TRA imekusanya Trilioni 11.11 kuanzia Julai hadi Desemba 2021 na trilioni 2.51 Desemba 2021 pekee

TRA imekusanya Trilioni 11.11 kuanzia Julai hadi Desemba 2021 na trilioni 2.51 Desemba 2021 pekee

TRA inasema lake, waziri mkuu amasema lake, Rais anasema lake, sasa 1.3 Trilion mlikopa za nini iwapo mlikusanya 11 Trilioni?

Hizi hesabu zao wanazipika!!! Si unaona zile hesabu walizomuandikia Mama Samia kwenye hotuba yake!! Wasimuamini huyo Mkuu wa TRA ana kila sababu ya kudanganya kwani ameokotwa jalalani hivyo anaogopa kurudi huko!!
Waziri mkuu kila siku anasema uongo, haaminiki!!
 
Ukweli ni kwamba mwamko wa watu kulipa kodi umepungua, kwa sasa mambo ya EFD wafanyabiashara hawaogopi tena tofauti na miezi michache imepita. Hayo makusanyo ya kuvunja rekodi yanatoka wapi?

Ni sawa na kusema rushwa imepungua wakati imeongezeka mara dufu. Polisi (hasa wale wa barabarani) siku hizi wanaomba rushwa waziwazi bila kificho, na kwangu mimi hawa jamaa ndiyo kipimo cha rushwa inchini.
Ndio maana nasema serikali irudishe kikosi Kazi maana tungeweza kukusanya zaidi ya hapo.
 
Umeniwahi au wanapika data Hangaya asionekana kashindwa kukusanya Kodi.
Hizi ramli haziwezi kukusaidia,hata akili ndogo za kutumia huna yaani unaona kila siku investors wanamiminika then unategemea Kodi isipatikane?

Tafuteni mengine ya kuongea kama propaganda za ukabila na uzanzibari .
 
Ukweli ni kwamba mwamko wa watu kulipa kodi umepungua, kwa sasa mambo ya EFD wafanyabiashara hawaogopi tena tofauti na miezi michache imepita. Hayo makusanyo ya kuvunja rekodi yanatoka wapi?

Ni sawa na kusema rushwa imepungua wakati imeongezeka mara dufu. Polisi (hasa wale wa barabarani) siku hizi wanaomba rushwa waziwazi bila kificho, na kwangu mimi hawa jamaa ndiyo kipimo cha rushwa inchini.
Kudhibiti polisi ni ngumu kwa sababu wanashirikiana na wenye vyombo vya moto kula rushwa.

Hiyo ni sawa na rushwa mahakamani
 
Watanzania wengi hatulipi kodi, huu ndio ukweli...hizi EFD machine zilipaswa kuwepo kila mahala.....kwa mama ntilie, viduka vya uswahilini huku, kwenye mabus ya abiria, magari ya mizigo...ifike mahala uwe utamaduni tu na jamii izoee..
 
Wazo zuri tatizo hatuna kiongozi wa kuyafanyia mawazo chanya kama haya...
True Kilimo hakiwapi kiki wanasiasa.
Matrekta udumu mda mrefu kuliko ndege, uajiri watu wengi kuliko ndege,urudisha pesa haraka kuliko pesa.
Kupanga ni kuchagua
 
Watanzania wengi hatulipi kodi, huu ndio ukweli...hizi EFD machine zilipaswa kuwepo kila mahala.....kwa mama ntilie, viduka vya uswahilini huku, kwenye mabus ya abiria, magari ya mizigo...ifike mahala uwe utamaduni tu na jamii izoee..
Sijui hapa govt imeishiwa mbinu au vipi..Watu wanalaumu Kukopa huku Kodi hawalipi..

Serikali imeshindwa kuunda kikosi Kazi kweli Ili kuwabana watu wote wanaonunua bidhaa bila risiti? Polisi wapo,TRA wapo na watendaji wapo sasa sijui tatizo ni nini..

Hii nchi watu hawalipi Kodi, yaani kuna maduka ya madawa nayafahamu ya jumla wanauza balaa lakini waliacha kutoa risiti kitambo ukiomba hadi wanakushangaa mara mbili mbili..

Au TRA wekeni mawasiliano rahisi Ili tuwafahamishe.
 
Hongera ila kiwango bado kidogo kwa nchi kubwa kama hii..endelee kukusanya kodi kwa ufasaha na weredi...pia tozo zetu za miamala ya simu ipo kwenye haya makusanyo au yenyewe inajitegemea?..na nani atakuja kutupa taarifa yake?

#MaendeleoHayanaChama
 
Yanajitegemea.
 
Back
Top Bottom