[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
MAREKANI YAKANUSHA TAARIFA ZA KUONDOA MAJESHI YAKE IRAQ
Waziri wa ulinzi wa Marekani, Mark Esper amekanusha madai kuwa majeshi yake yanataka kuondoka Iraq, baada ya barua kutoka kwa jenerali wa Marekani kupendekeza waondoke.
Barua ilisema kuwa Marekani itaondoa vikosi vya majeshi yake siku zijazo au wiki baada ya wabunge wa Iraq kuwataka waondoke.
Bwana Esper alisema kuwa hakuna maamuzi yeyote ya kuondoka ambayo yaliondolewa.Mkanganyiko huu wa vitisho ulikuja mara baada ya jeshi la Marekani kumuua kamanda wa jeshi wa Iran Qasem Soleimani.
Jenerali Soleimani aliuawa katika mapambano ya anga huko Baghdad siku ya ijumaa baada ya rais Trump kuamuru wafanye hivyo.
***************
Ya leo hio na inatrend kila media imezungumzwa na waziri wa ulinzi
Sent using
Jamii Forums mobile app