Aqua Man
JF-Expert Member
- Mar 17, 2017
- 336
- 1,144
Ilikuwa ni lazima wakamilishe zoezi lakini ikishindikana... Imani yako imekuokoa...
Dah! Ase na kwa hali hyo inaonyesha hawajafikiwa lolote?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ilikuwa ni lazima wakamilishe zoezi lakini ikishindikana... Imani yako imekuokoa...
LinatumikajeMmh hii sijawahi kusikia japo jivu linatumika sana na washirikina
Paka kulia usiku kwenye NYUMBA yako tena analia kama mtoto au mtu nn Maana yake na dawa pia?Hapana ni dawa fulani kama magadi ukiinywa kama kuna kitu kibaya tumboni kinatoka
Na dawa yake je?Duu ungezila ungeugua vichomi visivyo na tiba ama kukabwa na kitu kooni
Bro mshana Mimi niliota nipo chumbani Mara akatokea tandu,wakati nataka kumuua Mara akatokea Bui Bui mkubwa,nikatoka sebuleni nikapiga kelele nikarudi kumua yule buibui ghafla wakatokea nge wawili na wanamabawa ndipo nikakimbia Tena sebuleni,mdogo wangu akaenda akawauwa wale nge Mara ghafla akatokea nyoka na hapo ndipo tukakimbia wote Lkn mim kila nilipokua nakimbia mtaani Kuna nyoka kibao wananifukuza!!ndipo ikaja daradara nikapanda ila nishaingia ndani ya gari nikaona na nyoka nae anaangaika kuingia kupitia chini ndipo nikapiga kelele kwa konda kumwambia Kuna nyoka lakini sio konda Wala abiria walionesha kujali na hapo ndo nukashtuka zangu usingizi!!naomba unifafanulie ndoto hi na ilikua saa nne asubuh
Mmh ulinusurika kifo
hata mimi pia nimenusurika mara nyingi kula samaki,nyama ndotoniMlango wako wa sita wa fahamu uko vizuri
Mhm uliimaliza?Niliotaga nimenunua nyama mbichi mahala na nikaanza kula, ghafla kuna mtu akaja akiwa kama ananishangaa hivi, nikaanza kumtishia kwa kutaka atoke, nikatembea kuelekea duka lingine la urembo nikaanza kutazama wadada wakisukana (Something like that) 🙁🙁
Afu setting ni mjini kabisaa, yaaani daslam daslam hukoo
Roho yako ilikuwa nje ya mwili kuivinjari dunia ikawa inakutana na misukosuko ya hukoBro mshana Mimi niliota nipo chumbani Mara akatokea tandu,wakati nataka kumuua Mara akatokea Bui Bui mkubwa,nikatoka sebuleni nikapiga kelele nikarudi kumua yule buibui ghafla wakatokea nge wawili na wanamabawa ndipo nikakimbia Tena sebuleni,mdogo wangu akaenda akawauwa wale nge Mara ghafla akatokea nyoka na hapo ndipo tukakimbia wote Lkn mim kila nilipokua nakimbia mtaani Kuna nyoka kibao wananifukuza!!ndipo ikaja daradara nikapanda ila nishaingia ndani ya gari nikaona na nyoka nae anaangaika kuingia kupitia chini ndipo nikapiga kelele kwa konda kumwambia Kuna nyoka lakini sio konda Wala abiria walionesha kujali na hapo ndo nukashtuka zangu usingizi!!naomba unifafanulie ndoto hi na ilikua saa nne asubuh
Am not so sure, though nahisi sikuimaliza..... mana wakati yule mtu ananishangaa (nikawa namtishia kama namna nataka nipige kelele lakini sauti haitoki kwa kuzibwa na kipande cha nyama mdomoni), nilikuwa nimeshika kipande kingineMhm uliimaliza?
Kwa nini safi.Safi kabisa
NAKUMBUKA SASA: baada ya kuwa namtishia yule mtu atoke karibu yangu, kulikuwa na kibanda kidogo nje ya lile jengo la saluni nilimkuta mtu pale, nikamwambia anipe package moja ya kufungasha mzigo wangu, akanipa kijifuko kimoja ambacho kabla ya kulala nilikuwa navitazama E-bay (packages) nikaiweka mule kisha nikasogea kueleka huko kwa hao walimbwende 😀Safi kabisa
Habar samah naomba kupata ufafanuz wahii ndoto niliota tupo darasan mara ghafra akaingia mwanafunz mwenzetu Na gunia kalibeba mara ghafra akatoa nyoka wawili weusi mkubwa Na mdogo Ila ktk kuwatoa hao nyoka alikuwa anamlenga mtu mwingine Ila ghafra wale nyoka wakaanza kunifata mimi ktk kuwakwepa yule nyoka mdogo akaingia mdomoni kwangu nikaanza kuomba msaada kabla yule nyoka ajazama Ila niliyemuomba msamaadaa akanijibu bwana eeh me nimechoka akaondoka Na hatimae yule nyoka hajafanikiwa kuingia ndani kabisa ya tumbo langu hii ndoto nimeiota kama mwez sasa nasjapata jibu lake bdo inaniogopeshaVema tukarejea kwenye mada zetu hizi... Huko siasani ni tabu tupu... Kunaweza kukufanya mtu sometimes uwe na frustration zako... Nitajitahidi nisiende tena kule.... Japo naona kama naidhulumu nafsi.....
Dhana ya kula chakula ndotoni si jambo baya si jambo la ajabu japo kuna wakati huambatana na matatizo ya kisaikolojia kwa sehemu! Lakini lazima tutambue kuwa lazima tuote kuota ni lazima na kuna ndoto baadhi hazina maana yoyote zaidi ya kumbukumbu ya yaliyopita.....
Kuota mara kwa mara unakula ni ishara ya kutamani kufanikisha jambo fulani katika maisha, hamu ya kuwa na mahusiano , mali ama mafanikio yoyote yale.. Chakula ni uhai bila chakula uhai uko shakani hivyo kuota unakula ni dalili za kutaka kupata uhai kwenye jambo fulani
Lakini vilevile kuota unakula hutokana na kutamani chakula fulani lakini ikatokea hukukipata lakini ufahamu wako ukahifadhi ile hamu na usiku unapolala roho yako huondoka na kwenda kutafuta chakula husika na kuiridhisha nafsi tamanifu....
Sasa turudi kwenye mada... Kuota unakula nyama na kulishwa nyama... Kuna tofauti kubwa hapa
Kuota unakula nyama ni tafsiri ni dalili ya kutaka mafanikio ama kufanikisha jambo lako kwa njia ya kudhuru ama kuumiza wengine.. Yani ufanikiwe wewe lakini ukiacha wengine na madhara... Nyama inatokana na kuondosha uhai wa kiumbe hai kingine... Hii hutokana na mawazo tuwazayo bila kujua madhara yake kiroho... Kwa mfano penzi linazingua unatamani kurekebisha mambo lakini masharti ya mtaalam unatakiwa upate kuku wa kafara....
Ni kitu kama hiki... Unatamani cheo kazini, mvuto ama umaarufu nk unaambiwa dawa yake lazima itengenezwe na damu na mzoga wa mbuzi... Ni vitu kama hivi... Hivyo kupitia ndotoni hujidhihiri kwa njia ya kula nyama. Kwamba unashibisha nafsi huku kiumbe kikipoteza uhai
Sasa linapokuja suala la kulishwa nyama ndotoni... Hiki ni kitu tofauti kabisa.. Hizi ni ndoto zenye kuakisi uhalisia.. Ni ndoto za kichawi na unacholishwa ni nyama halisi kwa njia za kishirikina na nyama hizo si nzuri si nyama za wanyama tulao bali ni nyama za mizoga ya kenge nyani mbweha fisi konokono hata panya nk...
Sio nyama nzuri kwakuwa zina madawa ya kudhuru kiroho na hushibisha na hata kuvimbiza.. Hujaza tumbo kabisa na kukufanya ushindwe kula chochote.... Na tafsiri yake ni moja tu kukufunga usifanikiwe tena kwenye lolote.. Kwamba ukishakula na kushiba huwezi kula tena....
Namna bora ya kutatua tatizo hili ni kitunguu saumu na ndimu tuu... Kabla ya kulala hakikisha unalamba ndimu au kutafuna kipande cha kitunguu saumu ama vyote kwa pamoja... Kwa njia hii utakuwa umeidhibiti hiyo hali
Jr[emoji769]
Hapana huna haja ya kuogopa labda kama ingeendelea kujirudiarudia.. Sometimes ni ndoto za kawaida lakini inapojirudia ndio hapo sasa unaweza kuona kuna shida mahaliHabar samah naomba kupata ufafanuz wahii ndoto niliota tupo darasan mara ghafra akaingia mwanafunz mwenzetu Na gunia kalibeba mara ghafra akatoa nyoka wawili weusi mkubwa Na mdogo Ila ktk kuwatoa hao nyoka alikuwa anamlenga mtu mwingine Ila ghafra wale nyoka wakaanza kunifata mimi ktk kuwakwepa yule nyoka mdogo akaingia mdomoni kwangu nikaanza kuomba msaada kabla yule nyoka ajazama Ila niliyemuomba msamaadaa akanijibu bwana eeh me nimechoka akaondoka Na hatimae yule nyoka hajafanikiwa kuingia ndani kabisa ya tumbo langu hii ndoto nimeiota kama mwez sasa nasjapata jibu lake bdo inaniogopesha