Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 15,052
- 36,866
Aiseeh, nimecheka mpaka nimepaliwa.Plan B niolewe kabla haijafika niwe namuwinga mume..!! 😹😹
Punguza kamdomo uolewe sasa 🤣.
Aiseeh, nimecheka mpaka nimepaliwa.Plan B niolewe kabla haijafika niwe namuwinga mume..!! 😹😹
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesisitiza mvua kubwa za El Nino zipo na zitakuwa kubwa kuliko zilizotangulia.Umewasiingizia. Wamesema El-nino ipo kubwa. Hawajasema mvua kubwa za El nino.
Mamlaka ya ya hali ya hewa Tanzania(TMA) , imesema haijawahi kutangazia Umma kwamba kuna Mvua za El-nino.
Akiongea na Wasafi FM, Dkt. Mafuru Kantamla Meneja Ofisi Kuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) amesema wanaosema mvua za El-nino wanapotosha.
Kasema hivi, Namnukuu, "El-nino ni ongezeko la joto la bahari katika eneo la kati la Kitropiki la bahari ya Pasifiki. Lakini madhara yake ni madogo madogo kutokana na sehemu ulipo. Unajua tunakosea tunaposema mvua za El-nino, hilo ni kosa kubwa". Mwisho wa kunukuu
Amedai kwamba walisema kuna El nino si mvua ya El nino kwani El nino ilishaanza Tangu mei na itadumu kipindi kirefu 2027
TMA wamesema El nino ni hali ya hewa kutokana na sehemu. Sehemu zinginezo panawaka jua la El nino.
MY TAKE;
Mafisadi na Wala nchi ya CCM ndo walitia watu hofu ili wakope hela kwenye taasisi za kimataifa. Wamepewa hela wakagawana watu na Msoga rufiji na Zanzibar. Hela zimeisha na Miradi ya maendeleo imesimama. Kumbuka Serikali ya Tanzania ilitenga Bilioni 730 za kupambana na mvua kubwa za El nino. Walidai ni za kukarabati madaraja na kuzibua mifereji na zimeshaisha bila kufanyika chochote labda marekebisho madogo Madaraja ya Tanga.
Watu wamebomolewa nyumba zao kwamba nyumba zimeziba njia ya maji ya mvua za El - nino.
Sawa kama umeamua kukaa na ubishi wako...no problem.Ni bora ungekaa kimya tu boss, kuna mambo mengine hata kutetea ni aibu.
Hakuna mvua mkuu,labda useme tusubiri December ambayo haijaanza kuonekana kwenye rada,ila November no mvuaTatizo mpaka sasa hivi taarifa zinaonesha El Nino + Positive Indian Ocean Dipole. Hii kitu ni mvua kwa upande wa East Africa.
Kinachosababisha mvua hakuna (hali ya ukame) ni Madden-Julian Oscillation ambayo ipo Phase 2. Ni temporary atmospheric disturbance ndiyo inapelekea suppression ya warm air & delay in cloud formation. Ikienda Phase 4 tutegee mzigo wa mvua kushuka wa maana.
Tusubiri November - December
Wanaikanaje hii taarifa kindest ndezi hivyo? Kwamba watanzania hatujielewi wa hatujui hali rasmi inavyoendelea duniani?Dar Es Salaam – 18 Agosti, 2026
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa msimu wa mvua za Vuli (Oktoba – Desemba) 2026, ikitoa angalizo la msimu huo kuathiriwa kwa kiwango kikubwa na hali ya El Niño yenye nguvu kubwa iliyotokana na joto la bahari kuwa Juu ya Wastani katika Bahari ya Pasifiki, hali itakayochagiza ongezeko la Mvua za Vuli 2026 kuwa za Juu ya Wastani hadi Wastani katika maeneo mengi ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, Ukanda wa Ziwa Viktoria na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma.
Akizungumza juu ya utabiri huo, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia Nchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang'a alisema:-
"Msimu wa mvua za Vuli 2026 unatarajiwa kuathiriwa kwa kiwango kikubwa na hali ya El Niño yenye nguvu kubwa, hivyo mvua za Juu ya Wastani hadi Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi Ukanda wa Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, Ukanda wa Ziwa Viktoria na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma”. Aliongezea kusema kuwa Mvua hizo zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Septemba hadi wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba 2026 katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Viktoria, na kusambaa taratibu katika maeneo mengine katika mwezi Oktoba 2026, aidha alifanunua kuwa kwa kawaida mvua za Vuli huisha mwezi Desemba japo katika msimu wa Vuli 2026 mvua za nje ya msimu zinatarajiwa kuendelea hadi mwezi Januari 2027, na ongezeko la mvua likitarajiwa hasa katika kipindi cha mwezi Novemba 2026.
Akielezea juu ya athari zinazotarajiwa, Dkt. Chang’a ametahadharisha kuwa "vipindi vya unyevu kwenye udongo wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na miundombinu ya kilimo," pia aliongezea kusema kuwa ongezeko la kina cha maji katika mabwawa na mito linaweza kuathiri miundombinu ya rasilimali za maji na nishati, huku magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza kutokana na uchafuzi wa maji. Magonjwa ya mazao yanayosababishwa na kuvu, bakteria na virusi yanaweza kuathiri uzalishaji wa viazi mviringo, alizeti, maharage, ufuta pamoja na matunda na mbogamboga, huku sekta za usafiri, ujenzi na utalii zikitarajiwa kukumbwa na changamoto za mmomonyoko wa barabara, uharibifu wa madaraja na kuhama kwa wanyamapori kutokana na mafuriko.
Katika hitimisho lake, Dkt. Chang’a amewashauri Wadau wa sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii kupanga na kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia taarifa mahususi za hali ya hewa zinazotolewa na TMA ikiwa ni pamoja na kuvuna maji ya mvua, kuimarisha miundombinu, kutoa tahadhari za mapema na kudhibiti mazalia ya mbu ili kupunguza magonjwa ya mlipuko.
Na mitihani ya form four taifa ikasogezwa mbele kwa taarifa rasmi ya hawa jamaa. Leo wanakana kila kitu dah. Hivi hii nchi inauongozi na utaratibu rasmi uliopangwa wa uwajibikaji? Kiufupi tujue hakuna dereva na kila mtu ajiongeze kwa nafasi yake......Kwahiyo hadi wizara ya elimu wanasogeza mitihani ya kitaifa nyuma maana yake nao hawakuelewa kama hakuna Elnino?
Kwamba shule zitafungwa mapema ili kuwaepusha walimu na wanafunzi wasiaptwe na maafa ya jua kali la elnino?
Tangu lini mtanzania anajielewa?Wanaikanaje hii taarifa kindest ndezi hivyo? Kwamba watanzania hatujielewi wa hatujui hali rasmi inavyoendelea duniani?
Sasa wewe bibi wa ndio mzee utanielewesha nini mimi?unaonyesha mihemko na kiburi tena jukwaa, righ?🤣
Subutu! Task force zipite mtaa kwa mtaa kuhamasisha wananchi kupanua madirisha ya nyumba zao ili hewa ipite kwa urahisi.Kila kaya kwa jiji la dar tupatiwe air conditioner
Dj atupigie,,,,,Ccm mbele kwa mbele....Subutu! Task force zipite mtaa kwa mtaa kuhamasisha wananchi kupanua madirisha ya nyumba zao ili hewa ipite kwa urahisi.
Ili kufanikisha zoezi hili muhimu, fedha ya kutosha itengwe kununulia vitendea kazi muhimu ikiwemo vyombo vya usafiri vitakavyohimili jiografia yetu - kijiji kwa kijiji, mtaa kwa mtaa.
Mvua haionekani kwenye radar sababu kuna hiyo MJO phase 2. Hiyo muda wowote itaamia phase 3&4, mvua utaanza kuiona. Na ndiyo maana nimeweka November - DecemberHakuna mvua mkuu,labda useme tusubiri December ambayo haijaanza kuonekana kwenye rada,ila November no mvua
ok.Sasa wewe bibi wa ndio mzee utanielewesha nini mimi?