Ambao mpo kwenye mitandao ya kijamii,youtube au sky news Rais wa marekani yupo live kuzungumzia mgogoro wa Marekani na Iran.
Pia kama una tv unaweza kuangalia CNN,Aljezira .
Tupeane updates
*****
UPDATE
Baada ya Iran kushambulia Kambi mbili za Jeshi za Marekani huko Iraq, Rais Trump amebainisha hakuna Mwanajeshi yeyote wa Marekani aliyeuawa au kujeruhiwa na uharibifu kidogo tu ndio umetokea kwenye Kambi hizo
Aidha, amesema vikosi vya Kijeshi vya Marekani viko tayari kwa lolote ila hivi sasa Iran inaonekana kusitisha kutaka kulipa
BAADHI YA SENTENSI MUHIMU ZA TRUMP MUDA MFUPI ULIOPITA KUHUSU MZOZO WA US NA IRAN
"Madhara tuliyoyapata baada ya uvamizi ni kidogo na hakuna askari au mmarekani aliyeumia au kufariki''
"Kwakuwa mimi ndiye Rais wa Marekani, Iran hataruhusiwa kuzalisha silaha za Nyuklia''
''Tutaipiga iran na Vikwazo vya kiuchumi kufuatia kushambuliwa kwa kambi za Marekani na vikwazo hivi vitadumu hadi pale Iran itakapobadilisha tabia zake''
''Vikosi vyetu vinajiandaa kwa lolote''
"Kwa sasa Iran inaonekana haina nguvu tena na hii ni muhimu kwa wamarekani na duniani ili kudumisha usalama''
''Kwa watu wa Iran na viongozi wake tunaomba muwe watu wema na wa kuifanya dunia kuwa sehemu salama na sisi tunawatakia maisha mema katika nchi yenu''
''Marekani iko tayari kuhakikisha amani inatawala duniani na atakayekuwa tayari''
Kauli zake hizi zinaonesha ataanzisha mazungmzo na Iran muda siyo mrefu na sidhani kama ana mpango na Vita. Sentensi ya mwisho imekaa kidiplomasia sana na imetoa mwanya wa mazungumzo kwa mzozo wa Marekani na Iran
Rais Trump amemaliza kuzungumza na vyombo vya habari muda mfupi uliopita, Ikulu ya White House Marekani. Picha na Shirika la habari la AFP
, ambapo ni kitu kizuri kwa pande zote zinazohusika na kizuri zaidi kwa Dunia nzima
Awali, akiaza hotuba yake amezungumzia Iran na silaha za nyuklia akisema “Kwa muda wote nitakaokuwa Rais wa Marekani, Iran haitaruhusiwa kuwa na silaha za nyuklia.”