msukuma fekero
JF-Expert Member
- Aug 12, 2017
- 2,423
- 3,270
Nakuunga mkonoHiyo namba 8 ikawe namba 2
Nakuunga mkonoHiyo namba 8 ikawe namba 2
Hahahaaa! Mzee mwenzangu si unajua tena mambo ya utani , dont take it serious.Jamani hata wewe mzee mwenzangu unatushushua? Makubwaaaa!
Sisi ni watani wa kila mtu...
😹😹😹 Wasukuma mi nawapenda sana mna vituko halafu mnajiamini..!!Kuhusu muziki wa hiyo midude ya rangi muulize Kalpana atakupa mkanda mzima 😂😂😂
Kuupika ugali wa Kisukuma ni mtihani. Eti upike ugali wa njemba 10 zimetoka kulima huko siku nzima? Aaaa wapi! Mkinga mbona utakumbuka kurudi Kariakoo mapema tu?
Alikuja shemeji wa Kinyaki mpaka akawa analia yaani nikawa naingia jikoni kumsaidia; au nambembelezea kwa mawifi zake ili wamsaidie. Akaja kuletwa binti mmoja Mzaramo na mpwa wangu mmoja hivi ohooo! Huyu aliondoka bila kuaga. Kuja kumbananisha akaniambia anko hapo kwenu naweza kufanya kila kazi isipokuwa tu kupika ugali wa wanaume...
Vu bin vu ni mwenyewe nikapeleka pisi ya Kichaga kipindi fulani hivi (Mama E usicheke!). Yenyewe ikawa smart ilipoambiwa kupika ugali ikamuita chemba wifi yake mmoja ikamkatia 50K na mkataba ukafungwa kuwa haitakaa ipike ugali hasa wa wanaume. Rushwaaaaaaa!
Mpwa wangu Aaliyyah sijui amejiandaaje masikini na mtanange huu wa kupika ugali wa kuliwa na wanaume wa Kisukuma maana ugali ukiwa mlaini hata kiduchu tu hawali. Ni lazima uwe mgumu kama jiwe, uive vizuri na uwe wa motooooooooo!
➡️➡️➡️ Akanaye asili yake huyo ni mtumwa 📌📌📌
Najua mzee mwenzangu. Tunataniana tu hapa na kucheka japo bado nakumaindi sana kwa kunikatalia kuuliza swali langu kule kwa waziri mkuu wako 👐😂Hahahaaa! Mzee mwenzangu si unajua tena mambo ya utani , dont take it serious.
Kabisa hapo nawapongeza.
Kuna WUWA kaliwona hapo kwenye mujiii wa mzee wakoo 😁😹😹😹 Wasukuma mi nawapenda sana mna vituko halafu mnajiamini..!!
Mzee aliwahi kumpangisha msukuma ana mke wake wakianza kugombana wanashikiana mpk visu… nilivyorudi home kutoka shule si akamfata mzee anataka kuoa kwenye nyumba yake kuna ua kaliona..!! 🤣
Mzee akabaki anamshangaa kwanza bado nasoma halafu yeye mkubwa…!! Wasukuma mna nchi yenu🤣
Unawekwa ugali mlima wanakula wanaume huku mwingine umetunzwa pembeni au jikoni unapigwa mduara pale ugali unaliwa wengine wakiwa wamevua mashatu..ugali ukiisha mdogo kabisa kuliko wote anaagizwa genda ubhabwile bhachongeshe ubhosima inaletwa nguna nyingie kama ile ya mwanzo ujitani rahaKuna msemo wetu TUNAITAGA
"""FUGO""
Mfano
Akashusha fugooo
Hahaha! Noma sana..Kuna jamaa angu msukuma ni poti,jana nikamtembelea kwake,jamaa akarusha nguna kubwa nikajua ni ya watu 8 kumbe ni ya watu wawili,tumeipiga wee ,me nikasanda,mshikaji kiutani akaifyeka ile nguna halafu akashushia na jagi la maji.nikajisemea huyu fala hapa kwake debe la mahindi ni siku tatu tu linakata
Tafsiri ya chakula kingi ni nini?Mko poa?
Nimebahatika kuishi na jamii nyingi za Kitanzania, na hii ndiyo orodha yangu ya top ten ya makabila yanayoongoza kwa kula chakula kingi hapa Tanzania:
1. Wasukuma
2. Wanyakyusa
3. Wasafwa
4. Wajita
5. Wahaya
6. Waha
7. Wajaluo
8. Wakurya
9. Wangoni
10. Wagogo
Tafsiri ya chakula kingi ni nini?
Nakazia hapa..Hapo WAHA unawaonea nimekaa sana na WAHA sio walaji sana.
Aiseee!!!
Wala haihusiani na idadi ya watu, ukifuatilia hapo karibu makabila yote aliyoyataja ni wazee wa kazikazi.Wachaga, wanyamwezi umewaacha mbona.
WApo kwenye top 5 ya idadi ya watu wengi na chakula pia watakuwa wanakula kwa wingi.