TRA yaendelea kumkaba koo Toufiq Salum Turky kodi ya gari milioni 308.5

TRA yaendelea kumkaba koo Toufiq Salum Turky kodi ya gari milioni 308.5

Sina maana asamehewe hebu soma nilichoandika
Ifike mahali tutafute pia vyanzo vingi vya kutuingizia mapato ila kama tutaendeleza Tozo tu ni ukilema huo
Amini hamtaweza hata kutengeneza toothpicks kwa miaka 100 ijayo

Tozo ya miamala mnajengea zahanati
Kwanini msiwe na vyanzo vya kuingiza hela kuliko kuonea watu kwa kulipa kodi Mara 3 mshahara uliopo bank?
Be serious
Muhimu kwako kujua ni kuwa Tanzania hatujapoteza bandari zetu tulizonazo, we’re not a landlocked country, lazima hayo mapato kupitia bandari zetu yatunufaishe zaidi ya Rwanda, Uganda, Malawi na landlocked nations nyinginezo.

By the way, vyanzo vya mapato vimekuwa vikibuniwa vipya kila wakati pengine tu sniper umajifunga upofu… vikibuniwa mnalia lia, vikiondolewa mnalialia, mwanadamu ni useless kabisa….mfano mwepesi ni hizi tozo.
 
Gharama ya usajili wa magari TRA ni kwa ujazo wa injini ya gari (maarufu kama cc). Mfano gari za chini ya cc 1500 unakuta usajili wake ni Tshs. 500,000/=, na zaidi ya cc 1500 inaongezeka kidogo. Yaani hii ni bila kujali aina ya gari, zingatio ni ujazo wa injini. Napendekeza, muundo huohuo wa ujazo wa injini ndio ungetumika kwenye kupata gharama ya ushuru wa gari. Gharama zingekuwa sio kali na wanananchi wangemiliki magari mapya (ya miaka ya karibuni) na hivyo kupunguza uharibifu wa mazingira. Au serikali haipendi wananchi wake wamiliki magari ya kisasa?? DRC vinaenda vyuma vya hatari na vinapitishwa hapahapa nchini kwetu

Mkiona ujazo wa injini sio poa kutumika kama base basi wekeni hata muundo wa gari (salon, SUV, hatchbak na kadhalika,achaneni na habari za CIF, mnaumiza sana wananchi
 
Kuna watu wana wivu zaidi ya shetani!
Shetani ni kiumbe cha Mungu kwa mujibu wa maandiko, Mungu kaiumba Dunia na ulimwengu from utupu… bottom line, tabia zote za shetani zinaakisi uumbaji wa Mungu… sio mimi nasema ni maandiko.
 
Baba yake huyu Kijana ndio aligharimia safari ya Tundu Lissu kutoka Dodoma hadi Nairobi na kuchangia jumla ya Dola laki moja wakati huo (2017)

Mungu amrehemu Mbunge huyo wa Zamani Hayati Turky
Sasa ni wakati wa Wakili Msomi Lisu kuingilia kati huo mgogoro kupitia Mahakamani amtetee Dogo ili apunguziwe Kodi,alipe fadhila za Mzee!!
 
inasikitisha sana ukienda hapo congo,zambia,malawi, watu wanamiliki gari za maana,tena european cars na kama ni japan ni gari ambazo hazina miaka mingi toka kutengenezwa kwake ila bongo watu wanalazimika kuangukia kwenye gari ambazo walau zina cc ndogo na ushuru mdogo mfano mzuri ni gari ya taifa ist iliyoireplace gari nyingine iliyokuwa ya taifa toyota vits. tatizo kubwa ni ushuru, kwenye ile calculator ya tra jinsi gari inavyokuwa latest ushuru ndio unakuwa mkubwa maradufu,mtu anaamua aangukie kwenye gari kuukuu,kwa hiyo bado haizuii watu kuagiza gari kuukuu sababu ya ushuru. ambapo gari zilizotengenezwa chini ya 10 yrs ushuru wake ni mkubwa. Pili watu wanashindwa kumiliki europen car maana pia ushuru wake ni mkubwa, gari ya europe yenye cc sawa na year of manufacturing sawa na ya japan ushuru wake uko juu. hivyo watu wanashindwa kununua european car wanaaguilkia kwa mjapan zaidi.

Ushauri kwserikali ibadili hiyo fomula ya ukokotoaji wa ushuru, ushuru ushuke,watu waweze kununua magari yasiyo chakavu, na hata yenye uwenzo mkubwa . faida yake watakaonunua magari ni wengi, serikali itafidia kodi iliyoipoteza kwenye mafuta, na vipuli. ni bora hata wakapunguza hiyo kodi ikawa nusu ya bei ya manunuzi,wakaanzisha road toll.
 
Shetani ni kiumbe cha Mungu kwa mujibu wa maandiko, Mungu kaiumba Dunia na ulimwengu from utupu… bottom line, tabia zote za shetani zinaakisi uumbaji wa Mungu… sio mimi nasema ni maandiko.
Ndiyo kisa Mungu alimtupa duniani ili aungane na watu ambao hawatauona ufalme wa mbinguni!
 
Hii kodi ni sawa kabisa. Gari la kifahari hili. Kama hana hizo fedha basi hata kumiliki hilo gari hapaswi. Makapuku wenzangu kama wewe badala ya kuunga mkono serikali inapotoza kodi kwa mambo ya kifahari ndiyo mnajifanya kupiga kelele. Huoni ni busara wanaotaka ufahari kulipa kodi ili makapuku kama wewe tozo ziondolewe?
Achaa ujinga wako, hata IST ni Gari ya kifahari kwa mtu anaemiliki bodaboda au Baiskeli! Na Matajiri wa IST nao pia wako humu na wanalia pia wao wanatozwa Kodi kubwa sana kwa ki IST chake alicho aagiza kutoka Japani!!
 
Maskini ndiyo mnapiga kelele kumtetea tajiri aliyeamua kununua gari la la kifahari la karibu sh milioni mia saba asilipe kodi! Huu ni unyumbu wa hali ya juu. Mimi nadhani mngeunga mkono serikali itoze kodi kubwa zaidi matajiri wanaotaka kufanya mambo ya kifahari na maskini kama wewe mpunguziwe kodi! Duniani kote magari ya kifahari au vitu vya kifahari kodi yake huwa kubwa.
Hata wenye mkokoteni wenye akili Kama zako nao wanaombea Matajiri wanao milki Vitz nao wawe wanapigwa Kodi kubwa hadi washindwe kumiliki hizo vitz ili warudi kumiliki mkokoteni!!
 
Ndiyo kisa Mungu alimtupa duniani ili aungane na watu ambao hawatauona ufalme wa mbinguni!
Mungu anakimbia matatizo tena! Tena aliyoyaasisi yeye mwenyewe? Mungu gani weak hivyo, roho mbaya ndio msingi wa maendeleo ya dunia ya kale mpaka kesho… achana na siaza za dini kumrushia lawama shetani ingali una deal na mwanadamu… shetani/ Mungu ni theoretical work kwa wavivu kufikiria na waoga na kusonga mbele no matter the obstacles.
 
Back
Top Bottom