DOKEZO TRA, kodi za kuingiza Magari ni kichefuchefu kwa Wananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu hii hoja kila ninapokutana nayo kwanza lazima nimsikitikie anayeileta kwa kuwa na ufahamu finyu sana na sababu kubwa ya huo ufinyu ni kwamba Tanzania siyo mijini kwenye lami tuu jamani!!! Watanzania hawa tunaosema wako milioni 60 (hatujui sensa itasemaje maybe milioni 70) nearly 90 % wako huko vijijini na wao pia wanahitaji magari, hata kama barabara zao ni za vumbi au changarawe. Achaneni kabisa na hii mentality ya barabara za lami huko mijini kwenye watanzania asilimia 10 jamani, acheni kabisa!!! Sasa hivi nyie watu wa mijini (asilimia 10) na mnaojidai mnamiliki magari kwa sababu huko mijini kuna lami mmeanza kulalamika kweli kweli kwa mazao kupanda bei (mchele 2500, unga 1500,maharage 3000 etc) na kwamba eti mipaka ifungwe ili mkulima asiuze mazao yake kwa bei nzuri. Haya ni maajabu kwa sababu kama una gari unashindwaje kumudu kununua chakula?? Nirudi kwenye hoja ya msingi, acheni watu wa vijijini, ambao ni wakulima, wanunue magari yao kama pick up, Fuso, trekta, guta nk kwa bei nafuu ili waweze kuzalisha mazao mengi na kuwaletea huko mjini kwa bei poa. Hayo magari ya wakulima hayahitaji lami wala nini, na kama mimi ningekuwa kwenye maamuzi basi ningepitisha sheria kwamba magari na mashine kama trekta, pick up, Fuso na nyinginezo ambazo zinachangia uzalishaji shambani vingelipiwa kodi less than 15% ya gharama ya hiyo mashine ili kila mkulima amiliki trekta, powertiler, lori/Fuso, guta, water pump, harrow, planter, spray mashine etc...
 
Sasa tukubaliane, kila siku asubuhi, kabla ya kuchangie uzi wowote tunaanza kuchangia huu kwanza, kama sala ya asubuhi vile, then ndio tunachangia zingine. Haiwezekana kufanywa mataahira wakati tuna akili timamu
 
Tupaze sauti tunaumizwa na tuko kimya hawa tukiwachekea watatuua kabisa
Ni kweli, ona unyama na ukatili wa tozo tunaofanyiwa kwenye miamala ya simu na benki, bado huku tena, hapana aisee, tukiendelea kujikaza watatuuawa hawa, this unbearable, kwenye mafuta ndio unyama kabisa tunafanyiwa
 
Unaona sasa??? This is a very serious problem with our taxing system... Hata siku moja mkulima nchi hii hawezi kumiliki hii mitambo ili aongeze productivity, tutaendelea kusubiri Ukraine, ambao wako vitani for nearly 8 months, watuletee ngano!!! We have a very serious problem, ndiyo maana nikasema kule juuu it's time kupata external tax consultant... Really
 
Watanzania wanaenda kununua magari waliyotumia wazambia na Malawi kwa sababu yaliingia kwa kodi ndogo hata wakiuza yatauzwa kwa bei nafuu na yeye anaagiza lingine anakuachia chakavu ambalo Tanzania litaonekana ni jipya ndio maana tupo busy na Fusso sijui Tandamu ni kwa sababu ya kodi gari tani 4 ila linabeba mzigo mpaka tani 15 harafu tunasema yana matatizo ya breki...wenzetu wapo na International na aina zingine za Truck na kwa ukubwa wake zinatunza vizuri bara bara sisi tumejikita na pick up na kuziita truck kisa kodi kubwa..imefikia Watanzania eti ukimwambia chukua Scania anasita anataka Fusso wakati ni vitu viwili tofauti kabisa..
 
Kwa
Kwa mtizamo huu upo sahihi kiongozi yaani gari za kikazi ziwe na tax ndogo Mana zitakuwa zinafanya kazi na kurahisisha maisha Ila sio private.

Sema huko juu umeongea kwa hisia/beliefs zako so mtu akiwa na beliefs fulani Ni kazi mno kuiondoa na ku adapt nyingine.
Yaani we're hard katika behavior modifications. Mana hujui ukiongeacho hizi Ni fani za watu. Huwa Kuna research inafanyika na sio kuwa watu wanakurupuka. Unajua kuwa Kuna watu huwa wanakesha kihesabu idadi za magari zinazopita sehemu fulani kwa siku Saba za wiki mpaka mwezi mzima ama unaongea tu. Yaani Kuna kitu kinafanyika ili data fulani zipatikane ili ujenzi fulani ufanyike.


Yaani iko ivi bomba la maji haliendi tu sehemu Bali watalaamu wanajua Kuna watu wangapi so wanajua uwezo wa watu kutumia maji Ni muda gani matumizi yanakuwa makubwa ili wapeleke maji hayo yanayowatosheleza mahitaji.
Mtandao wa simu wanajua kuwa uwezo wa wateja wao kutumia signals zao unatosha sometime kunakuwa na traffic kubwa baadaye inakuwa jam or high density.


So hizi za road ziaje ishu Ni umasikini wa pesa,akili na mawazo watu wanawaza watamiliki lini v8 Ila hawakuwazii wewe Tena ujue.


Yaani kila roads zinajulikana uwezo wake ,uzito wake wa mzigo kubeba,uwongi wa gari,hata hizo roads za Kijijini mkizitembelea mno Kuna zile maintenance cost,unaona mvua ikinyesha corrugations,hizo pipe culverts ama box culverts unajua uwezo wake wa kupitisha Ni Tani ngapi.


Sasa Ni hivi vitu vyote vinakuja kwa kupiga hesabu sio Kama hizi tozo jemba anaamka anasema kuwa tukate na hela Benki ninunue hili la 560M nitembelee Mana saivi mie Nina value mno kuliko wa huko kijijini wakati jamaa majuzi tu hapa alikuwa mchunga ng'ombe Basi tu. Tuendeleze tozonia yetu.
 
Zama huko sajili kampuni Kama muwekezaji agiza semi zako kibao unawabebea watanzania mizigo yao. Inapigwa chapa ya transit
 
Zama huko sajili kampuni Kama muwekezaji agiza semi zako kibao unawabebea watanzania mizigo yao. Inapigwa chapa ya transit

Mbona watu wanapambana maana mazingira ya biashara Tanzania kwa maneno ya wanasiasa ni mazuri lakini kwa uhalisia mazingira mabovu sana
 
Tatixo kubwa ni CCM chama kinachotutawala . Mwarobaini wa hata yote ni katiba mpya tuu. Wana mawazo mgando na nchi haiendelei. Muarobaini wa haya yote ni katiba mpya
 
Tatixo kubwa ni CCM chama kinachotutawala . Mwarobaini wa hata yote ni katiba mpya tuu. Wana mawazo mgando na nchi haiendelei. Muarobaini wa haya yote ni katiba mpya

Kabisa kabisa
 

Hadi hapa ni wengi wanaghairi na ina maana pia wanapoteza mapato mengi kuliko kawaida
 

Hawakuzi uchumi wa mwananchi wanadidimiza uchumi haiwezekani guta, trekta, mashine za kupiga mpunga na mahindi navyo vina kodi halafu watasimamisha mashingo yao tunakuza kilimo how? Miaka yote mwanachi akuze kilimo kwa jembe la mkono
 
vile mwigulu na baadhi ya maofisa wa TRA wanamcheka mleta mada.
 
Lucas mwashambwa njoo hapa. Usipite kimya kimya kama unaaga marehemu....na hili peleka.
Sio kila uchao nyie ni mapambio tu.
Amkeni!
 
Bandari yetu imekuwa ya kuwafaidisha warundi, wanyarwanda, wazambia, wacongo na wamalawi sisi ni kutuumiza tu. Ukieleza kuwa kodi inatakiwa iwe chini kama majirani zetu, Mwigulu anajibu kikebehi kabisa kuwa tuhamie nchi hizo jirani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…