Top 3 GOAT Tanzania Rappers, Serikali itambue mchango wao ikibidi watunukiwe Phd

1. Nitajie wimbo wa Prof. Jay ambao anaimba.

2. Je, unajua kwamba kurap si lazima uwe unarap kama Fid Q, bali kuna delivery styles tofauti.?
 
1. Nitajie wimbo wa Prof. Jay ambao anaimba.

2. Je, unajua kwamba kurap si lazima uwe unarap kama Fid Q, bali kuna delivery styles tofauti.?
Ni sahihi kumuita prof Jay Mwanahiphop/bongofleva bora, Ila si sawa kumuita rapper bora. Mfano nyimbo kama zali la mentali,kamili gado,starehe,nikusaidieje n.k unaweza kunipa 'mstari kwenzi' hata mmoja hapo? Ni nyimbo za hiphop/bongo fleva za kawaida sana sio pure rap.
 
Itanibidi nikafanye sala ya toba kwa kusoma uzi uliojaa kufuru dhidi ya wakali wa muda wote wa Tanzanian Hiphop.
 
Kama kwenye list umemuweka Songa na young killer ila hakuna chindo,fazza Nelly, Hashim dogo .Jay Mo,Mwana FA ,Joh Makini ..Kala Pina,Afande sele.. Inspector Aroun...mkuu Nina mashaka na uelewa wako wa Rap Game
Mwana FA, Inspector wanaimba bongo fleva sio rappers, Chindo, fazza Nelly,Joh makini wanafanya hardcore hiphop, sio pure rappers. Jay mo hana uandishi, ila ana flow, ila anaimba zaidi bongo fleva tangu enzi za cheza kwa step.
 
Fid hana mchango wowote Kwa jamii
 
Huyo Dizasta vina ni mchumba na vimistar vya kuunga unga.... Hapo mkali Fid... Walau huyo Songa yupo vizuri kwenye story telling
Mpe sikio vina sio shoga kama wote ni kichwa haswa
 
Tujifunze kutofautisha, Prof Jay, Afande sele,Juma Nature, Mwana FA sijui kina Jay mo hao ni pioneers wa Bongo fleva sio rappers. Rapper pekee mwenye misingi ya Rap wa kutokea kitambo hicho ni Fid q angalau na Sugu, ila sugu ni hiphop zaidi sio speciffically rapper.
 
Hizo nyimbo ulizotaja ni story..focus ya uandishi inakuwa tofauti na nyimbo za mtindi mwingine. (Kasoro hiyo starehe. Professor hana wimbo unaitwa Starehe.)
Ushawahi kuandika hata verse moja?

Story telling inategemea zaidi mpangilio wa mawazo kuvutia hadhira kuliko hizo dope bars.

Nyimbo za kimtaa, hustle na starehe ndiyo hufocus kwenye mistari konzi ili hadhira iendelee kuwa engaged na entertained.

Kama unamsikiliza Tupac, utajua Keep your head up au Brenda gotta Baby hazina mstari wowote konzi. Yet ni Ngoma kali kabisa.

Pia, kuchanganya ladha kidogo, hakumfanyi rapper aache kuwa rapper. Tunzingatia catalogue yake kwa ujumla.

Hata Eminem ana Ngoma kama Hailie anaimba kabisa. Je, na mara nyingi anaimba bridges kwenye nyimbo zake. Ref: Not Afraid na So bad. Je, tuseme Em si rapper mkali tena kwa kuwa huwa anajiimbisha sometimes?
 
Misingi gani ya rap ambayo Fid Q anayo ambayo Professor Jay, Afande Sele au FA hana?
 
Acha izo
Hv Kuna mtu aliye Fanya vzuri kama Chidy Benz au sababu mnamuona ana shoti
 
Mpe sikio vina sio shoga kama wote ni kichwa haswa
Rapper inatakiwa uwe mkali kwenye flows... Sasa yeye flows zake zimepoa habadiliki... Rappers Bora 5 wa muda wote, fuatilia flows zao ndo utajua kama huyu jamaa Yako anajua ku-rap kweli au anaunga vimistari.
Tupac, Notorious BIG, Jay Z, Nas Eminem

Huyu jamaa Yako anazumbaa sana kwenye beat Hana ladha kabisa... Kuandika anajua but Hana flows nzuri na Yuko predictable/ dormant
 
Wazee vipi kuhusu Albert Mangwea RIP na Godzilla RIP
Hamna hata mmoja anaingia kwenye iyo list ya The best rappers?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…