TRA inazalisha mabilionea wengi kupitia wafanyakazi wake

TRA inazalisha mabilionea wengi kupitia wafanyakazi wake

Sina chuki na wafanyakazi wa TRA bali naongelea uhalisia
TRA ndo inayoongoza kuzalisha mabillionnaire wengi vijana wadogo wanamiaka michache kazini wanamiliki utajiri wa kutishi magari ya kifahari na mahekalu

Kwa sasa-hivi mabillionaire TRA ni jambo la kawaida na miaka ijayo kwa trend hii TRA kupitia wafanyakazi wake watatoa trillionaire

Kama unataka kuwa billionnaire na baadae trillionnaire pambana uingie TRA kama mfanyakazi kule hutumii nguvu kabisa
Serikali inatafuta sumu Kali kukomesha upigaji TRA Yani ikikamilika TRA na Halmashauri Ngoma droo
 
Watoza ushuru wasio waaminifu, wanasheria wanaopindisha sheria na wafanya Biashara wanaopunja kwenye mizani; Hao ni kati ya makundi yaliyo tajwa wazi wazi kwenye vitabu vitakatifu kuwa, watakuwa na wakati mgumu sana siku ya mwisho (day of judgement!)
Najua watu wanawaona kuwa wamepatia Maisha, lakini kwa Mungu hao ndio wameokota yai.
Wewe fanya kazi kwa bidii na kwa haki katika nafasi yako huku ukimtegemea Mungu, atakufungulia milango mingine ya halali ya kukuongezea kipato!
 
Back
Top Bottom