Hizo kurasa 33 hazijasema Bandari inakodishwa Kwa miaka mingapi Mkuu?
 
TPA haina uwezo wa kulisemea jambo hili , acheni kujipendekeza , hili msemaji wake ni lazima iwe serikali yenyewe .

Kwanza nyie TPA kila siku mnatimuliwa na wanawekwa watu wapya mnawezaje kuwa wasemaji wa Jambo la Kitaifa ?
Uelewa wako mdogo katika masuala nyeti. Wewe fanya kazi ya kuleta mada za Mbowe na umbea mwingine kuhusu CHADEMA.

TPA ndio serikali yenyewe. Kutimuliwa hata waziri mkuu anaweza kutimuliwa na akachaguliwa mwingine kisha akapitishwa na bunge.
 
Haina ukweli wowote hii habari.
 
Uafrika hasa utanzania ni LAANA
 
TPA ni sawa tu na kiranja wa zamu yeye kazi yake ni kutekeleza na kusimamia kinachoamuliwa pale bungeni na bunge la ccm, na wakikaa vibaya utasikia wametumbuliwa
 
Like ya pili ni ya kwangu. Watanzania tumezoea sana mipasho isiyoumiza kichwa, tuna uvivu wa kutafuta maarifa ule uvivu wa kusoma.

Pia ni siasa zile zile za masalia wa marehemu JPM wanaotafuta sababu ya kuipaka matope awamu ya sita, ni watu hawana kabisa umakini wa kuweka taarifa zao mitandaoni.
 
serikali itoke kuja kulisemea hili hizi barua za janjajanja hatuzitaki
 
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Serikali imepanga kuipa kampuni ya DP World ya Dubai kandarasi ya uendeshaji wa shughuli za Bandari ya Dar es Salaam kwa muda wa miaka mia moja ni upotoshaji unaofanywa kwa makusudi na watu wenye nia ovu.

Katika taarifa yake, TPA imeeleza kwamba Azimio la Bunge linahusu mkataba ambao Serikali ya Tanzania inaingia na Serikali ya Dubai wenye ukomo wa miezi 12 kwa ajili ya kutoa nafasi kwa Serikali ya Tanzania kujadiliana na Serikali ya Dubai kuhusu maeneo ambayo Serikali hizo mbili zinaweza kushirikiana katika uboreshaji na uendelezaji wa sekta ya bandari nchini.

“Ushirikiano wa Dubai na Tanzania una lengo la kuongeza ufanisi wa huduma za bandari nchini, kukuza ajira za Watanzania na kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kupitia uwekezaji kwenye baadhi ya maeneo ya Bandari ya Dar es Salaam, maeneo huru ya kiuchumi na viwanda (Special Economic and Industrial Zones) kwa kujenga viwanda na uwekezaji katika mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka Bandari ya Tanzania kwenda nchi za jirani ambazo zinatumia bandari zetu,” imesema TPA.

Aidha, TPA imeeleza kuwa jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuvutia uwekezaji nchini hususani katika maeneo ya bandari, zinalenga kumaliza changamoto za muda mrefu ikiwemo ucheleweshaji wa meli, mizigo na kukosekana kwa ufanisi.
 
Wapiga kelele wamejaa Tanzania hii, wengi uwezo wao mdogo wa kuelewa kinachozungumzwa na pia wavivu wa kutafuta maarifa.
 
Hivi unawezaje kukuza uchumi na kuongeza ajira kwa kumpa kazi mgeni??

Kwani hizo ajira hawewezi kuzitoa Sasa mpaka waje hao watu Toka Dubai??
 
Kama TICS hawakufanya na hakuna aliyeweza kuwagusa, unauhakika gani hao DP watafanya? Kwani Tanzania si ile ile na watu ni wale wale? Why then kama uwekezaji haujaleta mafanikio mbadilishe mvinyo wakati chombo ni kile kile?

Hiyo ni ego na katu hamwezi kutudanganya kwa maneno yenu haya yenye kuleta maswali kuliko majibu...Kama ni uwazi, tenda ya kuiboresha bandari iliwekwa linj wapi? Why DP na siyo kampuni nyingine? Je si rushwa hii ya wazi wazi? Unatofauti gani mtindo huu na ule wa TICS, acheni hizo!
 
Sio bandari ya dar tu, ni bandari zote
 
So wanaingia mkataba ili wajadiliane kwa miezi kumi na mbili!!? Sijawahiona watu wakiingia mkataba wa majadiliano! Siyo majadiliano ndiyo huzaa mkataba!? Au sijaelewa🙄
 
Ingekuwa ni vyema tungeibinafsisha Serikali kwani ndio imeshindwa kuwasimamia watu iliyowaajiri yenyewe.
Huko kwingine ni kutapatapa tu na kuongeza matatizo
Huu ndo ukweli.watu wanajitoa tu ufahamu kwa maelezo mengi ambayo hayana maana.
 
Sijaelewa na sitoelewa na siko tayari kuelewa na sina nia ya kuelewa hadi mafisadi wote wa bandari (wa leo na wa zamani) wawajibishwe na kufilisiwa hata kama wako makaburini.

Eti serikali 2 zinaingia mkataba wa miezi 12 wa kujadiliana tuuuu.... siyo wa uwekezaji [emoji85].

Maswali:-

1. Siku hizi kujadiliana lazima ni kwa mkataba?[emoji86].

2. Thamani ya mkataba wa kujadiliana ni shg bilioni mia ngapi?[emoji3517].

3. Thamani ya mkataba halisi wa uwekezaji ni shs trilioni mia ngapi?[emoji2089].

4. Mkataba wa kujadiliana ukifa nani anatoa fidia za gharama za mkataba wa kujadiliana ili fedha za walipa kodi zisipotee bure?

5. Kama nchi tumeshindwa kabisa kabisa kuendesha bandari yetu?

6. Lazima Mwarabu ndiyo aje atuendeshee bandari yetu?

7. Mashariki ya Kati inapata nguvu kubwa nchini awamu hii kuliko Asia, Ulaya na Americas. Kila awamu ina muelekeo wa upepo wake?

8. TPA haina wasomi wabobezi wa shipping industry? Kama wapo je, wanakwama wapi na nini?

9. Kwanini tusimpe rais PK aendeshe bandari? Au tutakosa mianya ya upigaji? Mbona Tz iliwapa Wamisri kujenga Bwawa la kufua umeme? Haijalishi hata kama PK ataingiza ujuzi toka ughaibuni lakini si tumempa Mwana EAC mwenzetu na Mwafrika mwenzetu? Ni miradi mingapi ya Waarabu, Waasia, Wazungu na Wamarekani wametupa Watz tuwaendeshee huko makwao? Kwani si tumesoma kwao huko huko mitaala yao hiyo hiyo hivyo tuna ujuzi kama wao.

10. Hakuna atayenibadilisha kuamini kuwa shida KUU za TPA ni 4 tuuu... 1) Ufisadi 2) Siasa 3) Utitiri wa taratibu 4) Utitiri wa taasisi ktk utendaji wa shughuli za sekta ya bandari.

11. Hizo zilizoko namba 10 ndizo hata akija Malaika toka Mbingu ya 2 kuendesha TPA atazikuta kama ndizo tatizo na ndizo atakufa nazo ili afanikiwe kupata tija.

12. Wanasiasa waondolewe (kuwe na zero rate ya wanasiasa) kwy kila hatua ya mikataba hii kuanzia no.1 ktk mfumo-rasimu wa siasa za nchi hii na ktk mfumo wa utumishi wa umma.

13. Ikibidi, bandari iwe chini ya Ikulu. Yaani Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ziwajibike Ikulu kwa Mhe. Rais badala ya waziri. Wizarani kuna mianya mingi ya ukengeufu.

14. Hiyo no.13 pakitokea ufisadi basi ni wazi kuwa ofisi kuu ya nchi ndiyo itawajibika.

15. Taasisi nyingi JMT (Tanesco, TRC, Kiwira, ATCL, TANAPA, SON GAS, MNH, TTCL, TAZARA, TPDC nk) ziliingizwa kwenye mpango kama huu wa TPA lakini baada ya wawekezaji kuondoka zimerudiwa na kansa ile ile ya ufisadi, siasa, urasimu, wasimamizi (wapishi) wengi na zingine zimefikwa na mauti kama UDA, TACOSHILI, TIPER.

NB.
Mpango huu wa kuwapa Waarabu kuendesha baadhi ya vitengo vya bandari kama ni wa kisiasa (kisirisiri) kutafuta fedha za 2025 basi ni bora JMT isiwe na chaguzi mama atawale hadi kifo maana chaguzi kumbe zinaiponza nchi.


Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…