Top 10 ya Makabila yanayoongoza kwa kula chakula kingi hapa Tanzania

Top 10 ya Makabila yanayoongoza kwa kula chakula kingi hapa Tanzania

Mko poa?
Nimebahatika kuishi na jamii nyingi za kitanzania, na hii ndio top ten yangu ya makabila yanayoongoza kwa kula chakula kingi hapa Tz.
1.Wasukuma
2.Wanyakyusa
3.Wasafwa
4.Wajita
5.Wahaya
6.Waha
7.wajaluo
8.wakurya
9.wangoni
10.wagogo
Ukiweza kula makande ya mbena bila kutapika basi utwaeza kula hata kinyesi bila shida
 
Wanyamwezi ni ndugu zao wasukuma ila cha ajabu hawapo kabisa kwenye list halafu umeweka wahaya kwenye top 5!

Kwanza wahaya ungewatoa kabisa hapo maana ndizi ni uji uliochangamka. Mnyamwezi/msukuma akitumia ndizi kama chakula chake kikuu atajikuta anakula kila baada ya masaa 2, yaani atakula angalau milo 6-8 kwa siku
Sisi kwetu hawakuwai kupika ndizi wala tambi kama mlo.Ni mwendo wa wali mwingi sana,ugali,kande ,viazi au mihogo.
 
Nilipoona tu title ya uzi nilijua kuwa akina ngosha hapa hatutoboi. Nimecheka sana aisee 😂😂😂

Naam! Msosi (ugali) unapigwa na kazi zinafanyika. Maguvu kama yote. Watu wako fit mpaka 80s huko. Unazalisha chakula chako mwenyewe. Hakuna kuomba omba. Na ukifikiwa na mgeni ni lazima ale ashibe - hata kama ni mpita njia tu.

View attachment 3376372
Ninachokupendea hujawahi kukataa asili yenu..!!
Kwahiyo hiyo midude ya rangi inaingia tumboni? 😹😹😹

Mkinga mwenzangu kazoea bumunda na ndosa, huo ugali atauweza kweli kuupika na kula?? 🤣😹
 
Kuna jamaa angu msukuma ni poti,jana nikamtembelea kwake,jamaa akarusha nguna kubwa nikajua ni ya watu 8 kumbe ni ya watu wawili,tumeipiga wee ,me nikasanda,mshikaji kiutani akaifyeka ile nguna halafu akashushia na jagi la maji.nikajisemea huyu fala hapa kwake debe la mahindi ni siku tatu tu linakata
😹😹😹
 
Kuna jamaa angu msukuma ni poti,jana nikamtembelea kwake,jamaa akarusha nguna kubwa nikajua ni ya watu 8 kumbe ni ya watu wawili,tumeipiga wee ,me nikasanda,mshikaji kiutani akaifyeka ile nguna halafu akashushia na jagi la maji.nikajisemea huyu fala hapa kwake debe la mahindi ni siku tatu tu linakata
😂😂😂😂
 
Kwa kula huko ni lazima wajenge mashimo makubwa ya vyoo😅😅😅maana mzigo unaoshushwa hapo sio mchezo.
 
Hi naweza amini, kuna kijana wetu wa kazi alikuwa ananiambiaga akila wali hashibi ili ashibe lazima ale sahani ya kula watu 4. Akila wali lazima atajipikia na kaugali ndipo atalala vizuri. Mwanzoni alipokuja mjini kufanya kazi, ile siku ya kwanza tu tumekula pilau, yeye akala kwa haibu akaenda kulala kudai ameshiba. Usiku bi mkubwa anaamka kwa sauiti ya mtu akilia sebuleni, kwenda sebuleni anamkuta kijana wetu kaloa machozi akilia kuwa ana njaa. Bi mkubwa akamwambia wewe si ulikataa mwenyewe kuendelea kula, vipi au kuna lingine linakuliza akasema hapana. Akaambiwa aende jikoni kujipakulia chakula kilichobaki, akasema anataka ugali, Dogo si akaingia mtamboni mwenyewe kupika, unaambiwa ugali wa kula watu 5 kala yeye peke yake na akaumaliza. Tunasimuliwa asubuhi tulishangaa ila akaja kututhibitishia baadaye kuwa yeye kwenye mlo ni zaidi ya tumuonavyo. Dogo hana mchezo aisee ila ni mchapakazi kwelikweli.
😂😂😂😂😂
 
Nimecheka sana!! 😹😹
Wasukuma kazi iendelee nyie kuanzia namba 1-20 mkae nyie…!!
 
Wakienda chooni huwa wanatoa mzigo nusu ndoo bila shaka.
 
Mkuu 1-10 ilipaswa kuwa ni wasukuma tu, halafu 11 na kuendelea ndo wafuatie wengine.
 
Mkuu 1-10 ilipaswa kuwa ni wasukuma tu, halafu 11 na kuendelea ndo wafuatie wengine.
 
Kula chakula kingi kinatokana na mambo mengi sana miongoni mwao ni aina ya kazi lakini upatikanaji wa chakula
Kwa mfano makabila yote uliyotaja ni watu wa kazi kazi, sasa mtu analima nusu heka kwa siku ulaji wake utalinganisha na mtu anayewaza kwenda kunywa kahawa asubuhi huku akibishana kuhusu simba na yanga?

Alafu ukiona chakula kinapikwa kingi ujue pia ndani kipo kingi mimi sio miongoni mwa kabila tajwa lakini toka nakua tunaambiwa wakati wa kula sharti chakula kibakie hvyo lazima kipikwe kingi.

Kuna makabila ni mavivu sana mtu msimu mzima analima robo heka huk ana familia na sio mfanyabiashara maeneo mengine anakodisha kisa hataki kazi ngumu.

Waacheni na maisha yao kwani wanakuomba pesa ya kununulia hvyo vyakula?
Woyooooo!!!
 
Bila wakunyumba kuwepo ktk list, ingekua batili.
Tena ilitakiwa tuwepo Top 5 hapoo, sisi kula sana ni humu tyuuh,

Nimekumbuka siku nimeenda KFC, nilicho agiziwa na kilicholetwa, nkaona huu utani, nisiongeze kingine cha tofauti ili nishibe vyedii.
Mwili haujengwi kwa mawe, ni Msosi. 😂😂😂😂
 
Nilihisi tu kwenye orodha lazima Wasukuma watashika namba 1.

Ila sina hakika kama ni ukweli unaoungwa mkono na tafiti …
Nako kutokula siyo sifa, watu wanatumia energy kubwa katika katika shughuli zao za kiuchumi lazima wale chakula cha kutosha. Nature ya kazi zao Hauwezi ukawlfananisha na wale wanasubiri wazungu wawainyeshe picture za wanyama au njia za kwenda milimani au wanaosubiri uwape mchongo wakuibie au wakudhurumu
 
Back
Top Bottom