TRA yafungulia akaunti zote za Wafanyabiashara zilizokuwa zimefungwa kutokana na madeni ya kodi

TRA yafungulia akaunti zote za Wafanyabiashara zilizokuwa zimefungwa kutokana na madeni ya kodi

Nafikiri huu utaratibu unatakiwa uwe wa kimahakama na kisheria na sio utashi wa TRA.Kodi inapokuwa ni deni basi ipelekwe mahakamani kama kesi ya madai na iendeshwe kama kesi ya madai.Kama kesi ni Kukwepa kodi basi ifanywe kama Jinai.
Akili kubwa.
 
Wewe ni binadamu mwongo, fanya utafiti ikiwezekana fanya biashara.

Utaratibu wa kodi ni kukadiriwa au kujikadiria. Wanaojikadiria wanapeleka hesabu kila mwaka wa biashara, Kuna mashine za mauzo kwa aliyekuuzia na ww unayenunua. Kwa mfumo huu huwezi kwepa kodi kwa muda mrefu usikamatwe. Ukwepaji upo ila si wa mda mrefu utadakwa tu.

Tatizo ni kutaka kodi isiyo halali, mtu ana mali kauli kapewa auze, anauza anabakiwa na kafaida anarudisha pesa za watu, ww TRA unaona mzunguko wa m900 kwa mwezi kwenye account unahisi mtu anatengeneza pesa na ana pesa unataka kodi kubwa. Kumbe kwenye m900 mtu anachobaki nacho ni m3 zingine zote si zake.
Kweli tupu,wafanyabiashara wengi,ni mikopo,sio mali zao.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Katika gazeti la Mwananchi, TRA wamefungulia accounts za wafanyabiashara zilizokuwa zimefungwa.

Accounts zilikuwa na mabilioni ya fedha lakini unarudishiwa account inasoma zero ,haina hata senti tano.

TRA wanasema fedha zilitumika kulipa taasisi zilizokuwa zinaidai Serikali.

Imagine serikali inapora fedha za wananchi halafu inazifanyia matumizi yake,inalipa madeni.

Serikali ya mwenda zake ilikuwa inawanyanyasa wananchi kwa kisingizio cha kodi.

Je, lini Serikali itarejesha fedha hizo kwenye account za wafanyabiashara ili wafanyabiashara wazifanyie biashara zao?
 
Muda utaongea. Kama staili hii ya kukusanya kodi kwa wabongo kwa kubembelezana inatufaa au haitufai, namba zitatuambia. Kama makusanyo ya kodi ya TRA kwa mwezi yatabaki tarakimu hizo hizo au kupanda angalao kidogo, basi utaratibu huu ni mzuri na wa kupongezwa. Kama makusanyo ya kodi kwa mwezi yataporomoka, basi utaratibu huu wa kujadiliana na kubembelezana kwa wabongo hautufai na itabidi utaratibu wa awali urejeshwe. Lakini ninavyowajua wabongo mhhhh, ngoja tusubiri na wala tusije tukasingizia corona!

Awamu iliyopita ilikuwa ya kupika data sana ,nani ana uthibitsho kwamba tulikuwa tunakusanya trilioni 2 kwa mwezi? Kama tulidanganywa kwamba ATCL inapata faida,vipi kuhusu mambo mengine? Kudai kodi kibabe ndio chanzo cha kupiga mweleka kwa uchumi wetu maana TASK force walikuwa wanapora mali na si kukusanya kodi.
 
Wewe ni binadamu mwongo, fanya utafiti ikiwezekana fanya biashara.

Utaratibu wa kodi ni kukadiriwa au kujikadiria. Wanaojikadiria wanapeleka hesabu kila mwaka wa biashara, Kuna mashine za mauzo kwa aliyekuuzia na ww unayenunua. Kwa mfumo huu huwezi kwepa kodi kwa muda mrefu usikamatwe. Ukwepaji upo ila si wa mda mrefu utadakwa tu.

Tatizo ni kutaka kodi isiyo halali, mtu ana mali kauli kapewa auze, anauza anabakiwa na kafaida anarudisha pesa za watu, ww TRA unaona mzunguko wa m900 kwa mwezi kwenye account unahisi mtu anatengeneza pesa na ana pesa unataka kodi kubwa. Kumbe kwenye m900 mtu anachobaki nacho ni m3 zingine zote si zake.
Umeandika upuuzi mtupu hujui tofauti ya income/corporate tax na VAT inavyokusanywa.

VAT ina utaratibu, income tax inautaratibu wake na corporate tax ina utaratibu wake.

Story ya income tax na corporate tax zinafanana for the most part (tofauti ni kwamba you don’t pay income tax, if you pay corporate tax; na formula zake kwenye kudaiwa kodi zina tofauti kidogo) ila zote zinalipwa mara mbili au tatu kwa mwaka kwa mfumo wa estimates and prepayments bases on previous year actual payments.

Kawaida kuna tarehe za malipo ya estimates, tarehe za kumalizia malipo halali baada ya kujifanyia self assessment on end of the year na mambo mengine luluki ya kisheria.

Usipotimiza masharti hayo kuna surcharges, interest and fines luluki za kisheria. Ambazo zinatokana na kuchelewesha malipo, kuchelewa kujaza form, kuongopa na mambo mengine kibao; kila adhabu inatokana na ukubwa kosa.

Maswala ya kodi ni taaluma tofauti na mnavyoyachukulia, tatizo letu ni copy and paste ya mambo bila ya kufundisha walipaji how the system works au kuandaa wafanyakazi wa TRA kuwa na skills sahihi, kuna wengine ukiwasikiliza wanapotoa elimu ya kodi ata ufahamu wa kodi wanazoelezea wanapwaya kwenye maelezo.

Ni story ndefu ambayo, tatizo lipo kwa walipa kodi wengi awajui how taxation works.
 
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imezifungulia akaunti zote za wafanyabiashara ilizokuwa zimeshikiliwa kutokana na madeni ya kodi
Hayo yamesemwa leo mjini Morogoro na Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa (TRA), Richard Kayombo, wakati akitoa mada kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri (TEF).

Kayombo amesema hivi sasa mamlaka hiyo inaingia mikataba ya makubaliano na wafanyabiashara hao wenye madeni ili walipe kwa utaratibu maalum.

Amesema sheria inairuhusuTRA kushikilia akaunti ya mtu yeyote ambaye anadeni la kodi kama njia ya kupata fedha ambazo serikali inadai.

Lakini Kayombo amesema uamuzi wa kushikilia akaunti ya mfanyabiashara huwa ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kama majadiliano kushindikana.

"Sikawaida kushikilia akaunti ya mfanyabiashara na uamuzi huu mara nyingi unakuwaga wa mwisho kabisa baada ya jitihada zingine kushindikana ikiwemo majadiliano na mhusika," amesema Kayombo

"Tumeamua kuziachia hizi akaunti ili sasa tuwe tunakaa mezani na kujadiliana na wafanyabiashara wenye madeni namna bora ya kulipa taratibu taratibu na tunaachana na ule wa kushikilia akaunti zao," amesema Kayombo

Chanzo: NIPASHE
Hao ndio SUKUMA GANG.
Huwezi amini kuwa Rais Samia katoa maelekezo karibia miezi miwili iliyopita, leo ndio wanachukua hatua.
Wasafishwe, kuna vimelea vya Mwendazame hapo.
 
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imezifungulia akaunti zote za wafanyabiashara ilizokuwa zimeshikiliwa kutokana na madeni ya kodi

Hayo yamesemwa leo mjini Morogoro na Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa (TRA), Richard Kayombo, wakati akitoa mada kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri (TEF).

Kayombo amesema hivi sasa mamlaka hiyo inaingia mikataba ya makubaliano na wafanyabiashara hao wenye madeni ili walipe kwa utaratibu maalum.

Amesema sheria inairuhusuTRA kushikilia akaunti ya mtu yeyote ambaye anadeni la kodi kama njia ya kupata fedha ambazo serikali inadai.

Lakini Kayombo amesema uamuzi wa kushikilia akaunti ya mfanyabiashara huwa ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kama majadiliano kushindikana.

"Sikawaida kushikilia akaunti ya mfanyabiashara na uamuzi huu mara nyingi unakuwaga wa mwisho kabisa baada ya jitihada zingine kushindikana ikiwemo majadiliano na mhusika," amesema Kayombo

"Tumeamua kuziachia hizi akaunti ili sasa tuwe tunakaa mezani na kujadiliana na wafanyabiashara wenye madeni namna bora ya kulipa taratibu taratibu na tunaachana na ule wa kushikilia akaunti zao," amesema Kayombo

Chanzo: NIPASHE

Lini serikali itarejesha fedha zilizokuwa kwenye account za wafanyabiashara?🧐​

Katika gazeti la mwananchi, TRA wamefungulia accounts za wafanyabiashara zilizokuwa zimefungwa

Accounts zilikuwa na mabilioni ya fedha lakini unarudishiwa account inasoma zero ,haina hata senti tano

TRA wanasema fedha zilitumika kulipa taasisi zilizokuwa zinaidai serikali

Imagin serikali inapora fedha za wananchi halafu inazifanyia matumizi yake,inalipa madeni

Serikali ya mwenda zake ilikuwa inawanyanyasa wananchi kwa kisingizio cha kodi,

Je lini serikali itarejesha fedha hizo kwenye account za wafanyabiashara ili wafanyabiashara wazifanyie biashara zao?
Hili swali ni la kiwango cha Bunge,sasa subiri bungeni kunavyoulizwa maswali ya Vibamia.
 
Ulikuwa utawala primitive. Magufuli alistahili kuwa kiongozi karne ya 17. Kwa karne hii alikuwa totally misfit. Ndiyo maana alikuwa anaonekana ni kiongozi primitive.
Alikuwa primitive zaidi ya hapo.
Sasa lianze suaka la kuchunguza waliouwawa katika mazingira tatanishi.
Ben Saanane.
 
Kisheria TRA walikuwa SAHIHI NA PESA HAZITORUSHIDISHWA NA KAMA KUNA MADENI KWA HAO WALIPA KODI LAZIMA WATAYALIPA TU. HAKUNA SHORTCUT KWENYE KODI HATA RAIS AWE NANI.
 
Kisheria TRA walikuwa SAHIHI NA PESA HAZITORUSHIDISHWA NA KAMA KUNA MADENI KWA HAO WALIPA KODI LAZIMA WATAYALIPA TU. HAKUNA SHORTCUT KWENYE KODI HATA RAIS AWE NANI.
Kuna mtu kauliza akaunti ikifungwa ndio na fedha zinachotwa?
 
Hili swali ni la kiwango cha Bunge,sasa subiri bungeni kunavyoulizwa maswali ya Vibamia.
Pia kuna fedha na vifaa vilivyoporwa kwenye bureau de change virudishwe kwa wenyewe. Mwendazake alikuwa mtu mwovu sana. Kinachonishangaza kuna watu watu walikuwa wanampenda! Mungu mwema sana!
 
Back
Top Bottom