TPDC yaingia mkataba na Kampuni ya Uingereza ya Baker Botts kwa ajili ya ushauri wa Kisheria

TPDC yaingia mkataba na Kampuni ya Uingereza ya Baker Botts kwa ajili ya ushauri wa Kisheria

Zile zama za makampuni ya nje kupiga hela kwa mgongo wa ushauri zimerudi.

TPDC imeingia mkataba ya kampuni ya Uingereza za Baker Botts kwa ajili ya ushauriwa kisheria kwenye mikataba ya gesi...
Duh kazi iendelee kweli
 
Mkuu samahani nami naomba MUNGU anifungulie ulichokiona wewe...
Ila Kwa sasa hivi naona Tanzania hamna wanasheria wa “Mafuta na Gesi” unajua sheria zinatofautina...Sheria ya Mafuta na Gesi na Mikataba Watanzania wangapi wanaijua hii?
...
Well, hapa nataka kukubaliana nawe Mambo kadhaa Ila with qualifications,.

Wanasheria wanaojua masuala ya oil and gas wapo tena wana elimu ya vyuo vya nje maana hapa kwetu hatutoi hii course.

Tatizo lililopo ni uzoefu wa offshore drilling especially ya kiwango hicho Cha huu uwekezaji.

Nasema haya Sababu wengi tunafanya hizi kazi lakini inapokuja kuwa na utaalamu wa kuwa consultant wa aina ya mikataba na vifungu vya muhimu vya kuangalia kwenye hii mikataba hapo huwa ni mtihani sababu kwetu sisi hii ni sekta mpya sana ambapo tusipokuwa makini tutaingia mikataba mibovu sana Kama ambavyo tuliingia mikataba ya madini.

Unajua kosa lililofanyika kwenye mikataba ya madini ni kwamba tulilazimisha kutumia wanasheria wetu ambao kwa kipindi kile hawakuwa na uzoefu tukaishia kuingia mikataba mibovu sana.

Unajua kila sekta Ina namna ya kuandaa mikataba yake na aina ya vifungu vya muhimu vinavyopaswa kuwepo sasa sio kila lawyer anajua kila aina ya mikataba hata mikataba ya construction Ina aina yake ya vifungu Kama Mambo ya liquidated damages ziweje na zitalipwa wakati ikitokea nini? Sasa usipokuwa na utaalamu utaingiza taifa mkenge.

Hao no consultant na wanashirikiana na local firm of lawyers inaitwa Apex Attorneys sasa ukiweka hivyo Ina maana tunayemtegemea hapa ni Hawa Apex Attorneys Ila hao wazungu watapokea maelekezo na wwtatumia utaalamu wao kunegotiate na katika hiyo wao wanashauri TGNT ambao wao ndio wanaonegotiate ni team inayoundwa na serikali.

So hao consultant hawanegotiate Ila wanaishauri team yetu ya negotiation wakishirikiana na Apex Attorneys ambao ni watanzania na kumbuka negotiation inaongozwa na Prof Kabudi.

Kuna vitu watu wanapotisha.
 
Makamba hafai kwa lolote serikalini, asiuhadaa umma wa watanzania. Hakuna kitu kitabadilika chini yake zaidi ya kuongezeka kwa matatizo. Acha aendelee kuuficha ukweli ila muda utaweka bayana ndipo huyo aliyembeba atamtua kwa uzito atakao mpa.
Mwache mwenzio afanye kazi, aliyemteua ndio anajua umuhimu wake, majungu hayasaidii, leo Makamba angetangaza kupanda bei za mita bila kumsikia mama aliagiza, ingekuwa balaa kwake, mnamfanya mtu asijiamini!
 
Ina maana wanasheria wetu hawana uwezo

Ova
Offshore drilling sio kitu rahisi na unajua ukweli ni kwamba Tanzania hakina chuo kinatoa course ya oil and gas au Masters, wengi waliosoma wameaoma UK au Marekani.

Offshore drilling ni kitu kipya Kama ilivyo kwa maengineer wanalazimika wasome inapokuja kitu kipya Kama 5G au kwenye IT nk sio kitu unakivamia tu.

Tulijiingiza kwenye mikataba ya madini bila kujua huwa inakuwaje ndio maana tukajikuta tunapigwa maana tulitumia local lawyers ambao hawakuwa na utaalamu wa mikataba ya madini.

All in all kutumia consultant wa nje ni Jambo la kawaida sio kwenye hii mbona miradi mingi sana tunatumia international consultant?

Kimsingi it works like this; huyu international consultant atafanya kazi kwa ushirikiano na Apex Attorneys ambao ni local firm of lawyers, ambao kwa pamoja Wana kazi ya kuishauri TGNT ambayo ni negotiation team ya Tanzania kwenye mazungumzo ya kuandaa mkataba wa offshore drilling na mwekezaji.

So wao watakuwepo kwenimajadiliano Ila wao hawajadili kitu Bali wanakuwa wanasikiliza majadiliano na kumshauri team yetu kipi wakubali na kipi wakatae na kinachokubaliwa kiwe vipi kulingana na utaalamu wao maana wamefanikisha makubaliano katika nchi kadhaa na miradi imeenda vizuri.

Kumbuka team ya majadiliano inaongozwa na Prof Kabudi wao ndio wanaonegotiate.
 
Zile zama za makampuni ya nje kupiga hela kwa mgongo wa ushauri zimerudi.

TPDC imeingia mkataba ya kampuni ya Uingereza za Baker Botts kwa ajili ya ushauriwa kisheria kwenye mikataba ya gesi.
...
Je, Prof. Palamagamba Kabudi ambaye ni Mwandani wa Rais wa ushauri na majadiliano ya mikataba ya kimataifa amehusishwa? Au naye tayari kama Nimrod Mkono ameishapigwa kwa mkono wa mbwa (ameishalambishwa asali ya Tabora yenye Nicotine ya Tumbaku)?
 
Hivi Tanzania bado hatuna kampuni zenye uwezo wa kutoa ushauri wa kisheria hadi tutoe Ulaya?
Tunayo kampuni yenye ofisi hadi barani Ulaya, ni "Mkono & Company Advocates.
Kila siku tuna waambia ng’eng’e ndiyo ufunguo wa kila kitu, mtumishi wa serikali unaingia kwenye ‘negotiation’ wakati ng’eng’e cheche lazima upigwe tuu alafu wananzengo wahakuelewi, afadhari TPDC wamevunja ukimya!!
Sasa hapo ndiyo wazungu hawamtakagi Prof. Kabudi kwasababu wanasema anawapaga shida ya kubeba Dictionaries hadi 3.
 
Kila siku tuna waambia ng’eng’e ndiyo ufunguo wa kila kitu, mtumishi wa serikali unaingia kwenye ‘negotiation’ wakati ng’eng’e cheche lazima upigwe tuu alafu wananzengo wahakuelewi, afadhari TPDC wamevunja ukimya!!
Unafikiri wajapan au wachina wakiwa katika negotiations na mabeberu wanajali hilo ng'eng'e, na sio lazima ujue ng'eng'e katika haya mambo unaweza kutumia mkalimani, kiingereza is overated na wanaoburuzwa na hiyo lugha ni maskini tuu wasiojiamini, manchi kama China au Russia wakija mezani ni kirusi au kichina tuu ni juu yako kutafuta mkalimani ili uwaelewe
 
Zile zama za makampuni ya nje kupiga hela kwa mgongo wa ushauri zimerudi.

TPDC imeingia mkataba ya kampuni ya Uingereza za Baker Botts kwa ajili ya ushauriwa kisheria kwenye mikataba ya gesi.

Hivi Tanzania bado hatuna kampuni zenye uwezo wa kutoa ushauri wa kisheria hadi tutoe Ulaya?


View attachment 2095378

Wanasheria wote hawa wabobevu tulionao bado tunahitaji ushauri toka nje? Mbina wakina Kabudi walinegotiate mikataba mizuri ya madini bila kusaidiwa na watu wa nje?

Kweli tumerudi Misri ufisadi kwa kwenda mbele.
 
Kila siku tuna waambia ng’eng’e ndiyo ufunguo wa kila kitu, mtumishi wa serikali unaingia kwenye ‘negotiation’ wakati ng’eng’e cheche lazima upigwe tuu alafu wananzengo wahakuelewi, afadhari TPDC wamevunja ukimya!!
Kwani Wachina watakaotaka kununua/kuwekeza kwenye gesi watakuja ng'eng'e?
 
Back
Top Bottom