Mkuu Pascal unayo hoja nzito. Kipo kingine kinachojitokeza ambacho ni muhimu kukiangalia kwa umakini mkubwa.
Hii inayoitwa vita ya kiuchumi, ni mpambano mkubwa wa kimaslahi, kushughulika na watu ambao wanauza almasi huko Ulaya na kupata mabilioni ya shilingi halafu leo hii biashara inaingia mchana, kwa kweli hao wafanya biashara wanao uwezo wa kuiharibia nchi heshima yake.
Miaka yote watu wanafaidika na madini yetu halafu leo hii ghafla bin vuup wanakuta mambo yamebadilika, ni lazima wafanye umafia kwa nguvu zote wakiwa na matarajio ya kuibuka washindi.
Nadhani ndio maana hata hao jamaa wa usalama wapo kimya, hawaongei mara kwa mara. Zipo taarifa kwamba kwenye masuala ya ukachero Tanzania inashika nafasi ya saba duniani. Hivyo pamoja na makosa mengi wanayofanya hao jamaa, bado wanao uhalali wa kuaminiwa kwenye maamuzi na nyendo zao.