...48
Nijibu basi, yule msichana alikuwa hapa muda si mrefu, sivyo? Alinikazia yunge,
Ebu leta hayo maziwa kwanza, mie ninanjaa,
Nilimpotezea,
Shauri yako, nilikuonya jana ila leo tu umeshaharibu, hao paka na bundi ni maarufu sana hapa kijijini, wale ni walinzi wa yule msichana, na wanafahamu kila kitu juu yetu mimi na wewe, sasa wameshajua kwamba unataka kumchezea mtoto wao na ndio sababu walikuwa wanakuangalia kwa hasira, bahati yako babu naona amekuwekea kinga, vinginevyo...!
Nyiee mbona mmejifungia ndani jua kali hivi? Kuna nini humo? Ilikuwa ni sauti ya bibi akiuliza.
Sihuyu mme wako nimemkuta amejilaza ndani muda huu, hata mimi namshangaa!
Alisema yunge,
Tulitoka ndani na kumsalimia bibi, kisha yunge alipeleka sufuria la viazi na birika la maziwa pale kivulini, tulikaa pale mimi na yunge huku bibi akiingia ndani.
Usiwaambie babu na bibi, hilo jambo dogo ntalimaliza mwenyewe, ila sasa umeanza kuamini niliyokuambia juu ya yunge,
Naomba uachane nae kabisa utapotea sawa mchumba..!
Nyie ndo mnakula sasa?