TRA yampiga faini ya 3,500,000 dereva kisa kapakia tenga 27 za nyanya

Boss wake alifanya vyema pia.
Si jambo la busara sana kumwibia boss wako.
Pia si busara kuziba riziki za dereva guta, bajaji, kenta ama fuso.
 
Enzi hizo, watu walikuwa huru sana kujiongeza. Hazina ikaishiwa hela kabisa. Nakumbuka Walimu wetu walipata shida sana kwenye mishahara. Kunusuru ikabidi "Sur tax" ianzishwe kwenye magari.
Sasa kwenye vyakula tena vinavyoharibika haraka lazima pawe na utaratibu maalum wa kuvishughulikia, wote tunajenga nchi moja, lakini nchi haiwezi kujengwa na watu wenye njaa au afya mbovu, hilo lieleweke kwa uzuri kabisa.
 
Kwani asili ya uchawi ni nini? Jiangalie na ujitafakari, hiyo roho uliyonayo si nzuri 😂😂
 
Kwani asili ya uchawi ni nini? Jiangalie na ujitafakari, hiyo roho uliyonayo si nzuri 😂😂
Huyu mwache kama alivyo,ila kwenye utawala huu hakuna atakaebaki salama,hata yeye kama si leo basi kesho,ninaimani siku moja atakumbuka huu mjadala unamaana gani.
Utawala huu unatesa raia kuliko mkoloni.
 
Safi sana, hatutaki wababishaji hapa Tanzania.
 
Na yeye ana makosa,,kwanini hakuwa na risiti?,
 
Inakuwa risiti ya bei gani?
Kwa mfano una semi imepakia mahindi junia 300 kutoka simiyu kuja dar,yule mwenye mzigo atakatiwa risiti ya ushuru kila junia tsh 1000 ,sawa na 300,000, hizo anatoa mwenye mzigo na lazima awe na leseni ya kuuza na kusafirisha mazao,anakua anatemb
ea na copy,
Mwenye gari,tuseme makubaliano na mwenye mzigo ni milioni 2 kusafirisha hadi dar,
Hivyo atatia risit ya EFD ya transport, ambayo makato yake ni ya VAT,,about kama tsh laki 3 na ushee,zitakatwa katika hiyo milioni 2 ya transport,,zinazobaki ndo pesa za Transporter
 
.... Si busara wala hekima kuficha elimu ya sheria kwa wahusika ili uwavizie kuwatoza faini! ...
... ndio wanatoa elimu kwa staili hiyo! Wakiitoa kupitia channels au means nyingine haisambai vya kutosha au kufika vizuri kwa walengwa. Kwa njia hii ya "kuumiza" inafika kwa haraka zaidi ndio maana hata sisi tumeweza kuipata kupitia JF.
 
Watendaji wa vijijini siku hizi wana EFD machine?
Tangu lini?
Je ni Wote nchini au wa mijini tu?

Unajua nature ya kazi za dereva wa masafa marefu?

Je ni rahisi kwake kutafuta mtendaji wa kijiji alipo apatiwe risiti?
Mzee,nenda kijiji chochote ndani ndani ukapakie mfano njugumawe,,utashangaa kabla fuso haijajaa mdada huyu hapa na EFD machine,anasubiria hela,yaani haina kukwepa,
Au nasema uongo nduguzanguni..?
 
Sawa huo ushuru wa kulipia elfu 1000 kwa gunia ni kawaida.
Ila wao tra hawakutaka hizo risiti. Walitaka risiti zao.
Kama mzigo unatoka shamba thamani ya hizo gunia unazijuaje? Na mzigo ulikuwa unaenda sokoni
Hiyo risiti aliyopigwa faini,haihusiani na mzigo,,hiyo ni ya Transporter,,yaani mwenye gari kafanya biashara lazima alipe kodi,
Mwenye nyanya analipa ushuru
 
... ndio wanatoa elimu kwa staili hiyo! Wakiitoa kupitia channels au means nyingine haisambai vya kutosha au kufika vizuri kwa walengwa. Kwa njia hii ya "kuumiza" inafika kwa haraka zaidi ndio maana hata sisi tumeweza kuipata kupitia JF.
Duh! Kwa utaratibu huu wa elimu yao hiyo, dereva ameadhibiwa wakati amevunjiwa" haki yake ya kikatiba ya kuhabarishwana kuelimishwa" bila vikwazo!

Si sawa hata kidogo kumnyima raia "haki yake ya kikatiba" wakati huo huo unatunia kunyima haki yake hiyo kumuadhibu.
 
Ni kweli lakini nini kinatathmini ukubwa upi unatosha?

Thamani ya matenga yote yakija sokoni na kuuzwa haizidi 700,000 hii inamaanisha hata 700,0500 ni kubwa.

Sasa kitathmini cha ukubwa wa adhabu ifike 3,500,000 ni kipi?
Faini haihusiani na nyanya,Transporter ndio kapigwa faini
 
Faini zitakuwa nyingi sana kwa sababu watu hawajui kuhusu kodi. Inatakiwa elimu kubwa itolewe kwa watu wote.
 
Hujawahi kufanya biashara acha kujidanya
 
Dereva ni mwizi na mketa hatari, hapo gari likingongana au pindikuwa, bima inakufa na hailipi, na mwenye mali aliyekodisha gari atamdai mzigo wake mwenye gari. Hao madereva kwa uroho wao wanamharibia kazi mwenye gari kwa sababu ya uroho, na hali madereva wanapewa , malipo ya milage.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…