Treni ya kwanza ya abiria kutoka Dar es Salaam yawasili Moshi ikiwa na abiria 294, ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM

Treni ya kwanza ya abiria kutoka Dar es Salaam yawasili Moshi ikiwa na abiria 294, ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM

Sijuhi ni kwa nini napata hisia kuwa hii treni muda si mrefu itasababisha janga la kitaifa!!
Sijuhi tu yaani!!
Mkuu JP Omuga, sisi watu wa precognition, premonition, na de javu, hatudharau kabisa taarifa kama hizi, please tembelea bandiko hili

Kama wewe ni mmoja wa watu hawa, hii taarifa yako tumpelekee Masanja Kadogosa aifanyie kazi. Mv Bukoba; kuna watu walipata hisia kama hizi, wakazisema, wakapuuzwa, hivyo hawakupanda MV Bukoba, lilipotokea la kutokea, wakakumbusha.

Hivyo taarifa yako hii ni muhimu sana.
CC. Jp Omuga
P
 
Treni ya kwanza ya abiria kutoka Dsm imewasili mjini Moshi saa 5 asubuhi na kupokelewa na maelfu ya wakazi wa Moshi.

Treni hiyo imewasili ikiwa na abiria 294 ambao wameipongeza serikali kwa kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM baada ya usafiri huo kusimama kwa takribani miaka 21. Pia abiria wamesema usafiri wa treni ni wa uhakika na hakuna mambo ya kuchimba dawa au kula magengeni kama ilivyo kwenye mabasi.

Baadhi ya abiria wameomba kwa kipindi hiki cha sikukuu wawekewe miti ya Krismas na zile taa zake kwenye kila behewa.

Source ITV habari!
Kumbe usafiri ulikuwepo wakausimamisha kwa miaka 21 iliyopita. Ni nani aliye usimamisha, na kwa nini ulisimama adi leo hii ndio ccm ije iweke kwenye ilani ya uchaguzi na kuitekeleza?
 
Treni iliyochukua watu 294 ina mabehewa mangapi?

Kwa nini watu ni wachache hivyo?

Kwa idadi hii, hii safari ya kwanza tunaweza kusema treni imejiendesha kibiashara?

Kuulikuwa na promotion gani kujulisha wananchi kuhusu treni hii?

Ushindani kati ya train na mabasi ukoje?

Tofauti ya basi na treni itakayomfanya mtu apande treni ni ipi?

Nauli ya basi na ya treni zina tofauti gani?

Muda wa safari kati ya basi na treni una tofauti gani?
 
Treni ya kwanza ya abiria kutoka Dsm imewasili mjini Moshi saa 5 asubuhi na kupokelewa na maelfu ya wakazi wa Moshi.

Treni hiyo imewasili ikiwa na abiria 294 ambao wameipongeza serikali kwa kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM baada ya usafiri huo kusimama kwa takribani miaka 21. Pia abiria wamesema usafiri wa treni ni wa uhakika na hakuna mambo ya kuchimba dawa au kula magengeni kama ilivyo kwenye mabasi.

Baadhi ya abiria wameomba kwa kipindi hiki cha sikukuu wawekewe miti ya Krismas na zile taa zake kwenye kila behewa.

Source ITV habari!
Abiria 294 kwa usafiri wa treni naona kama ni kidogo hasa ukizingatia umbali kwa maana ya km. Sijajua nauli ni kiasi gani lakini naona kama vile shirika litajiendesha kwa hasara. Huu ni msimu wa sikukuu kwa wenye imani hiyo na bado abiria ni 294, je pale msimu wa sikukuu utakapoisha watakuwepo abiria wakutosha ili shirika liweze kujiendesha kwa faida?
 
Treni hii huwa inaanza safari saa ngapi?

Inachukua muda gani kutoka DSM mpaka Moshi?

Gharama ikoje?

Mizigo ninaweza kuibebesha mwisho kg ngapi?

Msaada pls.
 
[emoji16][emoji16]imetumia 19hrs haina tofauti na treni ya 1945 kweli awamu hii imejaa vilaza
Inawezekana ila usije jikuta umekuwa kilaza wewe? Kwanza jiulize swali moja la msingi? Reli hiyo iliyotumika kupitisha treni hii ilijengwa mwaka gani? Hata google utapata jibu. Halafu kinachoongoza au kupanga mwendo wa treni ni reli,na si ukubwa wa injini pata hayo majibu halafu tujadili haya masaa 19.
 
Nliwahi kusikia mlevi mmoja anasema kaskazini tumebaguliwa katika awamu ya tano
 
This is good news, haya ndio maendeleo ya huduma tunayoyazungumza.
P
Mind you the distance from dar to moshi is a mere 541km, and that distance can be covered in less than 3 hours using mordern trains, this one took a whole 19HOURS. How is that development sir?????? siulizi kwa ubaya lakini, lets try and be critical thinkers pls, sio kusangilia na kuiba nyimbo za sifa wa wanakijani 😅 😛😛😛😛😛
 
Sasa toka dar mpaka moshi ni umbali wa 541km, kwa treni za kisasa hio safari inastahili kuchukua chini ya masaa 3 pekee, treni za kisasa nyingi zinafanya 240km per hour, sasa kaa hii treni ilichukua masaa 19 toka dar mpaka moshi, nini wabongo tunapiga makofi na kushangilia, hii inaoyesha vile uelewa wetu wengi hapo bongo ni mdogo kabisa, ni kaa hatujui yanajiri nje ya mipaka ya taifa letu, aina hizi za treni zinazokweda pole pole kaa hii ziko katika museum katika mataifa mengine, hapo ndipo watu huenda kuzitazama na kufundiswa historia ya vile reli za karne iliyopita zilikuwa zinafanana na vile zilikuwa ninaenda pole pole,masaa 19 umbari wa 541km!!!!!!!!!!!!!
 
Biashara ya train aiwezi kuwa na hasara ata siku moja kutokana na uhalisia wa mfuko wa mTanzania.

Tatizo ni upkeep maana hawa jamaa kama UDART ambayo kwa sasa ilitakiwa kuwa na double the capacity ya mabasi kutokana na demand wao ndio kwanza yamepungua na waliyoanza nayo mtu unabaki unajiuliza how is that even possible.

Train kama dalala tu watu wana panda na kushuka kila kituo sio watu wanaoanza safari wanafika mwisho na sio wote wanaoshuka mwisho walianza safari kituo cha mwanzo.

Hila kwa hawa waendesha biashara za serikari sitoshangaa kusikia mtu kachomoa mataluma huko sijui wapi na wao hawana stock ya karibu kufanya repair matokeo yake route ikasimama week nzima au maintance ya train zao ikawa shida, something is bound to happen I don’t what yet hila sababu ukija zisikia chanzo chake ni uzembe au poor operation planning na hiyo biashara kutokuwa reliable hapo ndio tatizo lilipo.
 
Mimi naona hii treni itasaidia zaidi mizigo hasa kilimo kutoka Arusha, Manyara na cement kutoka Tanga lakini masaa 19 bado ni mengi sana kwa safari.
 
Moja kati ya faida ya upinzani...kama upinzani ingekua haujakomaa Arusha na Moshi hii reli isingelifufuliwa.
Serikali ya ccm inaumiza kichwa wafanye nn ili wapiga kura wabadilishe mwelekeo kwenye chaguzi zijazo..Mwisho wa siku watu wanapata maendeleo.

Action and Reaction are equal and opposite.

NOTE; MOSHI NA ARUSHA ENDELEENI KUCHAGUA UPINZANI MUPATE MAENDELEO.
Kule CCM mpaka waibe au wapinzani wagome watu wa kule hawategemei serikali. Serikali iache pesa kule hata nusu tu ya watalii uone kutakuwaje kule. Pesa za watalii zinaingia Tanapa haziesabiwi kama mapata ya kule

wananchi wanaotegemea sana serikali ndiyo wanakuwa masikini zaidi. Mafanikio ya sehemu ni utamaduni hebu jiulize kwanini wenyewe wana lami vijijini? Wengi wamechanga kujenga barabara zao wenyewe wakati wa mwinyi
 
Tehe tehe,pinga pinga hamkosi la kusema
Treni ipo fully booked mpaka 31 dec
Hakuna mchagga atakusikiliza wewe wakati anafika moshi kwa 15,000
Waendao moshi miezi ya december ilikua ni kilio na kusaga meno,hayo masaa ulioyataja ndio walikua wanayatumia kulala ubungo kusubiri basi lije halafu nauli ilikua 90,000
Tumuogope MWENYEZIMUNGU
 
Back
Top Bottom