DOKEZO TRA, kodi za kuingiza Magari ni kichefuchefu kwa Wananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Umeanza vizuri umemaliza vibaya,
Nikukumbushe tu tozo alianza kutuwekea magufuli sh 100 kwa kila lita 1 ya mafuta ya taa, disel na petrol na na baadae ikawa 200, unanunua mafuta ya taa kwa ajili ya kujimulikia na familia yako lkn unamlipia na kodi mwenye gari, hii ndio ilitakiwa kukemea vikali sana lkn kwa kua kuna watu waliamini magu hua hakosei na hana baya ikitokea kakosea au kafanya baya unarudi kwenye kanuni ileile kua magu hua hakosei ndio maana hamkupiga kelele kuhusu hii tozo, wenye magari halipii tena kodi gari yake ila wamemuwekea kwenye mafuta ila tunasahau mafuta sio kwa ajili ya magari tu....

Kwa kua hamkuona baya kwa magu nami naungana na mama kua anaendelea alipoishia magu na kudumisha alivyovianzisha na kuviboresha ikiwa na pamoja na tozo. Ila tuwe wapole tu

Kuhusu kodi za magari wengi humu hawana uelewa, mtu unaagiza gari ya mwaka 2013 now tupo 2022 na ilishatumika ina km laki na ushee huko yaani tunaleta skrepa huku kwetu afu watuwekee kodi ndogo? Hata watoto wetu wa o level wangeenda shule kila mmoja na gari yake, ile kodi ya uchakavu ndio hua ni kubwa nenda kaagize gari mpya kabisaaa uone kodi zake zipoje ndio urudi hapa kuja kuilaumu serikali.

Hivi mshajiuliza gari umeitumia miaka 10 na ushee afu unamuuzia mtu hiyo itakua gari au skrepa?
 
Gari chakavu lazima watu watakufa kila siku na wataleta visababu kibao kumbe kodi inachangia hadi basi la abiria mtu anabembeleza used za miaka kibao kumbe kodi himilivu watu wataleta vyuma vipya, magari imara huokoa pia uhai wa watu
Wazambia walikua wanapiga picha wakiliona Scandinavia pale Lusaka leo hii wao wana bus zingine zinaenda vijijini huko na wametuacha mbali mno maana wapo kwenye series ya body za Iriza Q 10 wakati hizo Tanzania ni anasa kwa kodi yake wanaona wachonge chonge bus kwa kutumia nondo na flat bar...baadae wanashangaa ajali ndogo ila ina madhara makubwa kwa abiria wao hawajui hilo ukiona watu wameshindwa kuwapa wenye shule wapate punguzo ili watoto wapande bus nzuri za kwenda shule au michezo wao wanakomaa na kodi tuu kama vile Nchi ipo jangwani..
 
Mind set yeti bado ni ya kimaskini maskini..........mbali na ukubwa huo wa kodi urasimu/uzembe/ kutokujali ktk taasisi za umma ni janga kubwa. Amini nawaambia kuna walio tayari kulipa hiyo kodi kubwa nao wamepanginshwa foleni ndeeefu kwa sababu za kipuuzi kabisa!. ......utasikia kutoa kibali cha kufanya biashara hii ama Ile itabidi kusubiri mbio za mwenge zipite wilayani hii!, ....au inabidi kusubiri zoezi la sensa lipite,...subiri ziara ya mkuu wa mkoa iiishe,......
 
Kazi ya serikali ni pamoja na kusimamia rasilimali za nchi, kukusanya kodi na kuhakikisha kodi ile inatumika kuwahudumia wananchi ikiwamo kujenga barabara, hospitali, shule na vyuo vya ufundi, kulinda raia na mali zao, kurahisisha maisha ya raia kwa kuweka sera rafiki na himilivu kwa raia wake, sasa wale waliopewa dhamana ya uongozi wanapogeuka waongo, wezi wa kutupwa shida huanzia hapo maana hata sheria watatunga za kuwalinda wao wenyewe na kumkandamiza raia asiye na hatia
 
Wakiacha ten percent kwenye miradi uwezekano wa kujenga miundo mbinu na miundo msingi ya kisasa upo
 
Penye miti hakuna wajenzi, Tanzania ina kila kitu lakini ilikosa viongozi toka uhuru, viongozi ambao waligawa rasilimali zetu kwa matapeli waliokuja kwa jina la wawekezaji tena wakatunga na sheria za kuwalinda hao matapeli
 
Suluhu mojawapo ni kuwa na bunge 50% hao wanaosema watatawala milele na 50% upinzani.

Ila sasa sisi wenyewe wananchi ndio shida namba moja. Wacha tuendelee kulialia tu.

Kwa akili za mtu kama magufuli anaedhani mpinzani anarudisha nyuma maendeleo ndio akili za viongozi wengi huko chichiemu, hawajiangalii wao ndio wenye dhamana ya kila kitu wanaangalia wapi wawakabe Chadema ili hao chadema wasifanye siasa wakati muda wa kuwabana wanasiasa wa upinzani wanageutumia kubuni mambo mbali mbali maendeleo yangekua suala dogo sana
 

Kodi ya Tanzania kwenye magari na bidhaa nyingine itakushangaza hata wewe hadi gari mpya kodi yake haishikiki
 

Rafiki yangu mmoja wa ujermani aliwahi kunieleza always your leaders are at the picnic, maana alikua kila akienda kutafuta huduma anaambiwa mara subiri muda wa chai, mara katoka kidogo, mara kaenda kukojoa, mara anakikao yaani wanapoteza muda bila sababu na muda ni mali na kwa kutokujali kwao muda wanazidisha umaskini kila leo hakuna mtu ambae hakujali muda aliwahi kufanikiwa hayupo,
 
Inasikitisha SANA. Watanzania tunaishi kama mashetani yani...Ukiwa Tunduma unashuhudia lundo la gari nzuri nzuri za aina tofauti tofauti na hizi yebo yebo zetu tulizozizoea kuziona hapa bongo zikivuka boda kwenda nchi jirani.
Pana dogo mmoja Mzambia akitaka gari nzuri ananiuliza alianza na Cayyene,akaja Paramela,Evoque,Mercedes yatch back sasa hivi yupo na autobiograph range rover ya 2020 ana duka la hardware hapo Lusaka akitumia akilichoka miezi kadhaa analiweka sokoni anaongeza hela au ikiwa sawa ananunua gari zuri zaidi alishangaa nilipopita Lusaka na gari ya 2014 mwaka 2020 namwambia ndio yangu ya kutumia tena nilimwambia nimejitahidi sana maana kodi zetu sio rafiki akawa anasikitika tuu..
 
Unataka kulipa kodi tra mnaambiwa wapo kwenye kikao au mtandao mbovu unabaki kusubiri pana jamaa ni mtumishi wa Serikali hapa Tanzania nilimpeleka wizara wanayotoa vibali vya magari hapo Sunnside Pretoria tulipokewa na watu wawili na wanakimbizana balaa na customer care yao ipo juu balaa baadae namwambia hapa ni bure hatulipi kitu alishangaa sana..
 
==
Ni changamoto kubwa sana
 

Yaani ustaarabu wa wenye dhamana ni mdogo kupita kiasi hadi unashangaa hawa shuleni walisomea ujinga au uvivu
 
Poverty Minded leaders kama wewe hamkosekani.

Unaongelea pikipiki kwa nchi ndogo kama mkoa wa tanga?

Kuna nchi kubwa sana, usafiri wa gari ni muhimu hata hizo pikipiki ni anasa tu.

Unaweza tumia pikipiki toka dar kwenda morogoro achilia mbali kufika iringa, mbeya, mwanza n.k?

Usiwe mjinga kama viongozi wako, watu wakiwa na magari mengi, multiplier effects ni kubwa kuliko kuwa na magari machache.

Wape nafasi wananchi wawe na uhuru wa kufanya watakayo mradi hawavunji sheria.
 
Tuna janga
Hatuna viongozi
 
Kama una uwezo basi usilalamike. Ila hatuwez kuruhusu Kila mtu kumiliki magari Kumi lazima yawe machache wengine watumie usafiri wa umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…