Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Poa poa mkuuNikisema kila jambo nita-disclose information[emoji1]
SawaUkiEndelea ndugu naomba unitag, hv viumbe ni washenzi sana Kuna Rafiki yangu Alisha wahi weke dawa na kimada akatelekeza Familia na wazazi wake walipo enda kuongea nae arudi kulea Familia yake aliwatolea bastola na kuwafukuza kama mbwa ila yaliisha a karudi kwa mkewe na alilia kama mtoto kuwa omba msamaha wazee wake isingekuwa mkewe kuwa mvumilivu jamaa angeua kale kamada na yy kujiua
Hilo halikuwa tatizoHutaki kua CEREMONIAL FATHER?Kabudi anaitaga SOCIAL FATHER
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji119][emoji119][emoji119]Namtaleta Sana story zenu..mzee mwitore kawafungua akili [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ni mwepesi mnooo [emoji16][emoji16][emoji16]Mzee wa kuwajulisha nyumbani [emoji3][emoji3]
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119] aiseeSEHEMU YA 3:
Kipindi hiki cha ujauzito wake ndio nilipitia wakati mgumu zaidi, mambo mengi sana yaliendelea yaliyonivuruga sana, bidada alibadilika mno
Wakati mwingine najipa moyo huenda mimba yake tu inasumbua, au nafikiri mimba inanichukia lakini wakati mwingine nahisi noo hapana hata kama mimba inanichukia sio kwa kiwango hicho.
Simu zikawa hazipokelewi tena, zikipokelewa haongei, akiongea ananifokea(Nakumbuka Banana Zorro ameandika haya kwenye wimbo mmoja sikumbuki jina lake, basi nilikuwa nikiusikia huu wimbo naumia sana ni kama aliniandikia mimi)
Kilichokuwa kinaniumiza pamoja na mapenzi yangu kwake lakini nilikuwa najitahidi kuokoa penzi kukwepa aibu, kwanza penzi lisife sababu ntaonekanaje mbele za watu, pili sikutaka maishani mwangu kuwa na rekodi ya kuwahi kuvunja ndoa tatu isije kuwa tu nimepigiwa mimba maana ni aibu sana
Maisha yakawa yanakwenda kwa mtindo huo wa mimi ndio nipige simu nisipopiga siongei nae na nikipiga ndio lolote linaweza kutokea kati ya yale matatu, nikawa sielewi kabisa kinachoendelea, wakati mwingine napiga simu anapokea work mate mwenzie anasema "BM anasema usimsumbue" dah basi mimi huku nikikata simu nachanganyikiwa kabisa kabisa.
Halafu ushirikishwaji ukawa haupo kabisa, siku za kujifungua zinakaribia lakini hakuna kinachopangwa wala chochote juu ya maandalizi ya kujifungua kuna siku nikampigia nikamuuliza kwa unyoonge bibie mbona mambo sio mambo hivi mimba yangu kweli hiyo? Akanijibu kitanda hakizai haramu[emoji2307][emoji2307][emoji2307]mpaka kesho najiuliza alidhamiria au ndio hasira za ujauzito?
Kwamba mimba sio yangu ama? Sasa mbona kadi ya kliniki kaandika jina langu? Au kaandika kwa kuwa yuko ndoani na mimi? Maswali yalikuwa mengi mnoo!!
Kuna wakati nikampigia simu akakata ikafuata meseji nzito ikiniambia "kwani hicho ki*** hakitulii? Kama unataka tafuta mwanamke mwingine oa achana na mimi" Dah nikawaza sana mimba ndio zinakuwa hivi? Mimba ikikuchukia ndio inakuwa hivi? Mimba na kuachana vinahusianaje?
Hii meseji alikuja kuikataa katakata na hapo nikawaza jambo jingine kwamba huenda hakuandika yeye? Kwahiyo aliandika nani? Lazima ni mtu ambaye hakutaka niendelee na BM. Mwanamke? Hapana haiwezekani lazima ni mwanaume
Hayo ndio yanakuja kunipa mashaka baadae.
Kitu kingine suala la hela ya matumizi sasa, alikuwa anademand pesa nyingi sana na mimi kwa ulimbukeni sijui nilitengenezwa nikawa natuma tu
Miaka hiyo Laki ilikuwa ina heshima kidogo, sasa akawa anaitaka kila mwisho wa mwezi huku ana kazi yake
Alinipunyua sana hela mpaka nikamlalamikia mama yangu akasema asikubabaishe huyo kwani mimba inakula sh ngapi? Kwa kawaida gharama zinakuwepo kama mimba inamsumbua kama haimsumbui unachotakiwa kufanya ni kujiandaa kwa ajili ya kujifungua..
Kuna siku moja akaomba hela tu ghafla eti akatembee sabasaba nikatuma vipesa kidogo akavirudisha[emoji23][emoji23][emoji23]mimi nikachanganyikiwa kabisa kwa nilivyobadilikiwa, huyu hakuwa BM wangu
Niseme wazi bidada alinimalizia visenti mpaka wakati anajifungua sikuwa na akiba ya maana sana kumfanya ajifungue bila shida, bahati nzuri yeye pia ana kazi na pengine kuna baba mwingine wa mtoto alisaidia kugharamia maana sikusumbuliwa sana.
Kwahiyo kulikuwa kunaendelea vitu ambavyo vilikuwa vinaniacha njia panda
Kuna mambo yanatokea unaona kabisa mimba sio yangu, kuna mengine yanatokea unaona mimba ni yangu ila amenichukia sababu alipofika huko alipata wanaume wengine hivyo hakutaka mimba yangu, ni kitu ambacho hakukitarajia
Mfano kuna siku nilimlalamikia mabadiliko yake akasema kama vipi niachane nae au nafikiri nimemkomoa? Sasa mimi huku hata sielewi hayo yametoka wapi
Nilitafsiri kwamba hata kama nimempa mimba bado mambo yake yataenda tu inaonekana mimba ilimharibia mahali alipotaka yeye ndio aolewe kwa sasa
Kwahiyo suala la kuandikwa majina yangu(jambo ambalo sio zito jina linaandikwa tu)
Suala la siku aliyopata mimba(huwa nahisi alikuja siku za hatari)
Na hili kwamba nahisi namkomoa
Haya tu ndio yanafanya nihisi mimba ni yangu, mengine mengi yafuatayo ni wazi mimba haikuwa yangu[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Siku zilisonga, alipokaribia kujifungua akanitaka nikamchukue, nikaenda, nilikaa nae wiki moja kabla sijamchukua, ile wiki niliishi kwa shida sana, kejeli, dhihaka na mengine, yalinichanganya sana
Nikamchukua nikampeleka kwa dada yake ambaye tuko nae mkoa mmoja ambako ndio alipendelea akajifungulie
TUMEMALIZA KIPINDI CHA UCHUMBA, TUMEMALIZA KIPINDI CHA UJAUZITO, TUTAMALIZIA BAADA YA KUJIFUNGUA
NIMEAMUA KUMKATAA MTOTO RASMI
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]kaambiwa kitanda hakizai haramu .... Bm anasema usimsumbue [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] na yeye bado tu Yupo na Huyo mtu duuhh hii Ni level ya mwisho kabisa ya uzwazwahivi mimi ndo nna tatizo ama ww na wenzio, unawezaje kusumbuka namna iyo kwa kujifariji eti ni mimba tu imenikataa.
Indeed [emoji16]Popoma
Tuendelee mkuu achana na rikiboyKuandika sio kazi rahisi, halafu sifanyi biashara wala siombi ushauri, Mimi naweka kumbukumbu hapa
Tuko pamoja endelea kuleta uzi weekend Leo tunafunga mafile tu hamna kaziSEHEMU YA 6:
Wakati tukiendelea kuweka kumbukumbu lazima kuna kitu mfuatiliaji aki-note, kwamba huyu bidada yeye hanaga shida na mimi wakati wote, nikikaa kimya nae anakaa kimya jambo ambalo sio rahisi kwa wazazi, kuna mambo hupelekea kuwasiliana, ukizingatia mtoto anaishi naye yeye kwahiyo kuna kuumwa, kuna mipango mbalimbali juu ya mtoto na kuna kumuunganisha mtoto na baba, kwa maana kwamba labda kupiga simu niongee na mtoto au asikie sauti yangu
Au nikipiga basi ampasie niongee nae, hayo yametokea mara chache san. Hakukuwa na sababu ya kunitenganisha na mtoto ikiwa sijawahi kuwa na ugomvi nae juu yake, hata yeye mwanamke hakuna ugomvi hasa tumewahi kuingia kiasi cha kupelekea umbali wa mtoto na mimi.
Kwahiyo naweza kususa nikakaa hata miaka nae akatulia tu, ni mara moja tu amewahi kunianza, wakati alipotaka turudiane.
Basi bwana tuendelee na soga letu lilipoishia, siku aliyoomba msamaha akaondoka akijua yameisha, nakumbuka nilimpa tu kihela fulani kidogo kumsaidia nauli maana alikuja kwa kushtukiza na sikuwa na kitu, nacho nilimpa tu sababu ya mtoto sio sababu yake, najua alijiandaa na safari. Siku zote pamoja na kuona kuna vitu haviko sawa sikupunguza love kwa mtoto.
Alipoondoka akafika mkoani kwake ananitumia vimeseji sijui mbona sijamtakia safari njema au mbona sijampigia kuuliza kama amefika, mi nikala bati tu
Hayakuwa mambo ya kuisha kirahisi namna hiyo na mimi nilishaingia kwenye mahusiano mapya, as i said before nikishakuwa na mtu tayari basi ni huyo huyo huwa siyumbi wala kurudi nyuma
Mungu fundi bwana, mwanamke niliyekuwa nae kwenye mahusiano wakafahamiana, kuna mazingira yalipelekea wakafahamiana akili yangu ikanituma huyu ananirudia ili aharibu tu mahusiano ya sasa kimsingi hanipendi nikimrudia nitafurahi na show.
Nikabaki na msimamo wangu.
Akaendelea kuwa karibu akaona sielekei kibra akaamua kupotezea kama kawaida yake.
Lakini hiyo hali bado ikawa hainifurahishi mimi,
Kwanza katika maisha yangu niwe hai au nimekufa sikupenda kuwa na rekodi ya kukataa mtoto, maana huku mtaani watu wasioelewa nilisikia chini chini wakidhani nimemkataa mtoto,
Pili, haikuwa busara tofauti zetu wawili zimuathiri mtoto, kutengana kwetu ilitosha kabisa kuwa adhabu kwa mtoto tusimuongezee mengine tusingekuwa tunamtendea haki kabisa.
Yaani awe wangu asiwe wangu sikutaka aishi kwa upweke wa kutomjua baba ni bora hata ningekuwepo kivuli ili hata akijua ukubwani haitamuathiri kisaikolojia atakuwa ameshapita stage muhimu zilizohitaji masikio yake kusikia Baba/Mama.
Kitu tu pekee sikuwa nafanya kwa ajili yacho ni kwamba eti nikimkataa kuna siku atakuwa mtu gani sijui atashindwa kunisaidia. Mimi imani yangu ni kwamba mzazi anatakiwa kumsaidia mtoto sio mtoto amsaidie mzazi kwahiyo hata awe rais na asinisaidie hayo ni juu yake, sipangi kuwa fukara.
Ni umasikini ndio unafanya watua waogope eti ukimkataa utakuja kukwama.
Sasa mimi nimeamua kumkataa awe wangu asiwe wangu alaumiane na mama yake.
Wakuu wakumbuke kwamba tangu mtoto akiwa na mwaka mmoja hajakaa sio na baba tu bali hata mama yake, mwanzo alisingizia kwenda kujiendeleza kielimu lakini hata baada ya kumaliza bado mtoto aliendelea kubaki kwa bibi. Nikawa najiuliza ni kwamba huyu sio mama bora au kuna kitu anamkimbiza mtoto huko?
Nalo lilikuwa linaniudhi sana kila wakati tunapokuwa tuko poa nilijaribu kumsisitiza akae na mtoto haiwezekani mtoto akose mapenzi ya baba akose na ya mama pia halafu wazazi wote wawili wapo zao tu town wanadunda tena vijana kabisa.
Yeye udhaifu wake ni mmoja tu ambao pia unaniongezea mashaka juu ya ubaba wa mtoto huyo, ukiacha lile la kukaa kimya napokaa kimya lakini kuna la maamuzi.
Mwanzo yeye ndio aliita jina la mtoto kibabe tu, yaani yeye ndio aliamua mtoto aitwe nani utafikiri mtoto hana baba au baba mwenyewe sijulikani kwao. Yaani kama tulikutana tu njiani.
Pia hili la mtoto kukaa kwa bibi alinijulisha lakini akiwa ameshaamua, yeye akiamua hata umshauri vipi tayari ana maamuzi yake akanijulisha tu kwamba anapeleka mtoto kwa bibi ili akajiendeleze
Kwa mara nyingine maamuzi yangu juu ya mwanangu yakabaki kama kivuli, baba jina tu msemaji yupo.
Kwahiyo wakati alipoomba msamaha nikagoma alipoamua kukaa kimya maisha mengine yakaendelea, sasa kaumri kangu kalikuwa kanasogea nimeshaishi kibachela kwa kitambo(maana huyu BM sijawahi kuishi naye tulivurugana mwanzo tu wa ndoa) nikaanza michakato ya kuvunja ndoa ya kwanza ili nifunge ya pili.
Mwanamke ninayemuoa nae anamjua, kwanza akaona ni aibu kwake lakini pia ule wivu tu wa asili kwamba ulichokikataa wenzako wanakitafuta. Nafikiri akapanga lazima turudiane au aharibu tu, akaanza kutumia watu wa karibu wanipe somo huku akiwajaza uongo nikagoma.
Akahamia kwa wadogo zangu, wale maselasela akawa anawatumia vocha wanaona yeeess shemeji si ndo huyu, wale wa kike anawatia maneno ati huyu mwanamke wa sasa ndio aliharibu ndoa yake, kwamba ni bora nirudiane nae kwa kuwa tuna mtoto tayari kuliko kuanza upya na mtu mwingine, mara tulishafanya mambo ya kimaendeleoa sijui tuna kiwanja wapi na wapi sijui wakati si kweli.
Wanawake ni rahisi kumuelewa mwanamke mwenzao wakanivagaa, nikawatia mkwara wakaniacha.
Kwa upande wa wazazi akashindwa maana ukiacha la kutoa mimba lakini kuna wakati mzee wangu aliwahi kuumwa taabani pamoja na kumjulisha alipiga simu tu mara moja kwa kumlazimisha asije akaonekana vibayaa hakurudia tena
Kwahiyo kwa wazazi alishajijengea picha mbaya.
Nikaenda baraza la kata, akaitwa kwa simu ili kuchelewesha mambo akataja tarehe ya mbali ili kukwamisha mchongo, tarehe ilivyofika alikuja likizo kimya kimya siku namkumbusha kesho yake ndo anaondoka hakusema kama anaondoka akasema tu atakuja barazani, kesho akapanda zake basi akayeya(Angejua baraza halivunji ndoa linasuluhisha tu pengine angekuja tungeyamaliza, napo ni kama ningechemka hoja zote za kumuacha)
Alipoondoka mwanaume nikaliambia baraza lichukue hatua.
Baraza likaipeleka mahakamani(mahakama ya mwanzo), kule akalimwa wito/ summmons ya kimahakama. Akaahidi atakuja.
Hapo akaona mambo yamekuwa ya moto akanipigia kunichimba mkwara eti naongea na mwanasheria wangu juu ya hili[emoji23]kwanza najua hawezi kuwa na mwanasheria pili kama alitafuta mwanasheria inawezekana wanasheria wana zile "Sema ukweli wote tujue tunatoboaje" kama madaktari tu ili utibike kirahisi sema ukweli nilipita kavu mahali fulani sasa naona ute ute(joking)
Inavyoonekana mwanasheria alipopewa ukweli akamwambia tu ukweli kwamba hatoboi.
Akahamia kwa ndugu zake, siku moja nimekaa naona namba mpya, jamaa ananipigia anasema ni mjomba wake(kwa muda mfupi niliodumu kwa amani naye kuna ndugu sikuwafahamu) kumuuliza shida yake anasema anaomba tukutane tuyazungumze haya, nikamwambia imeshafika mahakamani tutazungumza huko, akarudishiwa jibu lake.
Pumbavu sana hao wakati napambania penzi langu niliwashtakia sana wakanitosa leo wanaibukia hata nisiowafahamu
Kwa upande wa yule shangazi inawezekana alitosa kuingilia maana walitakiwa kuyaweka sawa wakati nawalalamikia sasa yamefika pabaya wataingiaje.
Alichofanya hakuja, sio kwa kukaa kimya ila kwa kutafuta visababu.
Akasema anakuja nimtumie nauli nikataka kugoma mahakama ikanishauri nimtumie asije kuifanya kama sababu, nikawa tayari kumtumia. Nikamuelekeza njia ambayo akiitumia atatumia nauli ndogo akagoma anasema huko barabara mbaya anataka azungukie mbali apite Dar sijui
Wasichokijua wafuatiliaji kuhusu BM ni mpenda pesa, ndio maana huwa nahisi mtoto sio wangu ila ananipiga hela tu.
Ile kunipangia njia ya kupita na tunajua njia hiyo ilishawekwa lami mwanzo mwisho yeye anasema mbaya nikafura kwa hasira nikaenda mahakamani nikamwambia Hakimu aifute nitajua cha kufanya.
Yule hakimu abarikiwe huko aliko akasema usifanye hivyo atakusumbua baadae, mradi ameshasaini summons sisi tutasikiliza upande mmoja.
Na kweli kwanza mlolongo ukapungua nikasikilizwa mimi talaka ikaandika
Nikaambiwa nisubiri siku 45 za rufaa nifuate hati ya talaka.
Sheffer95
NIMEAMUA KUMKATAA MTOTO RASMI
Ni kweli mzee tatizo lilikuwepo nafikiri ndio lilinitibia tatizo unalozungumziaKuna kitu hakiko sawa na Maisha yako ya Mahusiano ya Kimapenzi, Inabidi Ubadilike haraka sana.
- Umekwisha jua kuwa mtoto sio wako.
- Mwanamke alikuwa na Mwanaume mwingine.
Na baso una entertain mahusiano naye. Ama kweli una stahili maumivu yote uliyo yapata.
View attachment 1700793