TRA yotoa ufafanuzi wa madai ya kutengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini usio halali

TRA yotoa ufafanuzi wa madai ya kutengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini usio halali

Ngoja nichanganue hili sakata kwa nilivyoelewa mimi.

Mfanyabiashara Ameingiza bidhaa zake nchini kupitia kampuni ya tosh cargo

Tosh cargo amesafirisha na kukamilisha taratibu zote za forodha na kukabishi mzigo kwa mteja wake.

Shida inaanzia hapo kwenye (Amesafirisha na kukamilisha taratibu zote za forodha)

Wakati mfanyabiashara anapelekea mzigo wake huko unapotakiwa kwenda gari ikapata ajali na kusababisha uharibifu na upotevu wa mali.

Kwakua mfanyabiashara alikua na bima, akaanza mchakato kufatilia ili apate fidia ya mali yake iliyoharibiwa na tukio la ajali.

Kampuni ya bima inawajibika kumlipa mteja wake, lakini kabla hawajamlipa lazima wapate nyaraka zote muhimu kuhusu mali zilizopotea, ikiwa ni pamoja na nyaraka zote halali za kikodi na mengineyo ili wapate uhakika wa thamani na uhalali wa wanachoenda kulipa.

Sakata linaanzia hapa kwenye nyaraka.

TRA hawatambui mali ya mlalamikaji, kwanini hawaitambui na hawajaiona kwenye mfumo?

Kuna mawili hapa;

1. Tosh cargo wameingiza mzigo kama mali yao, hivyo mteja mwenye mzigo hatambuliki na mfumo mzima wa TRA.

2. Rejea namba moja 😂, kama mfumo haukusomi basi unamsoma aliekamilisha clearance ya mzigo.

Kama Nyaraka za TRA hazikutambui kampuni ya Bima itakufidia vipi na umeshindwa kutoa vielelezo vya uhalali wa mali iliyoharibika, vipi kama umekula njama na mtu baki utumie mgongo wa mali yake iliyoharibika kujipatia bima kwa njia ya udanganyifu?

Swali jingine la msingi kwa mfanyabiashara.
Asijekua anataka huruma ilhali nayeye anajua fika changamoto ambazo zingejitokeza.

Je kabla ya kupata matatizo yote ya ajali n.k, aliridhika na nyaraka zote alizokabidhiwa baada ya kupewa mizigo yake, au akili imekuja kukaa sawa baada ya matatizo?
Umeelezea vizuri sana. Kuna wengine hapa wanachangia bila kujua tatizo ni nini hasa. Kwenye swali lako la mwisho ni kama nimesikia akisema kuwa aliambia kuwa utaratibu wa TRA unaruhusu mtu kuingiza mzigo wake kwa jina la hiyo kampuni. Inawezekana ndani ya TRA kuna wajanja wanatumia hii njia ili kupiga fedha. Na kama ni hivyo basi ni lazima kuna top personnel wanahusika kwa sababu jambo kama hili haliwezi kufanywa na ngazi za chini tu. Si ajabu hata waziri anahusika. Anyways, ni mwendelezo ule ule wa watendaji wa serikali kupiga kwa sababu juu, kuanzia kwa rais nako kumeoza.
 
Hili ni bomu ambalo inatakiwa kitu cha kwanza Wazziri wa Fedha, Makamishnana, manaibu Kamishna, vyombo vya usalama vyote waliopo TRA wanaohusiana na bandarin, wote wasimamishwe kazi wawekwe wengine haraka sana, uchunguzi wa kina ufanyike.

Hawa ndiyo wanaochelewessha maendeleo.

Huyo Mfanyabiashara apewe ulinzi wa saa 24, watamfinya.

Wameshaonesha wanataka kumgeuzia kibao. Barua ya kujibiwa ndani ya muda mchache kwanini ikae miezi kujibiwa?

Tena inaonesha imejibiwa ile "ficha kombe mwanaharamu apite).

Mama aSamia, nnauhakika hili limeshafika mezani kwako.
Kwa hili, tupo pamoja.
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu malalamiko ya Bw. Emmanuel Gadi kuwa, TRA imetengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini nje ya mfumo halali wa Serikali kinyume na Sheria ya Forodha.

Tunapenda kuufahamisha umma na jamii kwa ujumla kuwa, Mamlaka haina mfumo wowote mwingine inaouendesha wa kuingiza mizigo nchini nje ya mfumo wa Forodha wa TANCIS ambao unatumika kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACCMA).

Bw. Emmanuel Gadi alifikisha malalamiko yake kwa njia ya barua tarehe 27 Februari, 2023 akidai kupewa uthibitisho na TRA wa kuingiza mzigo wa vifurushi 471 vya “Toner Cartridges’’ kupitia kampuni ya Tosh Logistics Ltd. TRA ilifanya uchunguzi wa kutosha na kuthibitisha kwamba, hapakuwa na mzigo wowote ulioingizwa nchini kwa jina la Wintech Tanzania Ltd wa vifurushi 471 vya “Toner Cartridges” kupitia kadhia yenye namba TZDL-22-1382193 ya tarehe 18 Agosti 2022 kama anavyodai.

Hivyo, TRA ilimjibu mhusika kupitia barua yenye kumbukumbu namba CF 8/92/01 ya tarehe 25 Julai 2023 ikimjulisha kuwa, kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa “House Bill of Lading” na kutoonekana kwa mzigo huo kwenye kadhia iliyowasilishwa na kampuni ya Tosh Logistics Ltd, TRA isingeweza kuthibitisha kuingizwa kwa mzigo huo nchini.

Kupitia taarifa yake aliyoitoa kwenye vyombo vya habari tumebaini kuwepo viashiria vya ukwepaji kodi kwani ni dhahiri kuwa mzigo huu uliingizwa kwa njia za magendo. TRA inamtaka mlalamikaji kuwasilisha nyaraka na uthibitisho wa kampuni yake kuingiza mzigo huo nchini mara moja ili hatua stahiki zichukuliwe.

===========
Video ya Mfanyabiashara akiituhumu TRA
Pole yako, mfanya biashara.

Naungana nawe, na nakushukuru kwa ujasiri wako wa kujitokeza na kuonyesha waziawazi uozo mkubwa uliopo ndani ya nchi yetu sasa hivi.

Lakini naishia hapo. Hatua ya kuomba Rais akusaidie wewe na kuacha uozo uleule ukiendelea kwa wengine kunakuondolea hata hiyo huruma ndogo na sifa ya ujasiri uliyoionyesha hapa.

Huyo huyo rais, kwa udhaifu wake ndiye chanzo cha matatizo haya yanayowakabili nyinyi na sisi wengine wote katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
 
Emma wanamuonea kabisa Kabisa na ile ajari ya mzigo ndio imezibua uozo wa TRA hata ingekua Nani Lazima angekua katika situation Kama hii, Taasisi ya Bima haiwezi kunilipa bila ya valid documents za forodha under a valid process with EACCMA, kitu ambach TRA hawaku a bid hapo mwanz na Emma hawezi kutupilia mbali malipo yake kutoka kwa Kampuni ya Bima

TRA wamtoe tu mtu sadaka tu
Nahisi huyo jamaa kanufaika na huo mfumo miaka nenda rudi sema hiyo ajali aliyopata watu wa Bima wanahitaji documents huyo jamaa angepiga kimya tu
 
Hili ni bomu ambalo inatakiwa kitu cha kwanza Wazziri wa Fedha, Makamishnana, manaibu Kamishna, vyombo vya usalama vyote waliopo TRA wanaohusiana na bandarin, wote wasimamishwe kazi wawekwe wengine haraka sana, uchunguzi wa kina ufanyike.

Hawa ndiyo wanaochelewessha maendeleo.

Huyo Mfanyabiashara apewe ulinzi wa saa 24, watamfinya.

Wameshaonesha wanataka kumgeuzia kibao. Barua ya kujibiwa ndani ya muda mchache kwanini ikae miezi kujibiwa?

Tena inaonesha imejibiwa ile "ficha kombe mwanaharamu apite).

Mama aSamia, nnauhakika hili limeshafika mezani kwako.
Leo umenikosha sana. Heko bibi!
 
Naona mifumo fake ya ukusanyaji mapato imeenea sana. Tuliambiwa tena na Rais mwenyewe kuwa huko Mbeya kuna Halmashauri ilikuwa na mfumo tofauti wa Tax collection. Majizi kila mahali
 
Naona mifumo fake ya ukusanyaji mapato imeenea sana. Tuliambiwa tena na Rais mwenyewe kuwa huko Mbeya kuna Halmashauri ilikuwa na mfumo tofauti wa Tax collection. Majizi kila mahali

Mifumo yote inatakiwa iwe audited na approved na gov body husika.
Hili suala la kuwa na mifumo ya pembeni halijaanza leo wala jana.
Taasis nyingi wana mifumo ambayo sidhan serikali iko aware. Na humo humo ndipo wanapitia kufanya yao
 
Umeelezea vizuri sana. Kuna wengine hapa wanachangia bila kujua tatizo ni nini hasa. Kwenye swali lako la mwisho ni kama nimesikia akisema kuwa aliambia kuwa utaratibu wa TRA unaruhusu mtu kuingiza mzigo wake kwa jina la hiyo kampuni. Inawezekana ndani ya TRA kuna wajanja wanatumia hii njia ili kupiga fedha. Na kama ni hivyo basi ni lazima kuna top personnel wanahusika kwa sababu jambo kama hili haliwezi kufanywa na ngazi za chini tu. Si ajabu hata waziri anahusika. Anyways, ni mwendelezo ule ule wa watendaji wa serikali kupiga kwa sababu juu, kuanzia kwa rais nako kumeoza.
Hili jambo lina big fraud ndani yake,lichunguzwe kwa kina na ukweli uwekwe wazi kwa jamii,maana Mlalamikaji hadi kusema yuko tayari afungwe pingu kama anasema uwongo si jambo dogo kama tunavyozani! Mamlaka zinazo husika wote kwa pamoja walifanyie kazi, ni muhimu sana mifumo yote ikasomana!!
 
Atajua... Na huyo alie shauri aende kwenye midia ndio kampoteza.

Pale unapokuwa na invoice na packing list halali kutoka Kwa supplier ila Kwa wakala wa forodha unapeleka documents tofauti.. Lazima kiumane tu...

Loophole ya mfumo ikukunufaisha mara moja bhas shukuru.. Ila usichukulie ndio utaratibu.
 
Hujaelewa. Wao walikuwa na mfuo wa kuiba hivi unategemea wasemeje????? Yaani TRA hata ningekuwa mimi ningekataa kwa sababu ni mfumo fake
Hivi Mama Bonge wa vitenge walimaluzana vp na TRA!? Maana lile sakata humu hadi Waziri mkuu aliusishwa nae kwenye mavitenge
 
Nahisi huyo jamaa kanufaika na huo mfumo miaka nenda rudi sema hiyo ajali aliyopata watu wa Bima wanahitaji documents huyo jamaa angepiga kimya tu
Apige kimya vp wakati hizo documents ziko TRA for record in case of emergency when needed!!
 
Back
Top Bottom