Trump amsifia Putin kuwa ni 'Genius' kwa namna alivyoingia Ukraine

Trump amsifia Putin kuwa ni 'Genius' kwa namna alivyoingia Ukraine

Mkuu huyo Clinton ni Bill Clinton na alimsifia Putin mwaka 2014, miaka mingi kabla hata Biden hajawa Rais wa US.

Lakini pia hata George W. Bush alishawahi kumuelezea Putin kuwa ni mtu smart sana (cheki video hii kuanzia sekunde ya 30)

Raisi watatu wa Marekani anasema hivi, halafu bado kuna watu wanakomaa.
 
Wewe shida yako ni vita itokee., lakini wenzetu hawako uko uliko wewe Unaambiwa 40% ya gesi ya Russia anauza ulaya sasa niambie ni kwa vipi Russia hataanguka kiuchumi? na kuanzia ile juz alivyovamia sasa ameanza rasmi russia kulipa gharma yake ya uvamizi.
 
Ukweli mchungu ambao wengi wetu hatupendi kuusikia ni kwamba Raisi Vladmir Putin ni moja kati ya binadamu wenye akili mno. Tutabishana sana lakini uhalisia wa kihistoria umetuthibitishia hilo. Nafahamu wengi watasema Urusi inajificha nyuma ya mgongo wa silaha za kinyuklia, lakini mbona Urusi ilikuwa ina nyuklia tokea kipindi cha Chernenko, Gorbachev na Yeltsin. Hii ni hoja rahisi mno kwasababu kuna mataifa mangapi duniani yana silaha za kinyuklia lakini hayafanya kama Urusi ???

Leo nimesikiliza alichokisema Donald Trump kuhusu Vladmir Putin, kwamba "That was a genius move" and "I know him, he's a very savvy guy". Unaweza kumshambulia Donald Trump kwamba anasema haya kwasababu anamchuki Joe Biden, lakini hata Raisi Bill Clinton aliwahi kusema "Putin is smart, really smart". Donald Trump kasema anamfahamu Vladmir Putin baada ya kufanya naye kazi kwa kipindi kifupi kwamba ni mtu ambaye akisema kitu ni lazima akitekeleze.

Hapa siangaliaa suala la kimaadili "A Moral Side" lakini naangalia uwezo binafsi wa mtu. Hate Him or Love Him, Vladmir Putin is a very smart person.

Nuclear na hypesonic missile ndio zinampa jeuri.
Wanacho muogopa Putini wanajua ni mwehu kwamba anaouwezo wa kutumia hizo silaha kama akizidiwa kidogo ndio maana wanamuogopa.

Kingine ni silaha za kutungulia ndege hayo ma s-400 nk.

Kimsingi amejipanga kikamilifu.

Kibabu Bide sio kijinga,kinajua vita ikianza haitakuwa kama zamani sababu moto utawaka mbaka newyork.

Mkuu hypersonic hazitunguliki na kitu chochote ndio mana ukiingia vitani na nchi yenye hypersonic ujue huna namna ya kuzizuia hizo silaha,zisi kutwange.

Sasa babu akiangalia magotofa ya newyork jinsi yanavyo pendeza alafu anajua kabisa akijichanganya yanashushwa jumlisha uzee ndio presha inapanda anaona atakufa bure hahahahaaa.
 
Trump +Clinton wana malengo yao kisiasa kutamka hayo maneno., wanalenga kumdharau Biden ionekane ni advantage kwa uchaguzi wa Marekani utakaokuja, lakini Trump mbona wale North Korea wamekuwa wakivunja makubaliano ya umoja wa mataifa wazi wazi yeye akiwa madarakani ambapo Marekani ndio mdau mkuu , Trump akiwa ni rais kwanini hakuchukua hatua?

Huwezi kuwa Genius kwa vile Russia bado uchumi wake unaoanza kukua ni unategemea nchi nyingi za ulaya pamoja na Marekani ambazo saivi wameshatangaza kumuwekea vikwazo., Biden na Marekani wameona njia ya vikwazo ndio njia pekee ya kumkwamisha Putin kiuchumi ambalo ndio lengo kuu Marekani., Ni vile Putin amepigwa vita ambavyo vitaendelea kumuathiri siku hadi siku na uchumi wake kuporomoka

Kwa mfano ule mradi Norde Stream 2 bomba la gesi litokalo Russia kwenda Germany jana ujerumani wameshazuia kibali cha kuendelea na sanctions nyengine zinafuata. Hii vita ni ya kiuchumi sio ya hivyo vifaru alivyoviona trump na clinton
Unafikiri hata Putin asingepeleka majeshi asingewekewa vikwazo?
Alisema vikwazo lazima wangeweka.
Na vikwazo vinaweza visimuathiri kiviile sababu anaweza fanya biashara na wenzake waliotengwa kama China, Iran, Venezuela, North Korea nk. Na hili ndilo tatizo la kutenga nchi nchi nyingi sababu zitaungana kufanya biashara.
Laiti angefanya assessment akaona vikwazo vitamuumiza asingechukua uamuzi huo..
Halafu kwani kabla ya hivi vikwazo hakuwahi wekewa vikwazo hapo kabla?
 
Wewe shida yako ni vita itokee., lakini wenzetu hawako uko uliko wewe Unaambiwa 40% ya gesi ya Russia anauza ulaya sasa niambie ni kwa vipi Russia hataanguka kiuchumi? na kuanzia ile juz alivyovamia sasa ameanza rasmi russia kulipa gharma yake ya uvamizi.
Itoshe tu kauli ya Rais George W. Bush kuwa Putin is a very smart 'tactician', aggressive person.

Kwa mujibu wa online dictionary, tactician is a person who uses a carefully planned strategy to achieve a specific end.

Sasa hivi Putin ambaye ni 'very smart tactician' wadhani hajui matokeo ya kile alichokipanga ikiwemo hivyo vikwazo vinavyowekwa? Na namna ya kuendana navyo?

SmartSelect_20220223-153548_Chrome.jpg
 
Mkuu kati ya wewe na marais wawili wa US kwa pamoja, Trump+Clinton, tuchukue maneno ya nani? Hao marais wote wawili wanasema Putin ni smart a.k.a. genius

Wakati mwingine usisubiri mtu akuambie sasa tumia akili, soma alichokisema Trump afu jiulize alikuwa na maana gani.
 
Ni kisiasa zaidi Marekani ya sasa narudia tena na tena vita ya kukandamiza kiuchumi wao wameona ndio njia pekee endelevu itakayowasulubu kina Putini, uzuri wa Putini kisilaha haimaanishi kwamba Marekani hawezi kumshughulikia Russia chini ya dakika 5 kama Marekani itaamua.
Dk tano.
 
Kwa wasiofahamu tu ni kwamba, hivi vikwazo vya kiuchumi alivyolimwa Russia madhara yake kwa uhakika zaidi yataanza kuonekana kwenye miaka 2-3 ijayo na hivi vikwazo vyenyewe naona ni very calculated and punitive.

Kwa vyovyote vile endapo Russia ataendelea kukomaa na uvamizi wake ukweli ni kwamba wapende wasipende kamwe hawataweza kuhimili madhara ya hivyo vikwazo na lazima watakuja waombe tu poo.

Kama kuna mtu atabisha hili basi ni kwa kutokufahamu tu uzito wa vikwazo hivyo anavyowekewa Russia kwa sasa na athari zake kwa uchumi wa taifa hilo.

Madhara watakayopata kutokana na athari za vikwazo hivyo ni afadhali ya hasara watakayopata kutokana na Ukraine kujiunga na Nato.

Time will reveal what I'm saying here.
Mkuu kuwekewa vikwazo ni bora kuliko kuzingirwa kutekwa na kuwa mtumwa. Yaani uwe roboti la matope. Hakuna mtu mwenye akili timamu ataruhusu kuzungukwa kwa makombora na mizinga. Aza waisi labda hatuna braini.
 
Wakati mwingine usisubiri mtu akuambie sasa tumia akili, soma alichokisema Trump afu jiulize alikuwa na maana gani.
Mkuu nisaidie kutafsiri maneno ya Trump, kisha na maneno ya Rais George W. Bush aliposema 'Putin is a very smart tactician' kwenye video hii hapa chini. Natanguliza shukurani za dhati kwako kwa msaada wako huo uliotukuka.
 
Wewe shida yako ni vita itokee., lakini wenzetu hawako uko uliko wewe Unaambiwa 40% ya gesi ya Russia anauza ulaya sasa niambie ni kwa vipi Russia hataanguka kiuchumi? na kuanzia ile juz alivyovamia sasa ameanza rasmi russia kulipa gharma yake ya uvamizi.
Na mmeshaambiwa hakuna nchi 1 inayoweza ku cover hio 40% ya mrusi na bado gharama za hio source nyingine ya gesi........atakaeanza kulia ndo alieumizwa..............Mchina alishamuhakikishia mrusi soko la gesi yake............hapa yatajirudia tu ya crimea mtu anakaza baadae anaona anajipiga bao mwenyewe analegeza
 
Mkuu huyo Clinton ni Bill Clinton na alimsifia Putin mwaka 2014, miaka mingi kabla hata Biden hajawa Rais wa US.

Lakini pia hata George W. Bush alishawahi kumuelezea Putin kuwa ni mtu smart sana (cheki video hii kuanzia sekunde ya 30)

Haya mambo ya kusifiana yanawashangaza sana kwa sababu tu ya kutokufahamu jinsi siasa za kimataifa zilivyo. Ushamba!

Ni mambo ya kawaida sana haya katika siasa za kimataifa hasa za haya mataifa makubwa. Of course ni mambo mageni kwa watu wasiofuatilia haya mambo! Hata Putin naye ana tabia ya muda mrefu tu ya kusifia marais wa Marekani.

Putin amewahi kumsifia Joe Biden kuwa ni mtu "professional" na akaongeza kuwa Biden ni "completely knowledgeable on all issues".

Link hii hapa, utakuta video humo:

Nanukuu kwa uchache maneno ya Putin aliyowahi kuyasema kumhusu Biden:

"Mr. Biden is a professional, and you need to be very careful when working with him so as not to miss something."

Mwisho wa kunukuu! Sijaongeza neno wala sijapunguza neno!

Wakati fulani, Putin pia amewahi kumsifia Trump kwamba ni mtu mwenye kipaji cha hali ya juu (very colourful, talented person):

Haya ni mambo ya kawaida sana katika siasa ndugu zangu[ni]. Jitahidini kuzifahamu siasa hasa za kimataifa kwa undani zaidi, inasaidia sana kuondokana na ushamba juu ya mambo madogomadogo kama haya.
 
Weka hapa kusifia kulikoambatana na utekelezaji wa tukio zito, tete na tata kama hili alilolifanya Putin.
 
Weka hapa kusifia kulikoambatana na utekelezaji wa tukio kubwa na tata kama hili alilolifanya Putin.
Putin amewahi kumsifia Biden kuwa ni mtu "professional" na pia ni "completely knowledgeable on all issues". Umeelewa maana yake!

Pia akasema: "you need to be very careful when working with him so as not to miss something". Umeelewa maana yake!

Jitahidi kuzifahamu vyema siasa za haya mataifa makubwa.
 
Trump kamsifia Putin kuwa 'namna alivyojiingiza Ukraine' katumia akili kubwa mno na katamani pia US wangetumia njia hiyo ktk kudili na sehemu za nchi inayopakana nayo upande wa kusini.

Kusifia huko kumeambatana na tukio zito na tete ambalo macho ya dunia nzima yalikuwa yakilifikiria na mataifa makubwa yalikuwa yakipiga mikwara.

Sasa wewe mjuvi weka link ya sifa alizotoa Putin kumsifu rais yeyote wa Marekani kwamba katumia akili kubwa ktk kudili na changamoto fulani nzito na tete. Sio ulete stori za marais wanatembeleana nchini mwao kisha wapiga stori za mtu na mgeni wake huku wakisifiana kinafiki.
 
Haya mambo ya kusifiana yanawashangaza sana kwa sababu tu ya kutokufahamu jinsi siasa za kimataifa zilivyo. Ushamba!

Haya ni mambo ya kawaida sana katika siasa ndugu zangu[ni]. Jitahidini kuzifahamu siasa hasa za kimataifa kwa undani zaidi, inasaidia sana kuondokana na ushamba juu ya mambo madogomadogo kama hahaya.
Halafu jifunze nidhamu ya namna ya kujadiliana na mtu usiyemfahamu ktk mitandao ya kijamii.

Kutumia lugha ya ukakasi pekee hakuwezi ipa nguvu hoja yako (kama ni dhaifu), wala kutumia lugha ya staha hakuwezi idogesha hoja yako (kama ni madhubuti).

Na kwa kukupa faida tu ni kuwa ukitumia lugha ya staha ktk kujadiliana na mtu inakupa bonus ya kudhaniwa kuwa umestaarabika.
 
Back
Top Bottom