TRA yampiga faini ya 3,500,000 dereva kisa kapakia tenga 27 za nyanya

EFD MACHINE zinatakiwa ziwe kwenye haya magari ya mizigo(Tandam, singo, canter, scania, mende na nyinginezo) Na Sio kwa wachuuzi wadogo wadogo.

Sasa unaponunua mzigo wako wa kuokoteza kwa wachuuzi wadogo wadogo basi hakikisha unaukatia risiti. Ambapo hizo risiti zinapatikana kwa watendaji wa vijiji.
 
Sawa huo ushuru wa kulipia elfu 1000 kwa gunia ni kawaida.
Ila wao tra hawakutaka hizo risiti. Walitaka risiti zao.
Kama mzigo unatoka shamba thamani ya hizo gunia unazijuaje? Na mzigo ulikuwa unaenda sokoni
Risiti ni rahisi sana kuipata ,kama nilivyokuambia wanakatisha risiti ni hao watendaji wa vijiji. Maana watendaji wana EFD MACHINE na pia Huwa kuna mawakala wa vipimo wanazungukaga
 
Watendaji wa vijijini siku hizi wana EFD machine?
Tangu lini?
Je ni Wote nchini au wa mijini tu?

Unajua nature ya kazi za dereva wa masafa marefu?

Je nirahisi kwake kutafuta mtendaji wa kijiji alipo apatiwe risiti?
Mkuu maswali yako ni marahisi sana tena Sana.
Majibu
Watendaji wa vijijini ambapo mizigo hutoka katika hilo eneo wote wana EFD MACHINE. Na ikitokea hawana(japo haiwezekani) Basi kuna Kitu kinaitwa mageti ya ushuru huko barabarani, nenda kakate risiti hapo.


NB: Naandika kwa uzoefu coz daily niko rodini
 
Mliwapa mi 5 tena, wacha wawanyooshe, sioni huruma.
 
Sijakataa hyo faini.
Suala mzigo ulikuwa unatoka SHAMBA.
Na huyo derev kwa maelezo ya mleta mada.
Dereva alimsaidia tu huyo mwenye mazao yake..
Hata pale mkata Kuna watu ukaa na msgunia yao ya machungwa n.k wanasubiri malori ya kurudi nayo dar.kosa la dereva lipo wapi?
 
I wish ningekuwa commissioner wa TRA ningefukuza kazi hao wafanyakazi wa TRA, huo ni uonevu, common sense inahitajika, we’ve to relax some rule ili kuruhusu watu kukuza/kuanzisha biashara zao
 
Hapa tunamzungumzia transporter lazima awe na efd machine kwa ajili ya kuwapa risiti hao anaowabebea mazao eg tenga moja elfu 2 basi ampe na risiti.
 

Anayetakiwa kutoa receipt ni muuzaji au mnunuzi?

Huyo wa kwenda kwa mtendaji wa kijiji labda yule ambaye kununua labda hiyo kazi ya kununua bidhaa na kwenda kuuza ni ndiyo kazi yake mahususi lakini kwa mtu ambaye ni dereva wa malori ya masafa marefu inakuwa si sawa.

Halafu ni kwambie kitu kwa mikoani huduma za serikali za mitaa ziko scattered kwa sana, Yani ukiwa eneo moja tena mashambani kuambiwa umtafute mtendaji ni mtihani mkubwa sana!

Usichukulie ni rahisi kumfikia mtendaji wa serikali ya kijiji kwa maeneo ya mikoani.
 
I wish ningekuwa commissioner wa TRA ningefukuza kazi hao wafanyakazi wa TRA, huo ni uonevu, common sense inahitajika, we’ve to relax some rule ili kuruhusu watu kukuza/kuanzisha biashara zao
Msipende kuchangia kwa mihemko basi.. Mwenye gari anafanya biashara ya usafirishaji hivyo anatakiwa atoe risiti ya mauzo yake ya huduma ya usafiri. Na kwa magari lazima uwe na EFD na iko wazi faini ya kutotoa risiti za EFD ni 3M - 4.5 M so hapo mi naona wamempa nafuu kabisa kama ofisa nakuwa mimi nanyooka na 4.5M.
 

Ukisoma sheria ya usimamizi wa kodi(2015), nenda kipengele cha 36 imeelezea vizuri kabisa vigezo vya kutumia mashine ya EFD. Twende taratibu mfanyabiashara ambae ana mauzo ghafi ya 14m kwa mwaka(turnover) sheria inamtaka atumie mashine ya EFD na ambae hakidhi hivyo vigezo sheria inamtaka atoe risiti ya mkono ya kuandika ile.

Ila kwa wale wanaofanya proffessional services kama mawakili, consultancy nk hawa wanatakiwa wawe na mashine kwa lazima na lazima wajisajili na VAT (nenda value Added Tax Act,2014, s(29)(2))).

Kama wewe mfanyabiashara unatoa mzigo kutoka store kwenda dukani unapaswa kuandika delivery note inayoonesha jina lako na TIN jumla ya mzigo uliobeba, tarehe na unakoenda huo mzigo.

Kinyume na hapo juu sheria ipo wazi nenda kasome hio sheria ya usimamizi wa kodi(tax administration act) section ya 86 imeelezea offence ya kutotumia mashine, kutotoa risiti na kutoa risiti ambayo sio sahihi hapa imeelezea na faini zake ambapo ni kati ya 3m-4.5million.
 
Kosa la dereva hajampa mteja wake risiti ya kusafirisha mzigo
 
Flexibility ni muhimu, watoe elimu, wanaleta uhasama na serikali
 
Dereva alilipwa transport ambayo kama alilipwa gali sana ni 2000 kwa tenga (54,000 kwa zote) kwenye transport huwa tunaita chombeza na ofisi nyingi haizifuatilii na ndio maana hawazitolei risiti.
 

Mkuu ipo hv mtu ambae hatoi risit anakwepa kodi na kama amesajiliwa na Vat inaamana anakwepa kulipa vat na ili VAT ikusanywe lazima risiti zitolewe hivyo kutotoa risit unaikosesha serikali mapato, hio adhabu ni kuichangia serikali kiasi ulichokuwa unakwepa.
 
Sawa huo ushuru wa kulipia elfu 1000 kwa gunia ni kawaida.
Ila wao tra hawakutaka hizo risiti.walitaka risiti zao.
Kama mzigo unatoka shamba thamani ya hizo gunia unazijuaje?na mzigo ulikuwa unaenda sokoni
TRA wanachotaka kwa mwenye mzigo ni hivi:
1. Risiti ya huo mzigo (na iwe ni risiti ya EFD machine)
2. Ni leseni ya biashara ya mwenye mzigo( na Hii leseni iambatane na Kile unachokibeba zingatia Hili. Isije kuwa leseni yako imeandikwa nyanya halafu Wewe ukabeba parachichi)

TRA wanachotaka kwa mwenye Gari ni.
1. Kadi ya Gari
2. Ni risiti ya ya EFD MACHINE aliyomkatia mteja wake ambayo jina la kwenye hiyo risiti liendane na jina la risiti ya ushuru ya EFD Na pia liendane na jina la leseni ya biashara ya mteja wake. Na pia hiyo risiti ioneshe bei ya mzigo.

NB. Usije ukakosa hivi vitu unaweza ukaongea lugha zote na wasikuelewe. Na pia kama tenga Ziko mia katia zote mia mkuu
 
Hapa tunamzungumzia transporter lazima awe na efd machine kwa ajiri ya kuwapa risiti hao anaowabebea mazao eg tenga moja elfu 2 basi ampe na risiti.

Sheria ya EFD iko wazi anayetakiwa kutoa receipt ni muuzaji, wajibu wa mnunuzi ni kuidai hiyo fiscal receipt toka kwa muuzaji.

Tuanzie hapo halafu lete hoja yako maana sijakusoma vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…