Trilioni 1.5 Bwawa la Nyerere limepotelea wapi

Trilioni 1.5 Bwawa la Nyerere limepotelea wapi

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushuhudia uzinduzi wa zoezi la kuingiza maji kwenye Bwawa la Julius Nyerere Disemba 22, 2022 badala ya Novemba 2021 iliyokuwa awali.

Mheshimiwa Rais pamoja na hatua hiyo muhimu bado kuna mambo ya msingi sana ambayo Waziri wako wa Umeme hajayaweka wazi yakiwemo madai ya shilingi Trilioni 1.5 alizotakiwa kulipa mkandarasi Kampuni ya Arab Contractors kama faini ya uchelewesha mradi miaka 2 hadi 2024 badala ya Juni 2022 iliyokuwepo kwenye mkataba.

Fedha hizo zinatakiwa zilipwe kwa Serikali ili zisaidie shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi, sasa muulize hizo fedha amelipwa nani na hayo madai watanzania wote wanayafuatilia kwa karibu sana tofauti na anavyofikiria kwa sababu huo mradi sio wa Januari na Baba yake Watu Wazuri Hawafi kina Kinana na JK huo ni mradi wa watanzania wote milioni 61.

1671374108156.jpeg
 
Makamba bado anazidi kumwingiza mama kwenye chaka....
Wananchi wanahitaji umeme Tu hizo sinema za kujaza maji ni utoto Tu
Waziri Makamba amesema >> 'Tunategemea itachukua misimu miwili ya mvua kulijaza bwawa na kuanza kujaribu mitambo' - Makamba.

Bwawa la Mwalimu Nyerere linahifadhi lita 33.2 bilioni za maji na kama zikitumika na mitambo yote, itaweza kuendesha mitambo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
 
Wiki ya kesho ya desemba 22, 2022, Rais dkt. Samia Suruhu Hassan anatarajiwa kubonyeza kitufe maalum ambacho kitashusha geti la kuziba handaki lililokuwa limechepindisha maji katika mradi wa kufua umeme wa bwawa la Julius Nyerere (JNHPP).

Kuanzia hapo sasa inakuwa ni rasmi maji yataanza kujaa kwenye bwawa hilo na soon JPM (hayupo) ila anakuwa kafanikisha adhima ya Tanzania bila giza inawezekana.

Taarifa hii imetolewa leo na msiyempenda ambaye ni waziri wa wizara ya Nishati January Makamba.

 
ujazaji maji Bwawa la Nyerere wageni 2,300 kudhudhuria. Mbona gharama za ugeni huu ninaona ni kubwa sana?

Au bwawa hili limejengwa mjini ili watu wahudhurie wengi kiasi hicho?

Nimeuliza tu kwa sababu kuna matukio siku hizi watu wanatumia kupigia kodi za wananchi.
 
Back
Top Bottom