Shule ya St. JUDE wameifungia account zao kisa hawakupeleka watoto wao kwenye kampeni za CCM, kuimba mapambio kama shule nyingine.
Hii nchi kumpa huyu dereva lesseni ya kutuendesha, tumeingia chaka.
1) Mwenye kampuni ya kutembeza watalii, alipie kampuni yake kodi.
2) Na hayo magari yake ya kampuni ya watalii, alipie kodi.
3) Gari likiwekewa mafuta, unakutana na kodi.
4) Dereva nae, alipe kodi lesseni yake na ajira yake sambamba na kodi ya Trafic Police (Vijana wa kukusanya mapato TRA).
5) Mwenye hoteli wanaofikia watalii hao (Pengine mwenye kampuni ya utalii ndio hoteli yake pia), alipe kodi. Ndani ya hio hoteli yake anayoilipia kodi, chumbani kitanda nacho kikilaliwa, kilipiwe kodi.
Halafu serikali tunaambiwa haina hela. Shabaashi.
Wasisahau na KODI YA KUTUMIA VYOO KWA WATALII (Kama Vyoo Vya Kulipia Standi Za Bus).