Trump asitisha misaada ya ARV na dawa za Malaria kwa muda

Trump asitisha misaada ya ARV na dawa za Malaria kwa muda

Bara la Afrika linaenda kupoteza zaidi ya nusu ya watu wake kwa malaria, ukimwi, pepopunda, kifaduro, surua, kifua kikuu nk.
Ingawa si jambo la kufurahia lakini
Utegemezi umedumaza maendeleo ya bara hili lenye kila aina ya raslimali.
Sasa umefika muda wa kuzikabilii changamoto zetu kupitia raslimali tulizonazo.
 
Nchi za kiafrika sio maskini na sio kweli kwamba zinashindwa ku-run bajeti zao, shida kubwa Iko ktk mipango na matumizi, mipango ni mibovu na ufujaji wa hela uko Kwa kiwango cha juu...pesa nyingi zinaelekezwa kwenye matumizi na kipumbavu na anasa za watawala...ma vieite yanazunguka nchi nzima, huku mabasi ya kisiasa ya CCM yanapita, hujakaa vizuri Boeng linapaa kuelekea Korea limejaza machawa waliolipwa posho na huduma za hadhi ya juu ..NGOJA TRUMP ATOE ELIMU KWA VITENDO MAANA KUSKIA KWA KENGE NI MPK DAMU ITOKE MASKIONI
Umaskini wa kifikra unaitafuna afrika tunapeleka bajeti kwenye mambo ya kipumbavu sana yani hatuwezi kusimama na hatujawahi kufikiria kujitegemea kwenye mambo muhimu kama haya..Acha Tujifunze in a hard way ili upumbavu upungue afrika
 
Ni uamuzi mzuri kwa taifa la marekani,ila omba hali hii isikutokee wakati una nduguyo au wewe mwenyewe una maambukizi ya VIRUSI VYA UKIMWI NA UKIMWI,ni taarifa mbaya mno kwa waathirika,taifa na afrika kwa ujumla.

Ni kweli inasikitisha kama ulivyoandika lakini sio ndugu wote ni wema wengine wachawi.
Hao ambao ni wachawi Mungu ajue kuwalipa kwa mabaya yao ya kuharibu maisha ya watu kama ilivyoandikwa kuwa : “ asiachwe mwanamke mchawi kuishi” maana yake afe.
 
Ni utaratibu wa kawaida kwa US Gov kama Kuna executive orders ambapo hudumu siku 90 tu raisi ana hiyo power isipopotishwa na mamlaka zao basi hiyo order inakufa.Ametoa stop order ila sio kwa kila kitu ,ARVs zipo na hajasema zisimame wapendwa watu wana interpretation zisizo na ukweli Kuna waiver zimetolewa kwenye issue za kibinadamu WAtanzania huwa hawatafuti ukweli.Halafu Serikali ya Tz hawajasema lolote kwa kuwa hii ni stop order sio closure of USAID funds
 
Hii kitu sio ya kushangilia, wakati tunasema ni bora ili Serikali ijitegemea ila tuelewe sio Tanzania peke yake inayotegemea hiyo misaada, zipo Nchi zilizoathiiriwa sana na zinauhitaji mkubwa sana wa hizo dawa, so tutarajie vifo vingi vya watoto wachanga, watoto njiti na watu wenye maambukizi ya ukimwi maana imekuwa ghafla. Naamini hakuna Nchi ilitarajia hili
Serikali yako ta CCM ifanye hayo badala ya kununua ma V8.
 
Safi kabisa,simlikuwa mnasema Kamala asichaguliwe bora Trump
Na kuna clip nimeiona aliulizwa kuhusu kama anatenda haki kuwafurusha watu like that akajibu hao ni Alliens wanakuja kupora rasilimali za Wamarekani,
Lakini hapo hapo anaitaka Greenland, Panama, Canada huo sio uporaji?
 
Back
Top Bottom