TO wa mwaka 2006 kidato Cha sita anatrend mitandaoni baada kufariki 2020

AiseeπŸ€” Ila Kuna watu ambao walisona nae pale Tosa boys walisena jamaa alikuwa anakula msuli Ile mbaya.
 
Nchi hii ukiwa na akili sana, hakikisha unakuwa humble, maana wenye wivu, chuki zilizochanganyika na uchawi wamejaa sana, hasa kwa mizee ya huko chuoni inayojiita masupervisor.., wachawi sana hao..
Ni kweli kabisa hii kitu ni ya kuzingatia sana
 
Huyu mshikaji mi naanza form 5 ye ndo kawa t.o, alikuwa na kelele sana na nilikuwa nasikia habari zake kwa jamaa yangu alikuwa pale Tosa.

Nasikia aliwahi sema hata Mungu akae na shetan watunge swali, hawezi kukosa!
 
Miaka ya karibuni kuanzia pale zama za JPM. Kuna trend mbaya sana tuliitengeneza ya kuwadhalilisha wasomi hapa nchini, ndio hii inayozunguka mtaani mpaka leo.

Ukifuatilia kwa karibu hizi mada za wasomi na hawa vipanga utaona lengo la wengi linakuaga kuwadhalilisha na kuonyesha hawana lolote, cha kushangaza na wao wamesoma kwenye mfumo huo huo lakini wameshindwa ku-perfom kama hawa wenzao.

Kuwa TO sio mchezo ndugu yangu. Wakati naanza form pale azania, shule ya feza ilikua na utaratibu wa kufanya interview kwa vipanga wote watakaotaka kushiriki halafu top 3 wanachukuliwa na kusomeshwa kwa ufadhiri wa shule. Kuna jamaa tulianza nae form 1 pale azania alienda kupiga paper akapita kwenye 3 bora.

Wakati nipo shule ya msingi darasani nilikua na mpinzani mmoja ambae tulikua tunagombania nafasi ya kwanza yeye akishika 1 mimi 2,mimi nikishika 1 yeye 2. Katika story aliniambia ndoto yake ni kuwa TO form 4.

Nimesoma Azania olevel na Mzumbe alevel. Nimesoma na watu wana akili sana sana sana darasani. Walifaulu vizuri na hata ambao bado tuna urafiki mpaka leo wana maisha mazuri. Wengi ni diaspora na wapo kwenye mashirika ya kimataifa.

Pamoja na kukutana na mijitu yenye akili sana katika safari yangu ya elimu akini sijawahi kusoma na mtu yoyote ambae alipiga TO. Kuwa TO sio mchezo bhana, watu wana wivu tu.
 
Utaratibu wa kupewa scholarship kwa hawa vipanga ulishafutwa????
Nakumbuka miaka hiyo kaka yangu alifauli vizuri sana form six na alipata ufadhili na kupelekwa na serikali nje. Alisoma na yuko vizuri na yuko na kazi nzuri...... Inakuaje huyu kuishia kuwa mwalimu wa tuition???? Uwezo wake hakuutendea haki.
 
Tz bado haijali watu wenye akili sana, haijalishi mtu ana tabia mbaya kiasi gani lakini akishagundulika ubongo wake ni wa ajabu anatakiwa alindwe alelewe vizuri kwa maslahi ya umma.
Sio kumuacha tu, watu wa hivi hawatokei mara nyingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…