TRA yampiga faini ya 3,500,000 dereva kisa kapakia tenga 27 za nyanya

Thubutu!
Wakulia nani? [emoji2369]

Acha mikwala yako mbuzi hapa!

Kuwa Officer wa TRA ni mgawanyo wa majukumu tu na hao ni watumishi wetu sisi wananchi na wanalipwa kodi zetu!

Tusitishane wala nini!
Kila la Heri mkuu
 
Haha...
Msemo huu unaanza kushika kasi.
Kaka yangu kaniambia kitu kama hicho siku 7 zilizopita.
Tulikuwa tunajadiri biashara flani kwa ajiri ya kupata pesa ya mboga nyumbani.
nadhani watu wengi wameogopa TRA
 
Upo sahihi kabisa. Na haya usemayo nimeyaona kwa upande wa wamikiki wa magari.

Hiki wanachofanya sasa TRA kinawasaidia wamikiki kudhibiti udanganyifu wa madereva.
Mlalamikaji anatetea hii njaa na janja janja ya madereva.

Lakini pia wamikiki wa magari wajali maslahi ya madereva.

Wanaweza kufuata ushauri wangu kwa njia ile ya kwanza au ya pili lakini mmiliki anaweza kupata taarifa zote kupitia rekodi za EFD iliyopo TRA. Ina maana EFD ichukue na namba za usajili za gari. Pamoja na TIN namba ya Dereva au ya kampuni mmiliki wa gari.

Maoni yako mazuri.
Ila utachukiwa na watanzania watetea kupita madili haramu.
 
Lile ni tamko tu, ila halibadilishi nguvu ya sheria waliyonayo hao jamaa
Raisi alizungumzia ushauri wa mazao na siyo kodi ya biashara ya kusafirisha vitu.

Hiyo aliyozungumzia raisi inahusu mwenye mzigo au mkulima na hii ya usafirishaji inahusu mwenye gari au kampuni ya usafirishaji.

Jamaa kachanganya hizo tozo aina mbili tofauti. Hiyo anayolalamikia mdau ni ya usafirishaji siyo ya mazao.
 
Mkuu faini ni adhabu. Mara nyingi inakuwa kubwa kuliko pesa uliyokwepa kulipa ili usirudie tena kukwepa kodi.

Uone ni bora kulipa kuliko kuja kukutana na hiyo adhabu.
 
Wao wanajilipa mamilioni meengii wengine 9, wengine 12, wengine 15 huyu dereva wa watu pengine salary ni laki 5 au 6
Mwenye nguvu mpishe, usipompisha unaumia. Mifumo ya dunia iko hivyo na kamwe dunia haitakaa iwe na haki wala usawa.
 
Mkuu faini ni adhabu. Mara nyingi inakuwa kubwa kuliko pesa uliyokwepa kulipa ili usirudie tena kukwepa kodi.

Uone ni bora kulipa kuliko kuja kukutana na hiyo adhabu.
Ni kweli lakini nini kinatathmini ukubwa upi unatosha?

Thamani ya matenga yote yakija sokoni na kuuzwa haizidi 700,000 hii inamaanisha hata 700,0500 ni kubwa.

Sasa kitathmini cha ukubwa wa adhabu ifike 3,500,000 ni kipi?
 
Ni kawaida sana,kwa Nchi zenye uchumi wa kati,
Nasema uongo ndugu zangu?
 

Hapo umehama topic: Kesi iliyopo siyo kodi ya mzigo au mazao, bali kesi ni kwa dvr kupakia mzigo na kupokea gharama za usafirishaji bila kutoa risiti ya EFD ama nyaraka ya Kampuni ya kibali cha kusafirisha mzigo wa aina hiyo.

I believe sheria hizi zilikuwepo toka zamani lakini kulikuwa hakuna usimamizi serious kama sasa..
 
Kwahiyo kutotoa risiti haijalishi ni ya shilingi 5000, laki saba au laki nane faini ni milioni tatu na nusu?
 
Kwahiyo kutotoa risiti haijalishi ni ya shilingi 5000, laki saba au laki nane faini ni milioni tatu na nusu?

Hiyo ndiyo adhabu iliyowekwa dhidi ya kosa la kukika sheria ya kodi Mkuu..!
 
Mkuu inatakiwa msafirishaji atoe risiti kwa huduma ya usafiri ,
Hapo mwenye mzigo hajaguswa kabisa naye anatakiwa awe na risiti yake , maswala ya kusema nilikuwa namsaidia mtu hayapo kwenye sheria in fact kutokujua tu sheria ni kosa kisheria.
Unaweza kusema nawatetea Tra ,in fact mimi binafsi ni muhanga mkubwa wa hizi sheria za Kodi amabazo zilitungwa kimhemko tu bila kuzingatia Hali halisi.
Hizi sheria zikisimamiwa kikamilifu zitaleta mfumuko mkubwa wa Bei hasa kwa items perishable masokoni ,
 
Hapa tunamzungumzia transporter lazima awe na efd machine kwa ajiri ya kuwapa risiti hao anaowabebea mazao eg tenga moja elfu 2 basi ampe na risiti.
Not a chance , transporter hahusiki na mizigo midogo midogo Kama hiyo , yeye keshaandika ristii yake ya mzigo kwenda kongo anajua gari lake linarudi empty , hawezi kuandika risrit za namna hiyo ni hasara kwake , dereva akijiongeza ndo inatokea mlipuko Kama huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…