Top 10 ya Makabila yanayoongoza kwa kula chakula kingi hapa Tanzania

Top 10 ya Makabila yanayoongoza kwa kula chakula kingi hapa Tanzania

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
13,966
Reaction score
26,220
Mko poa?

Nimebahatika kuishi na jamii nyingi za Kitanzania, na hii ndiyo orodha yangu ya top ten ya makabila yanayoongoza kwa kula chakula kingi hapa Tanzania:

1. Wasukuma
2. Wanyakyusa
3. Wasafwa
4. Wajita
5. Wahaya
6. Waha
7. Wajaluo
8. Wakurya
9. Wangoni
10. Wagogo
 
Kuna jamaa angu msukuma ni poti,jana nikamtembelea kwake,jamaa akarusha nguna kubwa nikajua ni ya watu 8 kumbe ni ya watu wawili,tumeipiga wee ,me nikasanda,mshikaji kiutani akaifyeka ile nguna halafu akashushia na jagi la maji.nikajisemea huyu fala hapa kwake debe la mahindi ni siku tatu tu linakata
 
Kuna msemo wetu TUNAITAGA

"""FUGO""

Mfano

Akashusha fugooo
 
Wanyamwezi ni ndugu zao wasukuma ila cha ajabu hawapo kabisa kwenye list halafu umeweka wahaya kwenye top 5!

Kwanza wahaya ungewatoa kabisa hapo maana ndizi ni uji uliochangamka. Mnyamwezi/msukuma akitumia ndizi kama chakula chake kikuu atajikuta anakula kila baada ya masaa 2, yaani atakula angalau milo 6-8 kwa siku
 
Umenikumbusha siku flani nilimtembelea jamaa yangu flani ni msukuma,ilikua around saa 4 asubuhi, nikakaribishwa mezani hotpot limejaa ndizi nyama,nikapiga fresh tukatoka nje na jamaa yangu kupunga upepo nikajua ile ndio ilikua lunch,kufika saa 7 mchana naona mke wa jamaa anatukaribisha tena mezani kula ugali,huo ugali sasa ulikua mkubwaa kinoma afu walaji tuko watatu,me nikala kidogo nikanawa,huyu jamaa angu na ndugu yake mwingine wanaishi nae hapo kwake walipiga ule ugali mpaka ukaisha.
 
Mko poa?
Nimebahatika kuishi na jamii nyingi za kitanzania, na hii ndio top ten yangu ya makabila yanayoongoza kwa kula chakula kingi hapa Tz.
1.Wasukuma
2.Wanyakyusa
3.Wasafwa
4.Wajita
5.Wahaya
6.Waha
7.wajaluo
8.wakurya
9.wangoni
10.wagogo

Msukuma unga kilo moja hawezi kushiba labda kilo moja apike UJI.

Msukuma Ubwabwa ni kama Appetizer kwa ajili ya kula UGALI.
 
Kuna wasukuma niliishi nao jirani huko chuo, wao bana siku wakipika wali lazima wapike na ugali pembeni, tena ugali mkubwa kweli kweli.. wakimaliza humu yao ya kula wali wanahamia kwenye kula ugali sasa ndo wanajisikia wamekula na kushiba vizuri. 😀

Wanakuambia wali sio chakula cha kumshibisha mtu.
 
Back
Top Bottom