TRA: Hatuhusiki kwa namna yoyote ufungaji wa 'The Cask Bar' jijini Mwanza

TRA: Hatuhusiki kwa namna yoyote ufungaji wa 'The Cask Bar' jijini Mwanza

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuujulisha Umma kuwa, haijahusika kwa namna yoyote na ufungaji wa Bar ya THE CASK iliyopo Jijini Mwanza.

Tunaomba wahusika na Umma wawasiliane na Mamlaka husika juu ya jambo hilo.



-
Pia soma
hao TRA si watulize boli hata wao. Kwani lazima watoe tamko? Km ni taasisi ya serikali imefunga lazima kuna sababu, sisi wengine kinatuhusu nini km siyo kiherehere? Hiyo Cask bar inawahusu nini watanzania mpaka iwe mjadala humu? Tumekosa kabisa kazi za kufanya kiasi hiki? Mtu ameiibia serikali mnakuja huku kumtetea, watu wamekuwa wa hovyo kabisa utafikiri wanaumwa.
 
Hii issue kafanya Amos Makala...

Ni mtu wa siasa chafu za kulipiza kisasi baada ya bwana mmoja kuweka bango la OKOA BANDARI katika bar hiyo
Nashangaa Sana mshamba Makala kuitwa wa mjini
Surayake vaaji yake ongeajiyake ni vyakishamba saaana
 
Utawala wa nchi unayumba.
Wasiojulikana wamerudi.
Hii ni tuhuma kubwa sana anayehusika awajibishwe haraka
 
Inawezekana ujinga huu wamefanya viongozi wa hapo Mkoani Mwanza, ikiwa ni jitihada zao za kujipendekeza kwa mteuzi wao.
TRA kutolea tamko la kukana upuuzi huu, kunawaumbua viongozi hawa.
 
hao TRA si watulize boli hata wao. Kwani lazima watoe tamko? Km ni taasisi ya serikali imefunga lazima kuna sababu, sisi wengine kinatuhusu nini km siyo kiherehere? Hiyo Cask bar inawahusu nini watanzania mpaka iwe mjadala humu? Tumekosa kabisa kazi za kufanya kiasi hiki? Mtu ameiibia serikali mnakuja huku kumtetea, watu wamekuwa wa hovyo kabisa utafikiri wanaumwa.
Naona umeumia sana.
Na bado.
 
Hii Taarifa ya kufungwa kwa The cask bar imetufumbua macho. Tafasiri ya haraka haraka ni kwamba kumbe ukijipendekeza kwa mamlaka unaweza ukafanya biashra milele bila kulipa kodi.

Je haawa matajiti wengine wakubwa wanaoshadadia CCM hali zao za ulipaji kodi zikoje?.

Leo ndo naamini maneno ya mzee mmoja huko mbeya alisema CCM kimekuwa chama cha kuficha maovu. Ukitaka mambo yako ya hOvyo yasikwame jiunge CCM.
TRA wameshatoa tamko.....hawajamfugia wao. Huyu ni mlipa kodi mzuri, hana deni. Issue ni RC na Mkurugenzi wa jiji....chawa wa .....
 
Hayo ni mawazo ya Mkurugenzi na RC Makala full kukurupuka juzi wamesimamisha ujenzi wa jengo kubwa la kibiashara!
Amos Makalla alipokuwa RC Dar alifunga bar chawa wa Magufulli alipohamishiwa Dar. akazifungua zote! Ndio tatizo l kuteua watu wasio na viwango ili mradi ni Chawa.
 
Kupitia taarifa yao waliyoweka kwenye mitandao ya kijamii, Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imedai kutohusika kwa namna yoyote katika ufungaji wa Bar ya 'The Cask'

Imewataka wahusika na umma kwenda kwenye mamlaka husika kuhusu jambo hilo.
Watapewa kesi ya uhaini
 
Ccm ina roho ya kishetani , yaani unamtia njaa mtanzania mwenzako , kisa mwarabu hata hakujui aje apige hela tz, akizipata huyo kwao.

Kwenye majanga yetu . Utasikia viongozi wa ccm ...eti kuweni WAZALENDO wa nchi
Inauma sana. Rais Samia anahangaika na kukusanya mapato kupitia service levy za bar etc halafu anatokea mtu mmoja tu kwa utashi wake anafunga biashara ya mtu. Ila Mama ana kazi sana. Hayo mambo alishayakataa kabisa kuacha kunyanyasa wapiga kura. Sasa huyo mkurugenzi mapato yake yakishuka atamlaumu nani??? Maana yake ktk revenue projection mojawapo ni revenue from services levy ya hiyo baa leo kafunga hahahaha hakika kuna watu uelewa mdogo. Hapo it was simple ilikuwa ni kuitisha media angekiri kosa tena mbele ya vyombo vya habari na kumuomba msamaha rais etc yakaisha tena wangeenda kuchangamsha biashara.
 
Cask Bado ni Top manyota Mwanza .... na imeshakua Brand nambari moja ya starehe baada ya Villa kufa kibudu...
Sema villa park imekufa vibaya sana daah
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuujulisha Umma kuwa, haijahusika kwa namna yoyote na ufungaji wa Bar ya THE CASK iliyopo Jijini Mwanza.

Tunaomba wahusika na Umma wawasiliane na Mamlaka husika juu ya jambo hilo.



-
Pia soma
Mkurugenzi aliisimamisha biashara ya watu bila kuwasiliana na TRA? TRA ndiye mkusanya Kodi, Mkurugenzi alifahamuje kuwa Kodi haikuwa ikilipwa ikiwa hakuwashirikisha TRA?

Kati ya TRA na Mkurugenzi wa Manispaa, nani aliye na mamlaka ya kufungia biashara zinazodaiwa kodi?
 
TRA wametoa tamko mda mfupi uliopita kwamba hawausiki na ufungaji wa bar ya the cask na hii itakua ni baada ya wamiliki wa bar kwenda TRA

Hii pia inaonyesha rangi halisi ya waafrika walio wengi kukomoana, na pia upeo mdogo sana wa mkurugenzi alisahau kwamba wenye baa lazima wataenda TRA kwa maelezo zaidi, na madhara ya kuwaajiri makada kwenye kazi muhimu kama hizi za ukurugenzi
View attachment 2719782
TRA ieleze pia kama ni kweli kodi haikulipwa kwa miaka miwili.
 
Back
Top Bottom