Trump: Hakuna Mwanajeshi wetu yeyote aliyekufa au kujeruhiwa katika shambulio la Iran. Iran inaonekana kusitisha kulipa kisasi

Trump: Hakuna Mwanajeshi wetu yeyote aliyekufa au kujeruhiwa katika shambulio la Iran. Iran inaonekana kusitisha kulipa kisasi

Wakikata yale maARV tu watu wataanza kudondoka kwa mdondo...

Yaani vita yoyote itayomuhusisha USA itahusisha na mataifa ya Ulaya yale yapo NATO
gwajima yuko na manyaunyau watapata tiba mujarabu heheeeehee
 
Iran kumbe wanatisha hivi...hii soft tune ya Trump sikuitegemea.!!!
====
Lakini nadhani watakuwa wanaplan more 'evil' dhid ya Iran. Iran must not be ease to this soft bait!

Waache wajinga wajitape, hawamfahamu mmarekani,
Huwa anajifanya amesahau sasa litapigwa shambulizi Iran watabaki kulalamika, Marekana ana base kubwa sana kijeshi duniani, amewekeza sana kwenye silaha, atamtwanga tu maana hawezi kujionesha inferiority asije vutwa ndevu na vibonde
 
Vita ya marekani inaathari kubwa mno kwa mataifa kama ya kwetu,,mzigo unatoka USAID ukate wote na mingine mingi hali itakuwaje,,ni jambo la kuhuzunisha lakini pia mamilioni ya watu kufarika na kukosa makazi sababu za vita n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa ndiyo utamuelewa rais wetu magufuli nia yake kutaka tujitegemee, mtikisiko kidogo tu kama hii,unaanza kutetemeka juu misaada, bado mnaponda jitihada za anko magu
 
Waoga? Kapiga military base baada ya mikwara yote ya Trump na kasema kuwa ni yeye bado unamuita muoga? Dah kwa kujipa moyo... US anajiepusha kuingia vitani ashajua kuwa Iran yuko tayari na si ajabu anajua kuwa kuna sababu inayompa kiburi Iran siyo kawaida sasa hapa anafanya damage control ya kuikimbia vita eti angeua hata askari mmoja?
US this time kapatikana allikuwa kazoea washika waaarab makalio sasa kakutana na Muajemi
mawigi muongo sana hivi hizo kambi azina askari mpaka kusipatikane ata majeruhi nimecheka sana leo usa kaveshwa kikuku na iran
 
Ambao mpo kwenye mitandao ya kijamii,youtube au sky news Rais wa marekani yupo live kuzungumzia mgogoro wa Marekani na Iran.

Pia kama una tv unaweza kuangalia CNN,Aljezira .

Tupeane updates
*****

UPDATE
Baada ya Iran kushambulia Kambi mbili za Jeshi za Marekani huko Iraq, Rais Trump amebainisha hakuna Mwanajeshi yeyote wa Marekani aliyeuawa au kujeruhiwa na uharibifu kidogo tu ndio umetokea kwenye Kambi hizo

Aidha, amesema vikosi vya Kijeshi vya Marekani viko tayari kwa lolote ila hivi sasa Iran inaonekana kusitisha kutaka kulipa kisasi, ambapo ni kitu kizuri kwa pande zote zinazohusika na kizuri zaidi kwa Dunia nzima

Awali, akiaza hotuba yake amezungumzia Iran na silaha za nyuklia akisema “Kwa muda wote nitakaokuwa Rais wa Marekani, Iran haitaruhusiwa kuwa na silaha za nyuklia.”

Huyu Trump nisawa na Mbwa mwoga anaye bweka nakuonesha makali yake huko tweetani tu! Linapokuja suala la mapambano hata kati yake na Nyau Jeuri hurudi nyuma huku mkia akiuburuza chini kwa woga kisha kutoka mbio mabaya! Jasiri katika Marais wa Marekani niliye wahi shuhudia zama hivi ni George Bush tu. ambaye alikuwa anaamua kulianzisha varangati bila woga wala ruhusa ya hao wengine! Nadhani Bush Yeye alikuwa akiona NI BORA KUJUTIA KULIKO KUTIWA! hakuwa kama huyu Coward Trumpet.
 
Kusema ukweli nimeshangazwa sana na hotuba ya leo aliyoitoa Trump.

Yani raisi wa taifa lenye nguvu duniani anaongea kinyonge namna hii utafikiri raisi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar,!!?

Sio siri tena marekani ameshaanza kurealize njia aliyoingia is a dead end.

Sent from my Redmi Note 4 using JamiiForums mobile app
 
Marekani walitungua ndege ya iran miaka, wakaja kulipa wakatungua ya US.

Wameua kiongozi wa iran juzi... basi US wajianda hii lipizi litakuja timia tu na huo wakati haitajulikana lini wapi nasaa ngapi.. lazima walipe.
Waache wajinga wajitape, hawamfahamu mmarekani,
Huwa anajifanya amesahau sasa litapigwa shambulizi Iran watabaki kulalamika, Marekana ana base kubwa sana kijeshi duniani, amewekeza sana kwenye silaha, atamtwanga tu maana hawezi kujionesha inferiority asije vutwa ndevu na vibonde

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora wewe hata kitimoto kinapanda mwenzako hali taiti huko naskia hata maji anaomba alainishiwe

Mazee utamu wa vita usimame upande unaoshinda hili shati kubwa iran halimfit labda asubiri akue

Iran hata kombora la kuifikia tanzania hana, inamaana hata sisi tunaweza tukazicheza na tukamkalisha

Silaha za iran unazoziona wewe kama zakivita marekani anaziona kama zakutulizia ghasia mtaani yani kama maji ya upupu tu

nishakwambia kwamba ile laki 5 niliyoitunza baada ya kukosa wazo la biashara kwa muda mrefu nataka nikafungue biashara ya chips kule iran

Hapa anaye nikawiza ni mmarekani nasubiri arushe kombora mi nibebe viazi tu maana nyama ntaikuta kule kule

'Iran hata kombora la kuifikia tanzania hana, inamaana hata sisi tunaweza tukazicheza na tukamkalisha'

Hapo nimeelewa vzr exposure yako.

dodge
 
Kumbuka wenzetu hawana pupa, wanatengeneza timing ili wakishambulia wanaharibu nguvu na sehemu muhimu ambazo ni hatarishi kwao
Ndio uoga wenyewe huo,tangaza vita mpigane face to face story za kuviziana zinafanywa na vikundi vya waasi na sio nchi inayojisema eti ina nguvu kubwa duniani.

dodge
 
Trump ni msanii sana, hapa anakuja na stori za Alinacha, hana ubavu wa kusema ukweli kwamba hakuna mwanajeshi wa Merikani aliye poteza maisha hii ilitokana na Iran kuwa na uwanadamu/ustaarabu wa kutoa taarifa mapema kwa Kiongozi wa Iraq kwamba Iran itashambulia kambi mbili za Jeshi la Merikani saa mbili kabla ya tukio - ujumbe huo uliwafikia viongozi wa jeshi la Merikani ambao walitoa amri ya wanajeshi kukimbilia kwenye mahandaki ili wanusuru uhai wao - hicho ndicho kiliokoa wanajeshi wa Merikani huko Iraq, in other words Iran didn't plan to kill US troops.

Nimeona picha za satellite zikionyesha US military bases kabla na baada ya shambulio la makombora ya Iran - majengo muhimu manne ndani ya airbase yamechakazwa kweli kweli na runway kuharibiwa kabisa!! Lengo la Iran katika shambulio hilo ni kutuma ujumbe kwa USA kwamba hivi sasa Iran ina missiles ambazo ni dead accurate katika ulengaji shabaha na range ya kufanya mashambulizi katika bases zote za Merikani zilizopo mashariki ya kati na Continental Europe - accuracy za missiles za Iran zimeshtua sana US military top brass, ndio maana Trump amehamua kanywea kwa kupunguza war rhetoric zake - ukweli wa mambo Iran ni maji marefu.
 
Msaada Moderator JF rekebisha kichwa cha habari Iran kufanyatua makombora
 
Nawasikitikia sana mnao shangilia vita yaani vita ianze mafuta lita iuzwe elfu 5

Halafu vita haijawai kuleta tija katika ulimwengu wa leo na jana.

kuianza ni simple ila kuimaliza ndio balaa.
kuna watu watatoboa kama vita itakuwepo pia kuna mataifa yatakua dona kantry kama vita itakuwepo pia kuna kuna sisi tunataka tu zipigwe kuleta heshima so inategemea upo kundi gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waache wajinga wajitape, hawamfahamu mmarekani,
Huwa anajifanya amesahau sasa litapigwa shambulizi Iran watabaki kulalamika, Marekana ana base kubwa sana kijeshi duniani, amewekeza sana kwenye silaha, atamtwanga tu maana hawezi kujionesha inferiority asije vutwa ndevu na vibonde

Nikiona comments kama hizi unisikitisha sana!! Hivi waVietNam wangekuwa na mentality kama za kwako za kumuogopa Uncle SAM si wange kuwa chini ya Utawala wa Merikani mpaka sasa? Afghanistan, je, huu mwaka wa ngapi tangu Merikani ivamie Afghanistan - miaka karibu kumi na saba imekati wakati huo huo Wateliban wameshikilia karibu 95% ya aridhi ya Afghanistan huku Merikani inajaribu kupitia mlango wa nyuma kuwabembeleza Mullas wa Teliban wasitishe vita wafanye mazungunzo ya kumaliza vita baina yao - who can take Yankees seriously labda nyinyi mliokunywa maji ya bendera ya star and stripes.
 
IRAN anathubutuje kutunisha msuli mbele ya mmarekani?

America ingekua na nguvu mdomoni basi isingem-attack kasimu, IRAN isingekua na mdomo ingelipisha na sio kupiga off target

Umeweka taarifa nusu, weka na Satellite image ya majengo yaliyotandikwa ndani ya hiyo base

Ukweli ni kuwa Missiles zimetua ndani ya majengo kadhaa ndani ya hiyo base na zimeyachakaza.

Sasa huko siyo kupigwa au ulitaka kupigwa lazima watu wafe?

Kwa hiyo kama hakufa mmarekani ndo base hazijapigwa? -Kaka vitu vimetua kwenye base precisely siyo off target wala nini
 
Back
Top Bottom