TRA, inakuwaje ushuru wa kuingiza gari ni mkubwa kuliko bei ya gari lenyewe?

~ Roho za kwa nini haziwezi kutuacha salama...wanaona watu wa kawaida wakimilika magari watafaidi sana na kula nao sahani moja,hapo Botswana ushuru wao upo chini...wanatumia bandari SA...unaambiwa hata mama ntilie anamiliki chuma yake inampeleka kijiweni na kumrudisha nyumbani,bot ni afrika sio ulaya.
 
Sio na karoho ka korosho kama kawaida ya mbongo?
 
Siyo swala la mtu katoka wapi, hiyo ni sera ya serikali hata ukienda wewe hapo TRA utatumia formula hiyo hiyo
 
Hoja dhaifu kabisa Tanzania nchi changa bado tunahitaji nondo kwa ujenzi wa miundombinu so hayo magari yakichoka kabisa tunayeyusha kupata nondo
Kuna viwanda vingapi vya kuyeyusha magari skrepa kuwa nondo ?
 
Hii ishu nakumbuka last week nlikua namwagizia mshkaji vits ya mwaka 2003. Yaan gar inatoka kule mpaka inaingia bongo ni dola 1700. Ila huku ushuru wake ni milion 4 na upuuz mpka unajiuliza kisa nin kutufanyia hvi.
 

Umeongea nini sasa? Amekuambia hadhani kua ni realistic kulipa kodi ya kiasi hicho kwa gari la aina na mwaka huo, issue ni je hizi gharama za kuingiza gari kuwa kubwa karibia au zaidi ya thamani ya kuliagiza zinaleta maana? Taking aside issue za dumping fee!
 
Hakuna kiwanda cha magari bongo lkn tozo ya magari imeegemea misingi ya protectionism
Kabisa!
Sijui kwa nini tuna copy na ku paste kila kitu bila kufikiri.

Kama tungekuwa na viwanda halafu tunaweka restrictions za magari kuingia kwa kuweka kodi kubwa hapo Sawa. Lakini kwetu ni tofauti kabisa.

Pia si katika magari tu, bidhaa nyingi zinazalishwa nje na kuuza kwetu bei ndogo wakati vilivyozalishwa ndani bei kubwa kwa sababu ya msululu wa Ushuhuru na kodi.

Sisi ni pumba hasa yaani....!
 
Kuna viwanda vingapi vya kuyeyusha magari skrepa kuwa nondo ?
Hata kama hakipo je hatutakuja kuwa nacho kabisa? Je wanaonunua na kuexport scraper huoni kuwa watakuwa na wigo mpana wa kupata mzigo? Yaani huoni hizo fursa za multiplier effects za kiuchumi? Tatizo bongo tunaongozwa na watu wenye akili ndogo?
 
Mabeberu weusi ni wabaya maramia afadhali ya beberu mweupe
 
Nenda kaangalie Subaru Legacy BM9 ya 2009/2010/2011/2012 uone gari ni $3500-5000 ushuru wake ni 22,000,000-25,000,000 mzee
Huyo haelewi kuwa pamoja na kodi ya umri la gari 30% bado ni affordable kuliko gari lenye umri chini ya miaka 8 ambalo halitozwi kabisa kodi ya umri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…