "TISS imechafuka" ila siasa za vyama vingi vimechafua mila na tamaduni zetu. Wewe na mimi tunashuhudia maneno na vitendo vya ajabu, mchana kweupe, kana kwamba, nchi hii haina utawala.

TUEPUKE UMAARUFU WA KITOTO KWA LUGHA NA MANENO YANAYOCHOCHEA KUDHARAU MAMLAKA
 
Msiwalaumu sana wakuu, sasa mtu ameajiliwa na kapewa ' Job description' mbili tu, ya kwanza ni kuwalinda viongozi wa kitaifa na ya pili ni kuilinda serikali iliyopo madarakani kwa nguvu zote. Sasa hapo tutegemee nini? kuna tatizo la kifikra linatukabili si kwa Watanzania pekee bali Waafrika wote. Wakati maendeleo ya wenzetu ni uhusika wa moja kwa moja wa hizi taasisi sisi tumebaki kuzitumia kinyume, tumezigeuza kuwa kama mbwa wa kutulinda usiku na vibaka.
 
kuna series moja inaitwa 24, iangalie mtoa mada itakusaidia kupunguza resentment ulonayo kwa watu wa usalama. au alieiona amsaidie make mi binafsi imenisaidia mno kupunguza lawama za kitoto kwa wanausalama
 
Naendelea kuonganisha dot..na naendelea kujifunza na kuelewa mambo mengi juu ya "makirikiri"
 
Yote yawe nahisi yanayotamkwa na viongozi wa kisiasa, kuhusu utawala wa sasa, kuifitinisha na Raia, ni mchezo mchafu, hasara ya demkrasia katika jamii maskini.

Viongozi wa upinzani, wanachama, washabiki, wafuasi na wapiga debe, hamtoki kwenye kibano cha Rais Magufuli. Mtaendelea kukoromea kwenye kibano hadi mlegee. Hamna ubavu wa kubadilisha lolote na hata 2020 mtaambulia patupu.

PASKALI WAFIKISHIE UJUMBE HUO WALIOKUTUMA
 
Pascal Mayalla,
Paschal Manyalla!
Pole kaka kwa yaliyokukuta!
Niseme tu kinachoendelea sasa ni hofu ya viongozi, Why killing people, why torturing your fellow countrymen?
Hivi tatizo ni nini kama mishara kodi zetu sisi walala hoi simnapewa? Aliyekudanganya ukiwatesa wenzako ndio utakaa TISS milele yuko wapi! Kama ni kweli hawa TISS hawana weledi wowote, Hawapashwi hata kuhoji mtuhumiwa?
Nashauli wachunguzwe hawa japo naamini si wote , Huko TISS kuna vijana tumesoma nao tunawafahamu ni watu wachangamungu sana.

Mungu simama ujitete mwenyewe sisi tumeshindwa
 
Pascal Mayalla,
Huwezi kuniambia kiti, mazingira yote yanaonyeaha kuna baadhi ya wabunge wanakula mshahara wa muheshimiwa Manywele ili kukisaliti chama chetu. Haiwezekani hii hoja ya kutishiwa ichukuwe nguvu hivyo Bungeni na kuacha mambo ya msingi kujadiliwa. Mh Rais kuwa makini na wabunge Wako.
 
Wabongo bwana, kazi nzuri gani? Kwa Tanzania labda kusaidia kuiba kura ili chama tawala kiendelee kuwa tawala na wao waendelee kupata ulaji wao. Na wanafanya shughuli hiyo kwa kuchombeza na majungu ya vilabuni!
 
Yote yawe nahisi yanayotamkwa na viongozi wa kisiasa, kuhusu utawala wa sasa, kuifitinisha na Raia, ni mchezo mchafu, hasara ya demkrasia katika jamii maskini.

Viongozi wa upinzani, wanachama, washabiki, wafuasi na wapiga debe, hamtoki kwenye kibano cha Rais Magufuli. Mtaendelea kukoromea kwenye kibano hadi mlegee. Hamna ubavu wa kubadilisha lolote na hata 2020 mtaambulia patupu.

PASKALI WAFIKISHIE UJUMBE HUO WALIOKUTUMA
Wewe ni mchochozi tena ni mtu hatari sana kwa Taifa hili kama Mungu yupo basi ashughulike na wewe haraka.
 
Hapa kidogo zile halisi za kwako zimerudi, hongera kwa andiko hili lililoshiba, Mungu anakulinda na wewe wasikufanye watakavyo
 
Wewe ni mchochozi tena ni mtu hatari sana kwa Taifa hili kama Mungu yupo basi ashughulike na wewe haraka.
Mtashughulikiwa wote mnaotaka nchi isitawalike au mnaomba miujiza Rais Magufuli aondolewe madarakani.

Wewe na mimi tunashabikia tu upuuzi wa uchu wa madaraka wa watu fulani fulsni, lakini wakishika hayo madaraka, hali haitakuwa kama wanavyotaka tuamini.

NARUDIA KWA KUJIAMINI, WAPINZANI WASUBIRI 2025, LAKINI WAWE WAMRBADIRIKA - TANZANIA KWANZA WAO BAADAYE
 
Back
Top Bottom