TRA yotoa ufafanuzi wa madai ya kutengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini usio halali

TRA yotoa ufafanuzi wa madai ya kutengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini usio halali

Hahaa good analysis mkuu.
Sababu unaponunua bidhaa nje lazima BL(documents) zitangulie kwanza kabla ya mzigo means unajua mnunuzi na gharama. Sasa kama itakuwa kama ilivyosema hapo juu maana yake alijua tangu awali.

Au basi mzigo umetoka kwa arrangements za " nje ya uwanja" japo documents ni za kwake kweli ndomana TRA hawatambui. Hapo kuna mengi mkuu.

Hapo kwenye nyaraka naamini hakuna shida, bila shaka invoice ilikuja kwa jina lake na malipo akafanya hata kama hakufanya kunakuwa na arrangement inayompa obligation hiyo. Hivyo sitarajii kuwe BL inayosoma taarifa za mtu mwingine kwa mzigo wa mtu mwingine.

Clearing hapo ndo janja ilipofanyika. Period.
 
Kwani yule wa kkoo aliishia wapi alipata msaada baada ya kulalamika mbele ya Rais na vyombo vya habari? Tuanzie hapo nadhani
 
Ila walipoua wayahudi 1,300 ilikuwa ni sawa?
Usiamini kila unachokisikia kutoka kwa wayahudi, myzhudi anawezzza kuuliwa mmoja akasema "tumeuliwa elfu moja".

kwani kbala ya shambulio la Hamas wayahudi wameshwauwa wapalestina wangapi? Au hilo hiluielewi?
 
Yuko sahihi ila vita aliyoichagua ni ngumu sana
Huyo ni hamas, alishaamuwa kufa zamani sana. Kidume hicho hakitaki kuuliwa kibiashara huku kinatazama tu.

Si umesikia walivyomtisha?

Nnavyoijuwa Tanzania, huyo ndiyo wa kuungwa mkpo na kila Mtanzania. Wapo wengi sana wanaoonewa namna hiyo.

Na huyo godown lake lingekuwa halijawaka mto na asingetakiwa na kampuni ya bima kupeleka vielelezo, yasingejulikana kabisa hayo. Hata yeye alikuwa hafahamu, anajuwa kila kitu kinakwenda kihalali tu.
 
Atajua... Na huyo alie shauri aende kwenye midia ndio kampoteza.

Pale unapokuwa na invoice na packing list halali kutoka Kwa supplier ila Kwa wakala wa forodha unapeleka documents tofauti.. Lazima kiumane tu...

Loophole ya mfumo ikukunufaisha mara moja bhas shukuru.. Ila usichukulie ndio utaratibu.
[emoji38]
 
Mizigo ya loose cargo nikuwa mizigo ya watu tofauti inakusanywa kwenye kontena moja na kampuni ya usafirishaji inasafirisha kama mali yao.Ndiyo maana unachajiwa kwa CBM na unalipa kwenye kampuni ya usafirishaji bila kwenda mwenyewe forodha.

I think baada ya TRA kupata hili zengwe la huyu jamaa wakaja na mfumo wa kila mtu alipie forodha,ambapo kwenye mgomo wa Kkoo kipindi kile watu waliupinga huu utaratibu.Maana ilikuwa let’s say kontena ina mizigo ya watu 100,kila mmoja inatakiwa akalipie ushuru forodha.

Kitu ambacho hawakujua ndio kama sasa hivi inakuwa ngumu bima kulipa bila nyaraka za uingizaji mzigo.TRA walilijua hili ila kwa kuwa walikuwa wananeemeka bila kesi wakapuuzia.
Kuna mtu atatolewa mbuzi wa kafara kwenye hili.
Hapa uko sahihi kabisa...
Mizigo mnaingiza wengi....naona hapo kaitaja Hadi kampuni ya opo agency....
Sasa ishu Iko hivi Kwa mtizamo wangu...
Kama mtu anaingiza mzigo mkubwa ni Bora mzigo aulipie kodi mwenyewe(sijui hako kamchakato ) kamekaaje.....ila nachojua mpaka Sasa watu wanaingije mizigo Hadi ya milioni 200 kupitia agency hizi...
Na hakuna aliyekua anaona Kuna umuhimu WA kuingia yeye kama yeye....na hata tra walivyosema Kila mtu alipie mwenyewe watu waliona ni usumbufu lakin ukweli ni kwamba kwenye hili janga huyu jamaa sidhan kama atapa stahiki yake...
Alafu kingine tra hawamjui....Hilo ni sahihi maana hajaingiza mzigo yeye...dah
Sasa sisi wenye vi loose cargo tufanyeje jamani....
Na je wakiusimamia mfumo WA kulipa moja Kwa moja kule SI ni wazi kwamba makadirio ya kodi yatakuja makubwa....Bado umlipe agent
 
Umeelezea vizuri sana. Kuna wengine hapa wanachangia bila kujua tatizo ni nini hasa. Kwenye swali lako la mwisho ni kama nimesikia akisema kuwa aliambia kuwa utaratibu wa TRA unaruhusu mtu kuingiza mzigo wake kwa jina la hiyo kampuni. Inawezekana ndani ya TRA kuna wajanja wanatumia hii njia ili kupiga fedha. Na kama ni hivyo basi ni lazima kuna top personnel wanahusika kwa sababu jambo kama hili haliwezi kufanywa na ngazi za chini tu. Si ajabu hata waziri anahusika. Anyways, ni mwendelezo ule ule wa watendaji wa serikali kupiga kwa sababu juu, kuanzia kwa rais nako kumeoza.
Yaani ni utaratibum WA kawaida aisee....
Wanaooagiza mizigo waje hapa jamani....
Yaani ni kawaida agent kubeba dhamana ya mzigo ili hali wewe hujulikan kabisa
 
Hivi Mama Bonge wa vitenge walimaluzana vp na TRA!? Maana lile sakata humu hadi Waziri mkuu aliusishwa nae kwenye mavitenge
Mama bonge alikua hakwepi kodi Kwa sababu inalipoka ila alikua anakwepa Kwa sababu Kodi ya vitenge "HAILIPIKI" ni kama ilivyo kodi ya icing sugar 100% ili hali hapa ndani haizalishwi....
Na imewekwa kundi la sukari....
Hii nch Kuna watu wahuni sana Kwa kuwa Kuna viwanda vya kina mo low quality na urafiki iliyojifia kwenye kitenge kodi wameeka asilimia 100..
Yaani unanunua kitenge elfu 12000 kodi 12000....uje uuze Kwa jumla 28000 rejareja 30,000
Hapo Bado mlolongo WA kodi kuanzia la pango
 
Atajua... Na huyo alie shauri aende kwenye midia ndio kampoteza.

Pale unapokuwa na invoice na packing list halali kutoka Kwa supplier ila Kwa wakala wa forodha unapeleka documents tofauti.. Lazima kiumane tu...

Loophole ya mfumo ikukunufaisha mara moja bhas shukuru.. Ila usichukulie ndio utaratibu.
Mkuuu....kama unaingiza mzigo kutoa nje....
Ni nani anaenda kulipa kodi yako tra??
 
Kwa sababu TRA inatetea msimamo wake sitashangaa wachangiaji wengi hapa ni ama wa TRA au wana uhusiano wa karibu na TRA kwa hiyo wana maslahi yanayosigana. Hoja yangu ni kuwa TRA ina wajibu wa ziada wa kulinda sheria na taratibu zake zisitumike kuathiri kusudi la Serikali,pamoja na kuwaelimisha wadau . TRA katika hoja yao inaonekana hilo suala la wafanyabiashara wadogo ambao hawawezi kujaza content haliwahusu hususan kutoa utaratibu unaofaa, madhara ya kutofuata utaratibu na wajibu wa Clearing and Forwarding Agent ambaye ni wakala wa TRA kumwakilisha TR ipasavyo. TRA katika hoja yake hajamgusa mwakilishi wake Clearing and Forwarding Agent inakimbilia kumtuhumu mfanyabiashara ambaye aliihusisha TRA tangu mwanzoni na siyo kwamba TRA imegundua kuwa amekwepa kodi! Watanzania tunatakiwa tujue, hata katika kuchangia, wajibu wa kila Tassisi ni nini? Hili siyo suala la ushabiki. TRA ni taasisi kubwa na inatakiwa iendeshwe na mtu mwenye uelewa mpana. Hili suala lilipelekwa kwake amekaa nalo mpaka sasa linapelekwa kwa Mhe. Rais ndipo anatoa utetezi wake wakati umma unasubiri uamuzi wa Rais! Je, huu ndiyo utaratibu? Sasa TRA inataka Rais amwambie nini Gadi? Huu utaratibu unafanya kazi ya Rais iwe ngumu sana. Sijui kama wengi mnanielewa ninachoandika. Vinginevyo naomba msamaha.
Tra walisema hata hapo juzi Kila mtu alipie mzigo wake mwenyewe ....ukiona kilichotokea hapo k.koo
Hapa kosa la tra....ni moja na ni kubwa sana Toka awali kuruhusu hao agency wabebe dhamana ya mizigo ya wateja...
Wangekomaa tu kwamba Kila mtu alipie mzigo wake mwenyewe....Kwa agent mlipe ela ya usafirishaji tu....
Ndo maana wanasema kwamba jamaa haonekani kwenye mfumo....ni kweli...inaonekana kampuni aliyoitumia kusafirishia....
Na ndo kitu kinaendelea Sasa hivi
 
Waulizeni wafanya biashara wa Kariakoo kama kuna hata mmoja ana karatasi ya importation ya mali walizo nazo dukani. Mizigo yote inasafirishwa na kutolewa na GSM. Siri ndio iko hapa GSM na TRA wakanushe na hii kwani ni ya miaka yote
Sio GSM tu na opo yake a.k.a Simba WA bahari...
Ni makampuni yote kuanzia hao kina gnm....na mapembelo
Wooote ndo wanaotambulika tra..
Watu Wana mizigo mikubwa lakin hawana documents za tra...
Ila swali langu kubwa ni mbona juzi kati tra walivyosema Kila mtu alipie mzigo wake kukawa Kuna maandamano?
Kunani?
 
Hili swala limetufungua wengi...lakin way forward ni ipi...ukizingatia loose cargo ya box 20 kweli ukapangw folen tra....nayo ni kwikwi
 
Back
Top Bottom