TMA: Hatujawahi kusema kuna Mvua za El-nino, wanaosema hivyo Wanapotosha

Duh....kwahiyo na shule kufungwa mapema ili zile gharama za uendeshaji kama vyakula, Umeme na usafiri nao wakale kwa urefu wa kamba 😢
Hatuna serikali aisee zile 730b zimeliwa kirahisi sana
 
Umewasiingizia. Wamesema El-nino ipo kubwa. Hawajasema mvua kubwa za El nino.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesisitiza mvua kubwa za El Nino zipo na zitakuwa kubwa kuliko zilizotangulia.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Ladislaus Chang’a alisema El Nino inaendelea kuimarika na itaendelea kuimarika mwezi ujao na kumairika huko kunadhihirishwa na kuongezeka kwa kiwango cha joto katika maeneo ya Bahari ya Hindi.

“Neno moja leo tuondoke nalo, El Nino ipo tena yenye nguvu kubwa kuelekea mwezi Novemba, kwa sababu hali inazidi kuimarika,” alisema Dk Chang’a wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika kikaokazi Dar es Salaam jana.

Alisema miaka yote ambayo El Niño imepiga nchini na maeneo mengine ya Afrika ya Mashariki, kiwango cha joto bahari kimekuwa kikubwa.

Aliitaja miaka hiyo kuwa ni 1982/1983, 1997/1998, 2015/2016 na 2023/2024, kiwango cha juu cha joto kimekuwa nyuzijoto zaidi ya 2.6 kuelekea kunyesha kwa mvua hizo kubwa za El Nino.

Dk Chang’a alisema mwaka 1982 ilikuwa nyuzijoto 2.2, mwaka 1997 nyuzijoto 2.4, mwaka 2015 nyuzijoto 2.6 na mwaka 2024 nyuzijoto 2.0.

“Na hadi sasa kiwango cha joto ni zaidi ya nyuzijoto 2.6 baharini, hivyo El Nino inaimairika, ipo na itakuwa kubwa kuliko zilizotangulia,” alisema Dk Chang’a.

Alieleza kuwa hali hiyo ya joto inashuhudiwa katika maeneo ya Afrika Mashariki na hii hushuhudiwa hali inapokuwa chanya upande wa Magharibi mwa bahari.

Chanzo : Habar leo
 

Watanzania sisi tupo moto
 
Hakuna mvua mkuu,labda useme tusubiri December ambayo haijaanza kuonekana kwenye rada,ila November no mvua
 
Kwahiyo hadi wizara ya elimu wanasogeza mitihani ya kitaifa nyuma maana yake nao hawakuelewa kama hakuna Elnino?

Kwamba shule zitafungwa mapema ili kuwaepusha walimu na wanafunzi wasiaptwe na maafa ya jua kali la elnino?
 
Nchi zingine za ukanda wa Afrika mashariki, wanasemaje?
 
Wanaikanaje hii taarifa kindest ndezi hivyo? Kwamba watanzania hatujielewi wa hatujui hali rasmi inavyoendelea duniani?
 
Kwahiyo hadi wizara ya elimu wanasogeza mitihani ya kitaifa nyuma maana yake nao hawakuelewa kama hakuna Elnino?

Kwamba shule zitafungwa mapema ili kuwaepusha walimu na wanafunzi wasiaptwe na maafa ya jua kali la elnino?
Na mitihani ya form four taifa ikasogezwa mbele kwa taarifa rasmi ya hawa jamaa. Leo wanakana kila kitu dah. Hivi hii nchi inauongozi na utaratibu rasmi uliopangwa wa uwajibikaji? Kiufupi tujue hakuna dereva na kila mtu ajiongeze kwa nafasi yake......
Na hichi ndicho kinachoendelea sasa
 
Kila kaya kwa jiji la dar tupatiwe air conditioner
Subutu! Task force zipite mtaa kwa mtaa kuhamasisha wananchi kupanua madirisha ya nyumba zao ili hewa ipite kwa urahisi.

Ili kufanikisha zoezi hili muhimu, fedha ya kutosha itengwe kununulia vitendea kazi muhimu ikiwemo vyombo vya usafiri vitakavyohimili jiografia yetu - kijiji kwa kijiji, mtaa kwa mtaa.
 
Dj atupigie,,,,,Ccm mbele kwa mbele....
 
Hakuna mvua mkuu,labda useme tusubiri December ambayo haijaanza kuonekana kwenye rada,ila November no mvua
Mvua haionekani kwenye radar sababu kuna hiyo MJO phase 2. Hiyo muda wowote itaamia phase 3&4, mvua utaanza kuiona. Na ndiyo maana nimeweka November - December

Ila twende na mwezi wako wa December, utakuwa uhakika zaidi
 
Elinino inaweza kuwa hata Samia. Ni kitu chochote cha hatari kupitiliza ndiyo maana ya Elnino. Hivyo hii ya sasa huenda ni Samia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…