TRA yaendelea kumkaba koo Toufiq Salum Turky kodi ya gari milioni 308.5

TRA yaendelea kumkaba koo Toufiq Salum Turky kodi ya gari milioni 308.5

Ushuru kandamizi hata kama wamepitisha, haku uwiano wa million mitano na miatatu.. Wataalamu wetu wa kodi warekebishe baadhi ya mambo.. Sie hatuzalishi magari lazima tununue nje.. Wamenichosha nilitaka na mie kuagiza la hivyo acha nitulie na ist yangu 🤠🤠🤠.. TRA wana mchezo wa kubadiri ushuru mala kwa mala
Ile system wanachopeka wanavyojiskia
 
Nikuulize wewe kati ya Serikali ya Tanzania inayoagiza magari 600 kwa ajili ya wabunge tu achilia mbali MaRC, DC majeshi na idara zote VS huyo jamaa yako wa G-Wagon moja tena yakuomba msamaha wa kodi nani tajiri hapo, nani anamuonea wivu mwenzie? Be realistic basi.
Viongozi wa serikali wanamuonea wivu, wanataka wao tu ndiyo watumie magari ya kifahari kwa kutumia Kodi zetu!

Kwa taarifa yako wabunge hawanunuliwi magari na serikali bali wanapewa mikopo kwa wale wanaohitaji!
 
Mkp mtu unanunua gar milinion Mia tano Kweli Kodi ikushibde mm nadhani magar y kifahari kwa nnchi zetu hz za kiafrica hazipazwi na mtu akiliingiza itozwwe Kodi sawasawa haswa hongera Zanzibar piga Kodi had akili iwakae saawa hao wanaonunua magar ya kifahar Mara nyingi ni wahujumu uchumi tu mm ningekuwa commissioner ningepiga mili400 kbsa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Tatizo lako umejaa uchawi na roho mbaya
 
View attachment 2353083
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema mfanyabishara maarufu wa Zanzibar, Toufiq Salum Turky, bado hajalipa Sh. milioni 308.5 za kodi kutokana na kuingiza gari la kifahari aina ya Benzi, Januari, mwaka huu.

Naibu Kamishina wa TRA Zanzibar, Juma Bakary Hassan, aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kinazini, Unguja kuwa gari hilo ilingizwa na mfanyabishara huyo kupitia kampuni yake ya Mifuko Turky ya Zanzibar.

Juma alisema, kiwango hicho cha kodi kinatakiwa kulipwa baada ya maombi ya masamaha wa kodi kukataliwa mara mbili na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dk. Saada Mkuya Salum.
View attachment 2353084
“Baada ya maombi ya msamaha wa kodi kukataliwa mara mbili na kutakiwa alipe, waliomba kufanyike tathmini upya baada ya kutia shaka kiwango walichokuwa wanatakiwa kulipa kwamba ni kikubwa lakini hesabu ilikuja ile ile ya mwanzo kulingana na thamani ya gari,” alisema Juma.

Alisema, baada ya kutakiwa alipe, aliomba wapewe muda wa kulipa kidogo kidogo kwa madai hali ya kifedha si nzuri na kulazimika kupewa miezi mitatu kuanzia Mei hadi Agosti, mwaka huu.

“Mpaka muda unamalizika Agosti, amelipa Sh. milioni 138 na bado wanadaiwa Sh. milioni 170 kati ya Sh. milioni 308 .5 alizopaswa kulipa. Tunajiandaa kuhakikisha fedha hizo zinalipwa kupitia bodi ya dhamana aliyokuwa ameweka kwa kutumia taasisi moja ya fedha,” alisema.

Barua mbili za maombi ya msamaha wa kodi zilizotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Sheriff Ali Sharif, ziliweka wazi kwamba, mdaiwa anapaswa kunufaika na msamaha wa kodi kupitia Kampuni ya Mifuko Turky kama mwekezaji.

Hata hivyo, maombi hayo yalikataliwa na Waziri Mkuya kwa sababu muda wa kunufaika kisheria ulikuwa umemalizika baada ya ujenzi wa kiwanda cha mifuko kuwa umekamilika na uzalishaji kuanza muda mrefu.

“Unaweza kunufaika na msamaha wa kodi kama mwekezaji wakati wa ujenzi wa mradi na si baada ya ujenzi kukamilika na uzalishaji unaendelea kufanyika,” alisema ofisa mmoja mwandamizi wa ZIPA.

Wakati hayo yakiendelea, Bodi ya Mapato Zanzibar ilishasajili gari hilo la kifahari na kutoa namba Z-1 kwa malipo ya Sh. milioni 15, na kuonekana likitembea barabarani kabla ya kukamilisha malipo ya kodi.

“Sisi tumesajili na kutoa namba kwa masharti gari lisitembee mpaka wakamilishe taratibu za kodi tukazo kutoa kibali cha umiliki wa gari,” alisema Meneja Uhusiano na Huduma kwa Walipakodi ZRB, Makame Mohammed Khamis.

Gari hilo lenye thamani ya Dola za Marekani 214,668.71, liliingizwa kupitia bandari ya Malindi na kampuni ya uwakala wa mizigo ya Kimataifa HT Motors Group LTD (UK) kwa kushirikiana na kampuni ya uwakala wa mizigo ya ZARA Freight Forwaders ya Malindi, Zanzibar.
Kuna shida gani ya kupewa muda wa kulipa Kwa awamu?
 
Hilo siyo Benz. Ni Bentley.
Aiseee.
Mkuu National Anthem umeiona hio Bentley new model?[emoji1][emoji1]
FbURbz-XkAAAau_.jpg
 
hapana, nchi bado inaamini gari ni anasa, na gari inatakiwa kumikiwa na matajiri tu, nankununua gari inamaanisha una pesa hazina kazi
Ndio utaahira wenyewe huo, watumishi wa Umma wanataka kushindana na wafanyabiashara kuishi maisha ya anasa..

Na Ili kuwakomesha hao wafanyabiashara ndio maana wanawawekea vikwazo na usumbufu mkubwa sana.
 
Inasikitisha sna jmn mam Ni Bora uchukiwe na wote Ila kuwa na msimamo duh inchi hii Ina endeshwa kwa kelele na mlkila kitu kilalmikiwe

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Inabidi watu wenyewe waamue. Waorodheshe vyanzo vya mapato na kiasi gani na vitu gani vifanywe na vipi visifanywe maana hata shule za uma ni bure. So tuamue nani alipe kodi na nani asilipe kodi.
 
Kudiscourage importations ya magari ya kifahari toka nje ni muendelezo wa akili za kimasikini nchini ni SAwa na Sheria ya ant dumping.
Una ant dumping nini SAsa wakati product yeyeto inaenda recycling baada ya matumizi yake kwisha.
Ant dumping principal ilikuwa na maana kabla ya ujio wa recycling industry.
Wanaofanya hivyo kwanza hawana logic ila ni njia ya watumishi wa Umma kutaka kushindana na wafanyabiashara
 
Hii kodi ni sawa kabisa. Gari la kifahari hili. Kama hana hizo fedha basi hata kumiliki hilo gari hapaswi. Makapuku wenzangu kama wewe badala ya kuunga mkono serikali inapotoza kodi kwa mambo ya kifahari ndiyo mnajifanya kupiga kelele. Huoni ni busara wanaotaka ufahari kulipa kodi ili makapuku kama wewe tozo ziondolewe?
Watu wa namna hiyo wapo wngapi? Wapunguze mav8 hapo ndio kweli tutaona nia ya dhati
 
Mkp mtu unanunua gar milinion Mia tano Kweli Kodi ikushibde mm nadhani magar y kifahari kwa nnchi zetu hz za kiafrica hazipazwi na mtu akiliingiza itozwwe Kodi sawasawa haswa hongera Zanzibar piga Kodi had akili iwakae saawa hao wanaonunua magar ya kifahar Mara nyingi ni wahujumu uchumi tu mm ningekuwa commissioner ningepiga mili400 kbsa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Kwa taarifa yako sio magari tuu ya kifahari hata magari ya kawaida Kodi huwa ni kama theluthi ya thamani ya gari,huu ni wehu.
 
Gharama ya usajili wa magari TRA ni kwa ujazo wa injini ya gari (maarufu kama cc). Mfano gari za chini ya cc 1500 unakuta usajili wake ni Tshs. 500,000/=, na zaidi ya cc 1500 inaongezeka kidogo. Yaani hii ni bila kujali aina ya gari, zingatio ni ujazo wa injini. Napendekeza, muundo huohuo wa ujazo wa injini ndio ungetumika kwenye kupata gharama ya ushuru wa gari. Gharama zingekuwa sio kali na wanananchi wangemiliki magari mapya (ya miaka ya karibuni) na hivyo kupunguza uharibifu wa mazingira. Au serikali haipendi wananchi wake wamiliki magari ya kisasa?? DRC vinaenda vyuma vya hatari na vinapitishwa hapahapa nchini kwetu

Mkiona ujazo wa injini sio poa kutumika kama base basi wekeni hata muundo wa gari (salon, SUV, hatchbak na kadhalika,achaneni na habari za CIF, mnaumiza sana wananchi

Kweli kabisa mkuu
 
Hayupo bado wanalazimishwa visheria visivyo tija.Sheria iendane na mazingira, zamani gari ndio ilikuwa anasa sio siku hizi

Sijui kwanini marais wote waliopita na wa sasa hawalizungumzii suala hili, wamelikariq kimyaa, inakera mno mno babaa.

Mkuu, nikuombe tuu, anzisha mada kuhusu suala hili la kushusha kodi/ushuru wa magari.
 
Back
Top Bottom