Treni ya kwanza ya abiria kutoka Dar es Salaam yawasili Moshi ikiwa na abiria 294, ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM

Mabehewa 20 × abiria 80 = abiria 1600
Capacity 1600 - waliosafiri 294 = loss (1306 × nauli per person)

Tusikate tamaa tutangulize uzalendo tusafiri kwa reli yetu hata kama ni narrow gauge
These numbers are so scaring! I hope TRC watafanyia kazi (wanajua wanachofanya!). Tuwape muda.

Muhimu tu tufike mahali tuache kuchanganya kanuni za biashara na siasa.
 

Kwani kila kitu ni utekelezaji wa ilani? Haya kesho kukicha andika kwamba jumapili ya leo kumekucha ikiwa ni utekelezaji wa ilani. Mbona hii ni too much, kwani haya si yanafanyika kwa fedha za wananchi, mbona mnayafanyahaya kama ni fadhira vile. Huu nao ni upunguani
 
Usisahau ni narrow gauge rail (reli nyembamba), haiwezi kwenda kwa kasi, mpaka reli iwe pana na axel za mabehewa yote yabadilishwe na mengi mengine.

Hata kwa sasa mabasi yanachukua zaidi ya masaa 10
Sio kweli apo kwenye mabasi unadanganya..
 
Kula "like" mkuu
 
Unasafiri Siku 2 kutoka Dar hadi Moshi, safari ya Masaa 8???🤣🤣
 
Vipi kuhusu Dar-Dodoma-Tabora-Isaka ambao reli yao imeboreshwa sambamba na hii ya Dar-Moshi,
Wachague upande gani?
 
This is good news, haya ndio maendeleo ya huduma tunayoyazungumza.
P
Mkuu naomba elimu kidogo!
Hivi CCM ndiyo inatekeleza Ilani au Serikali inatekeleza majukumu yake?
Je,unaweza kutekeleza Ilani bila kua na fedha?
Je ,CCM inavyanzo vipi vya kupata pesa ya kutekeleza ayo tunayo ambiwa?
Mwisho,uoni kua huu ni ulaghai,uongo na uhuni kutumia pesa za watanzania alafu mwisho kujinadi kua unatekeleza Ilani ya chama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…