TRA yaendelea kumkaba koo Toufiq Salum Turky kodi ya gari milioni 308.5

TRA yaendelea kumkaba koo Toufiq Salum Turky kodi ya gari milioni 308.5

Mimi naona ufahari upo. Kulikuwa kuna sababu gani ya kununua mgari wa bei mbaya hivyo wakati gari za bei rahisi zipo na zingeweza kufanya kazi ile ile ukizingatia hiyo gari imenunuliwa kwa matumizi ya kampuni na itapata depreciation allowance kwenye ukokotoaji wa kodi mwishoni mwa kila mwaka wa mapato.
Ni njia moja wapo ya kudiscourage importation za aina hiyo na kuokoa fedha za Serikali ambazo zingekuwa exempted through depreciation allowances kwa huyo mfanyabiashara au investor.

Kwa matumizi binafsi ya gari ambayo si ya kifahari siungi mkono hoja.
Umenene vyema sana mkuu watu Happ wanaongeaongea eti kod kubwa alfu gar imeagizwa kupitia kampuni

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
I
Unaagizaje G Guard Brabus wakati una pesa ya kulia katanga? Kama gari limemshinda kutoa bandarini aseme tumrudishie gharama zake zote, pamoja na riba na hela ya usumbufu na ya kifuta machozi wanaume tuchukue hiyo ndinga, alisikika kaka Mshana Jr akihojiwa na vyombo vya habari vya nje
Gari kashapewa na usajili juu. Yuko nalo nyumbni.. eti hatakiwi kuliendesha hadi analizë kodi.tajir ni Tajir tu
 
Baba yake huyu Kijana ndio aligharimia safari ya Tundu Lissu kutoka Dodoma hadi Nairobi na kuchangia jumla ya Dola laki moja wakati huo (2017)

Mungu amrehemu Mbunge huyo wa Zamani Hayati Turky
Lbda bas serekali inamkomoa makusudically kwa kitendo hcho Cha Bab yake kwenda kinyume na maelekezo ya jiwe

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hii kodi ni sawa kabisa. Gari la kifahari hili. Kama hana hizo fedha basi hata kumiliki hilo gari hapaswi. Makapuku wenzangu kama wewe badala ya kuunga mkono serikali inapotoza kodi kwa mambo ya kifahari ndiyo mnajifanya kupiga kelele. Huoni ni busara wanaotaka ufahari kulipa kodi ili makapuku kama wewe tozo ziondolewe?
Babu inachanganya Sana sijui mitanzania ikoje humu wanaongeaongea utadhani kila mtu Ana gar kumbe hmn kitu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
View attachment 2353083
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema mfanyabishara maarufu wa Zanzibar, Toufiq Salum Turky, bado hajalipa Sh. milioni 308.5 za kodi kutokana na kuingiza gari la kifahari aina ya Benzi, Januari, mwaka huu.

Naibu Kamishina wa TRA Zanzibar, Juma Bakary Hassan, aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kinazini, Unguja kuwa gari hilo ilingizwa na mfanyabishara huyo kupitia kampuni yake ya Mifuko Turky ya Zanzibar.

Juma alisema, kiwango hicho cha kodi kinatakiwa kulipwa baada ya maombi ya masamaha wa kodi kukataliwa mara mbili na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dk. Saada Mkuya Salum.
View attachment 2353084
“Baada ya maombi ya msamaha wa kodi kukataliwa mara mbili na kutakiwa alipe, waliomba kufanyike tathmini upya baada ya kutia shaka kiwango walichokuwa wanatakiwa kulipa kwamba ni kikubwa lakini hesabu ilikuja ile ile ya mwanzo kulingana na thamani ya gari,” alisema Juma.

Alisema, baada ya kutakiwa alipe, aliomba wapewe muda wa kulipa kidogo kidogo kwa madai hali ya kifedha si nzuri na kulazimika kupewa miezi mitatu kuanzia Mei hadi Agosti, mwaka huu.

“Mpaka muda unamalizika Agosti, amelipa Sh. milioni 138 na bado wanadaiwa Sh. milioni 170 kati ya Sh. milioni 308 .5 alizopaswa kulipa. Tunajiandaa kuhakikisha fedha hizo zinalipwa kupitia bodi ya dhamana aliyokuwa ameweka kwa kutumia taasisi moja ya fedha,” alisema.

Barua mbili za maombi ya msamaha wa kodi zilizotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Sheriff Ali Sharif, ziliweka wazi kwamba, mdaiwa anapaswa kunufaika na msamaha wa kodi kupitia Kampuni ya Mifuko Turky kama mwekezaji.

Hata hivyo, maombi hayo yalikataliwa na Waziri Mkuya kwa sababu muda wa kunufaika kisheria ulikuwa umemalizika baada ya ujenzi wa kiwanda cha mifuko kuwa umekamilika na uzalishaji kuanza muda mrefu.

“Unaweza kunufaika na msamaha wa kodi kama mwekezaji wakati wa ujenzi wa mradi na si baada ya ujenzi kukamilika na uzalishaji unaendelea kufanyika,” alisema ofisa mmoja mwandamizi wa ZIPA.

Wakati hayo yakiendelea, Bodi ya Mapato Zanzibar ilishasajili gari hilo la kifahari na kutoa namba Z-1 kwa malipo ya Sh. milioni 15, na kuonekana likitembea barabarani kabla ya kukamilisha malipo ya kodi.

“Sisi tumesajili na kutoa namba kwa masharti gari lisitembee mpaka wakamilishe taratibu za kodi tukazo kutoa kibali cha umiliki wa gari,” alisema Meneja Uhusiano na Huduma kwa Walipakodi ZRB, Makame Mohammed Khamis.

Gari hilo lenye thamani ya Dola za Marekani 214,668.71, liliingizwa kupitia bandari ya Malindi na kampuni ya uwakala wa mizigo ya Kimataifa HT Motors Group LTD (UK) kwa kushirikiana na kampuni ya uwakala wa mizigo ya ZARA Freight Forwaders ya Malindi, Zanzibar.
Inawezekana kabisa Kodi ya gari Tanzania inaanzia robo ya thamani ya gari mpak Muda mwingine inazidi thamani n vizuri watu kucalculate kwenye calculator Yao tra IPO kwenye website mfano Kuna gari Moja inaitwa jaguar nilifatilia inauzwa million 50 Kodi yake ikawa million 100 hii Ndo nchi yetu mzee.
 
Maskini ndiyo mnapiga kelele kumtetea tajiri aliyeamua kununua gari la la kifahari la karibu sh milioni mia saba asilipe kodi! Huu ni unyumbu wa hali ya juu. Mimi nadhani mngeunga mkono serikali itoze kodi kubwa zaidi matajiri wanaotaka kufanya mambo ya kifahari na maskini kama wewe mpunguziwe kodi! Duniani kote magari ya kifahari au vitu vya kifahari kodi yake huwa kubwa.
Sahih kbsa walime Kodi haswa mambo ya kifahar ipigwe kod vzr

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Alikuwa mwanaccm bora kabisa mwenye roho nzuri aliyemdhamini Tundu Lissu Ndege iliyompeleka Nairobi.
Let the family be blessed
Kumbe kisa alimtete lissu ndio maana mnalia asamehewe Kodi ? No Dr saada Kaz hapohapo Kama vip nitume nikalichukue lirudi yad had Kodi ilipwe yote

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Babu inachanganya Sana sijui mitanzania ikoje humu wanaongeaongea utadhani kila mtu Ana gar kumbe hmn kitu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Ni ajabu mkuu. Maskini wanalalamika eti tajiri katozwa kodi kubwa kwa kuingiza gari la kifahari ambalo bei yake ni zaidi ya nusu bilioni! Tena mtu mwenyewe alitaka kufanya ujanja ujanja aingize bure serikali ikagundua. Wanataka nini sasa? Waendelee kulipa tozo huku matajiri wakiingiza magari ya kifahari bila kodi?
 
Ni ajabu mkuu. Maskini wanalalamika eti tajiri katozwa kodi kubwa kwa kuingiza gari la kifahari ambalo bei yake ni zaidi ya nusu bilioni! Tena mtu mwenyewe alitaka kufanya ujanja ujanja aingize bure serikali ikagundua. Wanataka nini sasa? Waendelee kulipa tozo huku matajiri wakiingiza magari ya kifahari bila kodi?
Inasikitisha kwa Kweli nimeshasema matahir wengi Ni wahujumu uchumi hvyo wasiachwe kirahis rahis na sehemu ya kuwapata Ni ktk Kodi za mambo ya ya kifahari tu hkn namna

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom