TRA imekusanya Trilioni 11.11 kuanzia Julai hadi Desemba 2021 na trilioni 2.51 Desemba 2021 pekee

TRA imekusanya Trilioni 11.11 kuanzia Julai hadi Desemba 2021 na trilioni 2.51 Desemba 2021 pekee

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya TZS trilioni 2.51 Desemba 2021, kikiwa ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kufikiwa tangu kuanzishwa mamlaka hiyo mwaka 1996.

Aidha, Julai - Desemba 2021, TRA imekusanya TZS trilioni 11.11, sawa 98% ya lengo la TZS trilioni 11.302.
IMG-20220101-WA0020.jpg
IMG-20220101-WA0021.jpg
 
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa TRA, mamlaka hiyo imevunja Rekodi ya kukusanya Kodi kiasi cha Shilingi Trilioni 2.51 kwa Mwezi Desemba 2021 ikiwa ni kiwango cha juu kabisa kukusanywa katika Mwezi tangia kuanzishwa kwake. Katika kipindi cha Desemba 2020, TRA ilikusanya pungufu ya kiasi hicho kwa asilimia 20. Aidha Makusanyo kwa miezi 6 iliyopita ni Shililingi Trilioni 11.11 ikilinganishwa na Trilioni 9.24 zilizokusanywa kwa kipindi kama hicho mwaka 2020.

Pongezi kwa Mhe. Samia, pongezi kwa Kamishna Kidata kwa kutokusanya kodi ya dhulma lakini matokeo yanaonekana. Watanzania lipeni Kodi kwa hiari mjenge nchi yenu.

Kazi Iendelee.

cc: Suzy Elias
 
Itoe tilioni 2 iwape ruzuku viwanda vya matrekta wazalishe matreka mengi waje watuuzie wakulima kwa robo bei tuzalishe Sana tuuze tupate mapato kupitia export tuwe na mapesa tele ya kufanya maendeleo bila kukopa.
 
Ni Nazi njema sana hii,

Nashauri tumwacheni JPM apumzike sasa!

Maana alichofundisha kinazidi kueleweka, na tumeamini pia kwamba kumbe mengi sana tumekuwa tukimzushia tuu,

Tulikuwa tukimshambulia sana kila akitangaza mapato kwa mwezi ni Tr.1.8 had I tr.2+

Na Leo hayupo, tuseme uwongo bado unaendelea?
 
Bado ni ndogo sana.
Kodi ikikusanywa kiufasaha bila janja janja na rushwa, kwa mwezi trillion 5 zinakusanyika.
Kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi na janja janja.
Unakuta mtu ana turnover ya 200m annually ila TRA mashine inasoma 45m au 30m. Na hii ni biashara moja sasa piga mahesabu maelfu ya biashara yanayofanya ujanja.
 
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa TRA, mamlaka hiyo imevunja Rekodi ya kukusanya Kodi kiasi cha Shilingi Trilioni 2.51 kwa Mwezi Desemba 2021 ikiwa ni kiwango cha juu kabisa kukusanywa katika Mwezi tangia kuanzishwa kwake. Katika kipindi cha Desemba 2020, TRA ilikusanya pungufu ya kiasi hicho kwa asilimia 20. Aidha Makusanyo kwa miezi 6 iliyopita ni Shililingi Trilioni 11.11 ikilinganishwa na Trilioni 9.24 zilizokusanywa kwa kipindi kama hicho mwaka 2020.

Pongezi kwa Mhe. Samia, pongezi kwa Kamishna Kidata kwa kutokusanya kodi ya dhulma lakini matokeo yanaonekana. Watanzania lipeni Kodi kwa hiari mjenge nchi yenu.

Kazi Iendelee.

cc: Suzy Elias
😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆

Unafikiri kwa nini leo wameamua kutoa huo waraka?!

Jiongeze.
 
Ukweli ni kwamba mwamko wa watu kulipa kodi umepungua, kwa sasa mambo ya EFD wafanyabiashara hawaogopi tena tofauti na miezi michache imepita. Hayo makusanyo ya kuvunja rekodi yanatoka wapi?

Ni sawa na kusema rushwa imepungua wakati imeongezeka mara dufu. Polisi (hasa wale wa barabarani) siku hizi wanaomba rushwa waziwazi bila kificho, na kwangu mimi hawa jamaa ndiyo kipimo cha rushwa inchini.
 
Back
Top Bottom