Trafiki wawili wakamatwa baada ya kunaswa kwenye video wakipokea Rushwa hadharani

Aliyerecord na kusambaza hajafanya poa, hao jamaa wanapiga sana kazi tena kwenye mazingira magumu sana, jua,mvua zao hao..mpaka unawaonea huruma.
Na hawana sehemu ya nyongeza zaidi ya humo barabarani...watu wanapiga mabilioni kila siku na allowances za kutosha...
Wawaache bana..
 
Ndo marupurupu yao
Hakuna marupurupu wala nini
Ajali haziishi kwa ajili ya watu kama hawa
Dereva hana leseni, matairi mabovu, breaking system hazifanyi kazi
Kila leo watu wanakufa kwa sababu magari hayaangaliwi kwa sababu ya haya majitu yameacha kazi zao na kujifungulia mradi
Naomba msiwatetee hawa kwani wakifanya kazi zao kwa uangalifu hamtaona ndugu zenu wakifa kila leo
Mara Lori limeparamia watu, mara basi limeacha njia yote haya ni kutokuwa waangalifu
 
Hii kesi mfano Hawa askari wakiamua kwenda mahakamani na kujitetea afu wakili wao awe Kibatala hawatoboi kweli?

Wajitete kuwa hatukuwa tunachukua rushwa ila hela za mchezo wale makonda ni watu tunaocheza nao mchezo wa kila siku buku buku

😌
 
Eti wanakamatwa. Huu ni mzaha mkubwa kuwadhihaki watanzania. Wanajifanya kama hili ni jambo geni kabisa kwa matraffic.
 
Wakipokea pesa/rushwa hadharani.

Je, ingekuwa kwa kificho ni sawa wasingekamatwa.

Kosa lao ni kupokea rushwa hadharani, sawa na kufanya ngono hadharani. Ila ndani chumbani inakubalika
 
jf kiboko huo mziki ulianzia humu humu asbh duh!
jf kiboko huo mziki ulianzia humu humu asbh duh!

Huyo Mpiga picha anapaswa ajifiche Sana ili utambulisho wake usijulikane ili kuepuka Kubambikiwa Kesi mbaya na Jeshi la Polisi Kama alivyofanyiwa aliyekuwa Mwandishi wa Habari za uchunguzi wa ITV Bw. Jerry Muro baada ya kuwapiga picha Askari Polisi wa Usalama Barabarani kule Bagamoyo wakipokea rushwa. Awe mwangalifu Sana huyo Mpiga picha.
 
Suluhisho ni kuweka body cam basi sio muwatie vishawishi watoto wa masikini waombe kidogo kitu alafu muwatimue
 
sasa hii ndio picha halisi ya polisi wa nchi hii. though hao wanawake wa kuwaonea huruma, kwa sababu hadi kupata iyo shift ya kupokea izo hela, kuna garama kubwa sana ametoa pia.
 
na hata hao unaambiwa wamefukuzwa hawawezi kufukuzwa,watahamishwa vituo na vitengo tu. nani asiyeijua hii nchi? though mafisadi wanakula mabilioni, .
 
Dah,mshawaharibia kazi hao watu, trafic wakisema wafuate sheria ipasavyo hakuna gari itatembea barabarani ila chache tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…