Treni ya kwanza ya mizigo yafika Arusha baada ya miaka 30

Treni ya kwanza ya mizigo yafika Arusha baada ya miaka 30

Kali _D

Senior Member
Joined
Feb 10, 2019
Posts
145
Reaction score
132
DC Arumeru Leo Tarehe 13/08/2020 Majira ya saa mbili kasoro asubuhi tumepokea Gari Moshi (train) ya majaribio ya kwanza ya mizigo baada ya miaka 30 ya kukosa huduma hii ya usafirishaji katika mkoa wetu wa Arusha. #ArumeruYetu

1597304088062.png

1597304132201.png
 
DC Arumeru Leo Tarehe 13/08/2020 Majira ya saa mbili kasoro asubuhi tumepokea Gari Moshi (train) ya majaribio ya kwanza ya mizigo baada ya miaka 30 ya kukosa huduma hii ya usafirishaji katika mkoa wetu wa Arusha. #ArumeruYetu
Kama imechukua miaka 30 serikali ya ccm kupeleka treni arusha je itachukua miaka mingapi serikali ya CCM kuivusha Tanzania kutoka kwenye lindi la umaskini?

Lissu ni chaguo pekee!
 
Najiuliza wakoloni ambao walijenga reli 1900 ikaingia Arusha kwanini tuliwatoa kama leo tunashangilia treni kuingia Arusha baada ya miaka 60 ya uhuru?
Kuwatoa was a must,ilikuwa ni lazima tujitawale,tatizo waliingia walaji wakala mpaka wakaua kila kitu,lakini tokea amaeingia JPM kila kitu sasa kimerudi kwenye mstari,sasa hapa utachagua mwenyewe kura yako umpe nani mwezi October...
 
Kuwatoa was a must ilikuwa ni lazima tujitawale,tatizo waliingia walaji wakala mpaka wakaua kila kitu,lakini tokea amaeingia JPM kila kitu sasa kimerudi kwenye mstari,sasa hapa utachagua mwenyewe kura yako umpe nani mwezi October...
Kama Lisu na Membe hatagombea hata kwenda kupinga kura sitahangaika, siwezi kwenda kuchagua maisha magumu hiyo laana siitaki kabisa
 
Faida yote ya reli waliipeleka Kwao pesa haikubaki nchini

Utetezi dhaifu. Muda hao wajerumani waliojenga hiyo reli na kuitumia, ni mfupi kuliko muda tuliokaa nao sisi hiyo reli. Kama ni faida, sisi ndio tulipaswa kufaidika zaidi na hiyo reli kuliko wao.

Mkoloni wa mwisho ambaye ni muingereza anaondoka hapa nchini, hiyo reli ilikuwa ni katika hali nzuri sana, hivyo ccm mlichemsha wenyewe.
 
Kuwatoa was a must ilikuwa ni lazima tujitawale,tatizo waliingia walaji wakala mpaka wakaua kila kitu,lakini tokea amaeingia JPM kila kitu sasa kimerudi kwenye mstari,sasa hapa utachagua mwenyewe kura yako umpe nani mwezi October...

Kwa hiyo lengo la hiyo reli ni ili mpate kura? Hakuna mtu mwenye shida ya usafiri huko Arusha.

Ukitaka kujua watu hawababaiki na hiyo treni, kaangalie waliokwenda kuilaki hiyo treni, na watakampokea Lisu kesho.
 
...siku izi treni la DSM-Moshi silisikii likishadadiwa sanaanaa.. safari zake bado zipoo?

Zipo japo zilisimama kwa ajili ya mvua iliyopelekea baadhi ya vipande vya reli kubomoka. Tatizo la hiyo treni ni muda, na ukitazama muda wa basi ni mfupi zaidi kuliko wa treni. Hivyo ni vigumu kwa mtu anayefanya kazi kwa muda kupakia hiyo treni. Labda kwa mizigo, lakini sijafanya utafiti wa kutosha kuhusu ufanisi wake vya kutosha, na huwezi kutegemea taarifa vya ufanisi kutokana serikalini, kwani mazingira ya kudanganywa huko ni makubwa sana.
 
Back
Top Bottom