Toka Bongo Fleva ianzishwe hakuna mwanamziki wa kike mwenye sauti ya kuvutia, kipaji cha kutunga na kuimba kwa hisia kama Lady Jaydee

Toka Bongo Fleva ianzishwe hakuna mwanamziki wa kike mwenye sauti ya kuvutia, kipaji cha kutunga na kuimba kwa hisia kama Lady Jaydee

Hapana sio kweli....msanii mwenye sauti nzuri na vocal Kali ni ruby na hata kwenye interviews nyingi walizofanya wasanii wengi wa kike walipoulizwa wote walikiri kuwa Kwa ruby hawaoni ndani...ruby anauwezo wa kuimba tunes ya chini kabisa ambayo wasanii wengine hawawezi kuifikia na anaimba tune ya juu (base) ambapo sio kitu Cha kawaita katika sauti...
Yeap Ruby ni miongoni mwa wasanii wa kike ninaowakubali sana kwa sauti na uimbaji wao.
Tatizo sauti yake huwa kali sana kiasi ya kwamba ni ngumu kuichuja ikachujika.
 
Kwenye Sauti hapanaaa. Ila vingine vyotee yuko vizurii mnooo.
 
Zuchu anabebwa zaidi na mazingira ya sasa ya mziki kama vile YouTube, wasafi, na ukizingatia suppoter kubwa anayoipata kwa Diamond, mama yake Hadija Kopa nk.

Ila bila hivyo angekuwa hamna kitu.
Wewe una wivu binafsi Zuchu anatoa hit song nyingi sukari, chechen, utaniua, fire baada ya hizo ngoma wakasema hatotoa Tena mbona Kali kama sukari lakini akajakuprove na Kwikwi ikahit Sana ebu mpe bidada maua yake ngoma zinapendwa Sana kuliko msanii yoyote vile ningekuelewa hoja yako kama angekuwa anatoa ngoma mbovu alafu anatamba
 
Yuko vizuri lakini kwa kipindi chake alikuwa anakiki sana kwa kuwa muziki ulishikwa sana na upande aliokuwepo (Clouds) lakini si kweli kuwa ana sauti nzuri kuliko wengine wengi.
 
Back
Top Bottom