TRA yafungulia akaunti zote za Wafanyabiashara zilizokuwa zimefungwa kutokana na madeni ya kodi

Ila ukae ukijua watanzania bado hatujafikia utaratibu wa kulipa kodi kwa hiari!! Elimu ya kuona fahari kwa kulipa kodi hatuna!! Ukiweka loop hole ya watu kukwepa kodi utegemee watakwepa kodi!
Hebu tupeni data za malipo ya kodi kwa March na April tuanzie hapo kuona picha kamili!
 
Bila kusimamia kidete ukusanyaji wa kodi KAZI IENDELEE itakuwa nj ngonjera isiyotekelezeka! Wafanyabiashara ukiwalegezea kidogo hawawezi kulipa kodi kwa uaminifu!! Bado wanaamini kulipa kodi ni uonevu!! Bado wengi wanakwepa kutoa risit za EFD!!
 
Lakini TRA walivuka mipaka unaendaje kufungia akaunti ya mtu ya mshahara? Fungia akauti ya biashara basi.
 
Ubaya ni kuwa mmeachia zikiwa zero...mipunga yote mmeivuta huko...sasa ina maana gani ?? Rufaa ya kodi itachukua miaka 5 hivi ukishinda ndio mtakatana kila mwaka ....upuuzi mtupu watu wameibiwa 40bil huko ukirudisha account zero inamsaisia nini ???
 
Hongera kwa kitabu mkuu, lakini nina maswali machache

1. Soko kubwa unalolenga wanunuzi wa kitabu ni watu wa nje au wa Tzania?

Nimeuliza kwa kuwa nimeona suala hili sana mtu analenga kitu kiuzwe Tzania kama hicho kitabu hlf anaandika kw Eng wakati asilimia 99% ya watz wote tunaongea kiswahl tu.
 
Safi sana Mama. Sasa hivi kila mtanzania ni kazi na bata na mapesaaa ya kutosha mtaani mpaka msemo wa laki si pesa milioni ni ya bia mbili tu urudi.
Wabongo bwana ulaya mwenyewe tu usulipe Kodi uone moto wake hii nchi Ina watu WA hovyo sana unataka maendeleo alafu unawachekea wakwepa kodi

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu upo Mwanza eh? Imenikuta the same issue.. kuna vijana waelewa sana na wanasikiliza kwa makini sana na ukarimu sana, hongera sana kwao

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Umeongea pumba tu uyo jk aliekua akilipa mishahara mwezi unaofata tarehe 5 kwenda huko ndio WA kumuongelea hapa? nchi ilichoka kila sehemu umeme kukatika hovyo,panya road Leo mnajitia kusahau hii nchi Ina viumbe WA ajabu Sana,Bila Kodi Hakuna maendeleo lipa Kodi ili usiingie matatizoni

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 

Kama unafungia account wafanyabiashara 6 katika 10 mfungaji ndo tatizo. Mwisho utabaki na bodaboda na machinga wasio na account za kufunga. Watu hawataweka pesa bank. Utaua uchumi wako.

Mtu kaleta hesabu zake on time 2015 wewe unakaa nazo kindezi mpaka 2021 halafu unamcharge interest na penalt ya kakodi kilikosahaulika kuanzia 2015 mpaka 2021. Kuna ujinga ujinga sana.
 
Aliyekua kamishna mkuu aliyeondolewa alikua na PhD. Hii itakua PhD ya Mambo ya saluni.
Utamfungiaje mtu akaunti? Maana yake Ni kwamba asizalishe kabisa, halafu asilipe Kodi kabisa. Sawa na kukata mkono unaokulisha.
Sheria inasemaje
 
Hii nchi kuna vitumbua kweli. Kodi inakusanywa kwa haki na akili acha kuponda awamu zilizopita.

Mm nimeshuhudia mfanyabiashara kapeleka hesabu kwa wakati tra imekaa nazo miaka 5, inakuja kuzipitia inasema kuna kakodi hukukalipa kalipe na adhabu kila mwezi kwa miaka yote na interest juu.

Wakati bado haelewi kwann pesa yote hiyo account inafungwa anapachikwa jina MKWEPA KODI.

Angekuwa anataka kukimbia kodi angeleta hesabu? Usingekaa na hesabu zake kodi ingekuwa kubwa isiyolipika?

TUWAPENDENI WAFANYABIASHARA WANA UMUHIMU NCHINI SANA.
 
Zimeachiwa zikiwa na Zero bal,,,

Zko Empty,,
 
Nafikiri huu utaratibu unatakiwa uwe wa kimahakama na kisheria na sio utashi wa TRA.Kodi inapokuwa ni deni basi ipelekwe mahakamani kama kesi ya madai na iendeshwe kama kesi ya madai.Kama kesi ni Kukwepa kodi basi ifanywe kama Jinai.
 
Wewe ni binadamu mwongo, fanya utafiti ikiwezekana fanya biashara.

Utaratibu wa kodi ni kukadiriwa au kujikadiria. Wanaojikadiria wanapeleka hesabu kila mwaka wa biashara, Kuna mashine za mauzo kwa aliyekuuzia na ww unayenunua. Kwa mfumo huu huwezi kwepa kodi kwa muda mrefu usikamatwe. Ukwepaji upo ila si wa mda mrefu utadakwa tu.

Tatizo ni kutaka kodi isiyo halali, mtu ana mali kauli kapewa auze, anauza anabakiwa na kafaida anarudisha pesa za watu, ww TRA unaona mzunguko wa m900 kwa mwezi kwenye account unahisi mtu anatengeneza pesa na ana pesa unataka kodi kubwa. Kumbe kwenye m900 mtu anachobaki nacho ni m3 zingine zote si zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…