TRA yafafanua ongezeko la ushuru wa magari

TRA yafafanua ongezeko la ushuru wa magari

Mie nilitegemea magari madogo yote yangeshushwa kodi na kuwa mil 3.5 chini ya CC 1500 ili wakushanye kodi zaidi ila mtanzania nayeye aone serikali yake inamjali nchini kwake mambo rahisi

Ila hichi walichokifanya ni kupoteza mapato mengi mno tofauti na mategemeo yao,kumiliki Gari ni ndoto ya watu wengi ila Serikali yetu sio rafiki kwa Raia wake,wachache wanaoshiriki wanakisea sana as kama hawajii maisha ya Mtanzania.

Hata hayo makubwa pia hakuna sababu ya kuweka kodi kubwa unamkomoa nani? Alaf kodi ya Magari Serikali inapokea tu pesa kutoka kwa Mwananchi hakuna inachopoteza

Ila pia wajitafakari TRA kuna malalamiko mengi sana ya kodi kipindi hiki tena sana Mtanzania kawa kama mtoto wa kambo kwa nchi yake
 
Duuh hii kubwa kuliko!

Na bahati mbaya magari huwa hayaandikwi mwezi na tarehe halisi ya kutengenezwa kwake bali huandikwa mwaka gari lilipo tengenezwa. Kwahiyo mwaka ukibadilika tu, tayar TRA wanakusanya mara mbili ya kodi kama umri wa gari unakua ule unao elekezwa kisheria.

Yote haya yanatokana na TRA kutokutoa elimu sahihi kwa walipa kodi.Wanatuvizia kwenye ujinga wetu na kututoza pesa ambazo hatukujiandaa nazo
 
Kisichoeleweka hapo ni nini, amesema kuwa ushuru unatozwa kulingana na umri wa gari, kwa walioagiza magari mwishoni mwa mwaka jana yakafika mwaka huu, ni dhahiri kuwa mwaka umeongezeka na ushuru inabidi upande kwa kuwa kama gari ilikua na miaka 8 mwishoni mwa mwaka jana kwa sasa sio nane tena ni 9 .. kwa hapa Uganda kama ilikua na miaka 14 isingewezekana tena kuingiza nchini kwakuwa kwakuwa nchi hairuhusu magari chakavu yaliyozidi miaka 15 .. Mi5 tena [emoji109][emoji109] ..
 
Duuh hii kubwa kuliko!

Na bahati mbaya magari huwa hayaandikwi mwezi na tarehe halisi ya kutengenezwa kwake bali huandikwa mwaka gari lilipo tengenezwa. Kwahiyo mwaka ukibadilika tu, tayar TRA wanakusanya mara mbili ya kodi kama umri wa gari unakua ule unao elekezwa kisheria.

Yote haya yanatokana na TRA kutokutoa elimu sahihi kwa walipa kodi.Wanatuvizia kwenye ujinga wetu na kututoza pesa ambazo hatukujiandaa nazo

Sio kweli ukiingia kwenye google andija JP CENTER unaingiza aina ya gari na chassis ya gari inakuonesha gari imetengenezwq mwezi gani na customs wanaitumia hiyo
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetolea ufafanuzi taarifa juu ya kupanda kwa gharama za kodi za magari yaliyotumika yanayoingia nchini.
Ufafanuzi huo umekuja wakati kukiwa na malalamiko ya wafanyabiashara ya magari wakidai kuwepo kwa ongezeko la kodi za magari ya mitumba.

Taarifa ya TRA iliyotolewa katika gazeti la Mwananchi leo Ijumaa Januari 8 imekuongezeka kwa ushuru wa baadhi ya magari kuanzia Januari mwaka huu kutokana na uthaminishaji uliozingatia bei halisi za magari hayo, huku pia magari mengine yakishuka bei.

“Kimsingi ongezeko hilo limetokana na bei halisi ya magari husika na hivyo haimaaishi kwamba TRA imeongeza ushuru wa magari,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

TRA imesema kuwa magari yaliyotumika hutozwa ushuru wa bidhaa kutokana na umri wa gari ambapo umri wa gari huhesabiwa kwa kufuata mwaka wakalenda.
Kwa upande wa magari madogo yenye umri wa maika minane hadi tisa pamoja na kodi nyingine hutozwa ushuru huo wa bidhaa kwa asilimia 15 na gari yeye umri zaidi ya huo hutozwa kwa asilimia 30.

“Hivyo ikiwa mwagizaji aliagiza gari binafsi lenye umri wa miaka tisa mwaka 2020 na likaingia nchini mwaka 2021 itatozwa ushuru wa bidhaa kwenye umri wa asilimia 30 badala ya asilimia 15 ambayo ingetozwa ikiwa gari yake ingewasili kabla ikiwa gari yake ingewasili kabla ya mwaka huu,” imesema TRA.

Mamlaka hiyo imefafanua kuwa kutokana na sababu hiyo waigizaji wa magari yenye umri huo waliagiza mwaka 2020 na kuingia mwaka 2021 ni wazi kuwa kodi kwenye gari aliloagiza itaongezaka hivyo wakasema hakuna kiwango cha kodi kilichoongezwa kwenye magari.

TRA imesema katika taarifa hiyo kuwa uthaminishaji wa bidhaa hufanyika kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya forodha ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 iliyorejewa mwaka 2019 kikisomwa pamoja na jedwali la nne la sheria hiyo.
Lakini gari si iliagizwa katika quater ya mwisho wa mwaka kwanini wali treat kama limeagizwa mwaka mpya?
 
Na ukiwafuata HQ wanakwambia Mambo yote Ni kwenye system mkamalizane huko huko, system ndio inajua Ni nn kinatakiwa kirudishiwe kwenye annual return.au ndio tunataka tufikie trillion 300 kwa mwaka!?
Tra nako visanga tupu,Tunataka kutengeneza mabillionea kwa njia ipi!?[emoji24]
Wapangishaji wa majengo nao hawataki Kodi miezi 6 Ni mwendo wa mwaka tu sasa hv [emoji867]

Mnapoambiwa kuishi kishetani ndiko huko
 
Back
Top Bottom