Top 3 GOAT Tanzania Rappers, Serikali itambue mchango wao ikibidi watunukiwe Phd

Hapo kwa Tupac, unajua kwanini sometimes Eminem, Kendrick Lamar,Nas hata Lil Wayne wanatajwa mbele ya 2pac ila best Hiphop anabaki kuwa 2pac na BIG?
Mbona ROSTAM wanafanya story telling lakini humohumo kuna dope bars? Same to fid q, Songa n.k

Prof na wengine kama Afande sele, Jay mo n.k wako vizuri kwenye story telling lakini sio rap.
 
Inaonekana umezaliwa around mwaka 2000, jaribu kupata nafasi ya kusikiliza kazi za wasanii kabla hujazaliwa.
Pfofesa Jay alifanya wazazi wetu waanze kusikiliza muziki wa kufoka foka baada ya kusikia wimbo wake wa chemsha bongo.
Sugu alianza kuimba harakati zilizokosoa maovu ya Serikali kupitia Album yake ya Muziki na Maisha.

Hiyo ni mifano michache tu ya wasanii wanaopaswa kuwa kwenye kundi la G.O.A.T, hao uliowataja ukiondoa fid q hawastahili kuwa kwenye hilo kundi.

Mimi binafsi naona kama kuna wasanii watatu wanapaswa kupewa tuzo za u GOAT kwenye sanaa ya muziki Tanzania ni :
1. Profesa Jay
2. Sugu
3. Afande Sele
 
Sugu duh!
 
Mkuu ukimsikiliza Kendrick Lamar unaona amepoa au hajapoa? Hao kina BIG na Jay z wanafanya hiphop zaidi, ila kwenye rap hapana
 
Misingi gani ya rap ambayo Fid Q anayo ambayo Professor Jay, Afande Sele au FA hana?
Mwana FA huyuhuyu aliyeimba bado niponipo, mwanaume suruali, mabinti? Nitajie punchline moja tu kwenye hizo nyimbo! Prof jay nineshazungumza hapo juu, Afande sele hao ni bongo fleva
 
Kama unaongelea bilingual naungana na wewe ila kama ni kuongelea wasanii ambao style yao ilibamba na kufanikiwa kufikisha message kwa jamii! Huwezi muacha Jay hapo!
 
Acha izo
Hv Kuna mtu aliye Fanya vzuri kama Chidy Benz au sababu mnamuona ana shoti
Chid huyuhuyu wa Chaguo langu? Mpaka kuchee? Ni mkali ila sio mwandishi wala rapper mkali. Ni bongofleva mkali
 
Mkuu ukimsikiliza Kendrick Lamar unaona amepoa au hajapoa? Hao kina BIG na Jay z wanafanya hiphop zaidi, ila kwenye rap hapana
Yeah nakubaliana na Ww kuhusu Jigga na Big kutokuwepo kwenye rap lyricism haswa but mantiki yangu ilikua kwamba mkali wa rap anatakiwa awe na flows nzuri zisizochosha.....

Kendrick anajua but kwangu dizain flan simkubali.... But frankly speaking huyu dizasta vina humwoni km Hana flows nzuri na anachosha?
 
Wazee vipi kuhusu Albert Mangwea RIP na Godzilla RIP
Hamna hata mmoja anaingia kwenye iyo list ya The best rappers?
Mamgwea ni mkali, ila kidogo yupo kwenye Bongofleva, sio mwandishi mzuri na hana mistari kwenzi ya rap. Anajua kuflow tu.Godzilla hana tofauti sana, Ila ni best freestyler
 
Nimeshatolea ufafanuzi hapo juu mkuu, Hao ni wasanii wa Bongofleva/hiphop kiasi, Ila sio Rappers. Rappers wengi wana IQ kubwa na uandishi wao upo more complicated
 
Mwana FA huyuhuyu aliyeimba bado niponipo, mwanaume suruali, mabinti? Nitajie punchline moja tu kwenye hizo nyimbo! Prof jay nineshazungumza hapo juu, Afande sele hao ni bongo fleva
Nilikuambia huwezi judge ubora wa msanii kwa nyimbo mbili au tatu.. angalia catalogue yake nzima..
Pia, kwako punchline ni nini?

Kwa mfano FA anaposema 'umimegewa demu wako nawe tafuta mnyonge ummegee, haipunguzi maumivu inarudisha hadhi ya kiume'. Je, hiyo ni punchline au siyo?
 
Catalogue zao haziwaonyeshi kuwa rappers,na waandishi bora, bali zinawaonyesha kuwa wasanii wa bongofleva. Tofauti na Catalogue ya Fid q
 
Kama unaongelea bilingual naungana na wewe ila kama ni kuongelea wasanii ambao style yao ilibamba na kufanikiwa kufikisha message kwa jamii! Huwezi muacha Jay hapo!
Jay ni bilingual pia, Zamani alikua ana rap kwa English..isikilize fascinating rhythms ngoma ya 1997
 
Nimeshatolea ufafanuzi hapo juu mkuu, Hao ni wasanii wa Bongofleva/hiphop kiasi, Ila sio Rappers. Rappers wengi wana IQ kubwa na uandishi wao upo more complicated
Tupe tofaouti ya rapper na hip hop kiuimbaji huyo songa nae alishafanya story telling nying tu. Na kuimba kabisa, mimi nafikiri wewe umedata na ile style tu Stanza ambayo imetumiwa sana na Tamaduni, at list ungemueka NAsh Maalim juu kuliko songa ningeelewa lakini art aliyonayo prof hasa kwenye kutembea clean kwenye beat na utunzi hafananishwi hapa bongo labda marehemu Ngwair angekuja kumfikia. Prof ni rapper ni mtunzi na entertainer vile vile ni complete package inaweza kushindanishwa kwenye nyanja zote za rap na hiphop sanaa hio. Ndio msanii nimewahi kuhudhuria show yake miaka hio akichana nusu verse anasikia mashabiki then dk nzima akijakuendelea anaikuta nyimbo katikati ya verse ya mwisho na haruk mstari na hapo ni beat tupu anaiiunga. Mpeni maua yake jamaa anakipaji na hakuna mwandishi wa kumgusa
 
Bongo wanahiphop watatu wa muda wote ni
1. Jay
2. Fid
3. Langa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…