Top 10 ya Makabila yanayoongoza kwa kula chakula kingi hapa Tanzania

Top 10 ya Makabila yanayoongoza kwa kula chakula kingi hapa Tanzania

Mko poa?
Nimebahatika kuishi na jamii nyingi za kitanzania, na hii ndio top ten yangu ya makabila yanayoongoza kwa kula chakula kingi hapa Tz.
1.Wasukuma
2.Wanyakyusa
3.Wasafwa
4.Wajita
5.Wahaya
6.Waha
7.wajaluo
8.wakurya
9.wangoni
10.wagogo
Hi naweza amini, kuna kijana wetu wa kazi alikuwa ananiambiaga akila wali hashibi ili ashibe lazima ale sahani ya kula watu 4. Akila wali lazima atajipikia na kaugali ndipo atalala vizuri. Mwanzoni alipokuja mjini kufanya kazi, ile siku ya kwanza tu tumekula pilau, yeye akala kwa haibu akaenda kulala kudai ameshiba. Usiku bi mkubwa anaamka kwa sauiti ya mtu akilia sebuleni, kwenda sebuleni anamkuta kijana wetu kaloa machozi akilia kuwa ana njaa. Bi mkubwa akamwambia wewe si ulikataa mwenyewe kuendelea kula, vipi au kuna lingine linakuliza akasema hapana. Akaambiwa aende jikoni kujipakulia chakula kilichobaki, akasema anataka ugali, Dogo si akaingia mtamboni mwenyewe kupika, unaambiwa ugali wa kula watu 5 kala yeye peke yake na akaumaliza. Tunasimuliwa asubuhi tulishangaa ila akaja kututhibitishia baadaye kuwa yeye kwenye mlo ni zaidi ya tumuonavyo. Dogo hana mchezo aisee ila ni mchapakazi kwelikweli.
 
Hivi kusifiana kula Wanaume ni sifa pia? Mwanaume anasifiwa kazi sio kula hayo mambo yashapitwa na wakati
Basi wewe si Msukuma au mwanamme wa Kanda ya Ziwa, kule mtu anasifiwa kwa kula hovyo na kulima pamoja na kunuka makwapa. Wanadai mwanamme kazi, muda wowote unatakiwa kunuka kukabiliana na kazi nzito nzito za kufanya.
 
Ikiwa unatumia nguvu nyingi katika maisha ya kila siku badala ya kutumia akili lazima ule sana Ili ufanye kazi nzito..
 
Nando kabila pekee linalopiga kazi ngumu nahalitegemei kulishwa nachakula chakutoka sehemu nyingine. Kwahiyo wanahaki yakula make walimaji niwao
 
Mko poa?
Nimebahatika kuishi na jamii nyingi za kitanzania, na hii ndio top ten yangu ya makabila yanayoongoza kwa kula chakula kingi hapa Tz.
1.Wasukuma
2.Wanyakyusa
3.Wasafwa
4.Wajita
5.Wahaya
6.Waha
7.wajaluo
8.wakurya
9.wangoni
10.wagogo
Kyusa huwa tunapenda sahani ijae tu kuwafidhisha wamama huko.
Huku kuna majogoo yanaliwa km hamna akili nzuri.
Niliwai nunua jogoo 2 nikajua tunakula ukoo mzima,
Nilipewa kibawa tu.
Turiani huko.
Mungu mkubwa niko salama.
 
Kuna jamaa angu msukuma ni poti,jana nikamtembelea kwake,jamaa akarusha nguna kubwa nikajua ni ya watu 8 kumbe ni ya watu wawili,tumeipiga wee ,me nikasanda,mshikaji kiutani akaifyeka ile nguna halafu akashushia na jagi la maji.nikajisemea huyu fala hapa kwake debe la mahindi ni siku tatu tu linakata
Umenikumbusha siku flani nilimtembelea jamaa yangu flani ni msukuma,ilikua around saa 4 asubuhi, nikakaribishwa mezani hotpot limejaa ndizi nyama,nikapiga fresh tukatoka nje na jamaa yangu kupunga upepo nikajua ile ndio ilikua lunch,kufika saa 7 mchana naona mke wa jamaa anatukaribisha tena mezani kula ugali,huo ugali sasa ulikua mkubwaa kinoma afu walaji tuko watatu,me nikala kidogo nikanawa,huyu jamaa angu na ndugu yake mwingine wanaishi nae hapo kwake walipiga ule ugali mpaka ukaisha.
Nilipoona tu title ya uzi nilijua kuwa akina ngosha hapa hatutoboi. Nimecheka sana aisee 😂😂😂

Naam! Msosi (ugali) unapigwa na kazi zinafanyika. Maguvu kama yote. Watu wako fit mpaka 80s huko. Unazalisha chakula chako mwenyewe. Hakuna kuomba omba. Na ukifikiwa na mgeni ni lazima ale ashibe - hata kama ni mpita njia tu.

meza.jpg
 
Mko poa?
Nimebahatika kuishi na jamii nyingi za kitanzania, na hii ndio top ten yangu ya makabila yanayoongoza kwa kula chakula kingi hapa Tz.
1.Wasukuma
2.Wanyakyusa
3.Wasafwa
4.Wajita
5.Wahaya
6.Waha
7.wajaluo
8.wakurya
9.wangoni
10.wagogo
Kwa ushahidi na utafiti upi wakati kila binadamu ana uwezo wa kila kitu tofauti na wengine au ni chuki na ujinga?
 
Kuna jamaa yangu msukuma tulisoma nae chuo sasa mwamba mlikuwa mkiingia kafteria anagonga chapati sita na chai ya maziwa halafu anaweka supu ya samaki baada ya hapo anashushia ndizi za kuiva tano zile kubwa akimaliza anakunywa dasani ile kubwa yote.

Fungakazi sasa kaka yangu alioa msukuma sasa nilipoenda kutembelea ukweni nilipokelewa vizuri maana tulienda na shemeji ( mke wa kaka)

Picha linaanza likaletwa sinia la viazi vimejaa na maziwa kale kandoo ka lita kumi halafu tupo watu watatu mimi nikajua ndio msosi sasa nikala nikashiba wale jamaa walipiga maziwa yote.

Baada ya kumaliza kula tukawa tunacheza karata ilikupoteza muda
Aise baada ya masaa mawili ukaletwa ugali na samaki sangala da mimi niligusa kidogo nikawa hoi wale jamaa waligonga msosi balaa ukaisha.

Baada ya kula nikamwambia shemeji twende home akasema nisubili kwanza eti bado muda wa chakula cha mgeni.

Kufika mida ya saa kumi ndio ukaletwa wali na nyama aise nilijilaumu sana kula viazi vingi halafu shemeji hakuwa ameniambia utaratibu wa kwao kama upo hivyo yani nilikula nyama finyango tatu nikawa nimeshiba.



Nyingine hii hapa kaka yangu huyu ni mtumishi hukohuko usukumani sasa wasukuma walikuwa wanampenda sana hata nilivyokuwa nikitoka likizo ya advance nilikuwa naenda kwake

Sasa sikumoja nipo likizo kwake kaka akawa amealikwa harusini yeye ndio alikuwa mwenyekiti wa kamati ya chakula.

Aise picha inaanza muda wa chai tukaletewa lilelijaba limejaa maandazi mzee wasukuma wanakula sana yani tulikula jaba zima watu wanne mimi nilikula kidogo nikawa nimeshiba nilisubilia muda wa nyama na wali maana nilikumbuka ule utaratibu wa kwao na shemeji

Zile njemba zinajua kukomba nyama hatari utasikia ng'wana juma makubhi! 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kuna jamaa yangu msukuma talisman nae chuo sasa mwamba mlikuwa mkiingia kafteria anagonga chapati sita na chai ya maziwa halafu anaweka supu ya samaki baada ya hapo anashushia ndizi za kuiva tano zile kubwa akimaliza anakunywa dasani ile kubwa yote.

Fungakazi sasa kaka yangu alioa msukuma sasa nilipoenda kutembelea ukweni nilipokelewa vizuri maana tulienda na shemeji ( mke wa kaka)

Picha linaanza likaletwa sinia la viazi vimejaa na maziwa kale kandoo ka lita kumi halafu tupo watu watatu mimi nikajua ndio msosi sasa nikala nikashiba wale jamaa walipiga maziwa yote.

Baada ya kumaliza kula tukawa tunacheza karata ilikupoteza muda
Aise baada ya masaa mawili ukaletwa ugali na samaki sangala da mimi niligusa kidogo nikawa hoi wale jamaa waligonga msosi balaa ukaisha.

Baada ya kula nikamwambia shemeji twende home akasema nisubili kwanza eti bado muda wa chakula cha mgeni.

Kufika mida ya saa kumi ndio ukaletwa wali na nyama aise nilijilaumu sana kula viazi vingi halafu shemeji hakuwa ameniambia utaratibu wa kwao kama upo hivyo yani nilikula nyama finyango tatu nikawa nimeshiba.



Nyingine hii hapa kaka yangu huyu ni mtumishi hukohuko usukumani sasa wasukuma walikuwa wanampenda sana hata nilivyokuwa nikitoka likizo ya advance nilikuwa naenda kwake

Sasa sikumoja nipo likizo kwake kaka akawa amealikwa harusini yeye ndio alikuwa mwenyekiti wa kamati ya chakula.

Aise picha inaanza muda wa chai tukaletewa lilelijaba limejaa maandazi mzee wasukuma wanakula sana yani tulikula jaba zima watu wanne mimi nilikula kidogo nikawa nimeshiba nilisubilis muda wa nyama na wali.

Zile njemba zinajua kukomba nyama hatari utasikia ng'wana juma makubhi! 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Ha ha ha hao watu mpaka unajiuliza huwa wana matumbo ya ziada?
 
Back
Top Bottom