Tuache Ufyatu: Mtu Hawi Gaidi kwa Kuitwa Gaidi

Tuache Ufyatu: Mtu Hawi Gaidi kwa Kuitwa Gaidi



Unaweza kumuita mtu chechote kile; lakini kumuita mtu tu kitu hakimfanyi mtu kuwa kitu kile. Ni kweli kwamba kuna majina mwingine ukimuita mtu unamvunjia heshima, hadhi, na utu wake mbele ya jamii. Kwa mfano, mtu ameachana na mke wake au mume wake lakini kwa sababu ya machungu ya kuachana anaenda na kumtangaza kuwa "yule alikuwa malaya" au "alikuwa mlevi" n.k Sasa watu wengine wanaweza kweli kuamini na wao wanaweza kueneza habari hizo kuwa "yule alikuwa malaya". Hata ukimuuliza alijuaje atasema "jamaa yake walioachana" ndio alimuambia.

Kwenye siasa hili nalo ni kweli. Kuna mambo unaweza kumuita mpinzani wako wa kisiasa ili kumvunjia heshima, hadhi, na utu. Na wakati mwingine unaweza kumuita kitu ili kumharibia nafasi zake za kisiasa. Sote tunajua jinsi gani jina aliloitwa Dkt. Salim A. Salim lilivyomvurugia nafasi yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano 1995. Na tumeona mbinu hii ikitumiwa karibu na pande zote za kisiasa nchini - unaweza kuwaita watu "wachochezi" au "mafisadi" au unaweza kumuita mtu jina lolote.

Hata hivyo, linapokuja suala la kisheria - ambalo ni tofauti na la kisiasa - ukimuita mtu jina na mkaenda mahakamani basi suala huko ni ushahidi na uzito wa ushahidi huo (preponderance of evidence). Ndio maana kuna kesi za kumtangaza mtu vibaya au kumzushia ubaya (libel and defamation). Dkt. Salim huyo huyo aliwahi kushinda mamilioni ya hela dhidi ya gazeti la The East African miaka kadhaa nyuma kutokana na makala yao moja hivi.

Sasa Mbowe amedaiwa kuwa ni "Ghaidi" na jeshi la polisi. Kwa vile hili ni suala la mahakamani na la kisheria basi ni jukumu la mleta mashtaka kuleta ushahidi usio na shaka wa ughaidi huo. Na ili kitu kiwe ushahidi ni lazima kikidhi matakwa ya kisheria. Kusema tu "tuna ushahidi" hakufanyi ushahidi huo kukubalika mahakamani. Ni kwa sababu hiyo binafsi nasubiria kuona hicho kinachoitwa "ushahidi" hasa utakaposimama na kuhojiwa na upande wa utetezi na kupimwa kwa mwanga wa sheria kuona kama unaweza kumtia mtu hatiani.

Nje ya hapo, inawezekana hili la "ughaidi" linatumika tu tena kisiasa kama nilivyoelezea hapo juu. Kinachotakiwa kufanyika siyo tu kutaka kesi ifutwe au iondolewe bali iachwe iendelee mahakamani ili ushahidi uletwe, vieleleze viletwe ili kwa mara moja na daima uamuzi wa mahakama utolewe juu ya tuhuma hizi. CHADEMA wasitake tu viongozi wao waachiliwe pasipo masharti bali watake haki itendeke na kesi iharakishwe.

Kwani, kumuita mtu ughaidi hakumfanyi kuwa ghaidi bali ushahidi usio na shaka (siyo wa kupika) unaoweza kumtia hatiani mtu katika mahakama yoyote iliyo huru.

Haki Itendeke na Ionekane Inatendeka na Imetendeka kama inavyotakiwa kutendeka bila kuteteleka.

MMM

Mahakama zetu zingekuwa zinatenda haki kwa maana ya haki, hata hawa wanaombikiza kesi wasingethubutu. Lakini kwa sasa mahakama zimekuwa sehemu za kukomolea wapinzani wa watawala, ndio maana unaona kesi za kubambikia zinakuwa nyingi, maana mahakama zimekubali kutumikia siasa chafu. Na mifano ya dhahiri ya mahakama kutumikia siasa chafu yapo.
 
I see you got my dick in your mouth!

Nani mwingine zaidi yangu aliyemchana Magufuli humu?

Nikuwekee orodha toka 2015 mpaka 2021 ya mada za mimi kumchana Magufuli?

Stupid brainless dunce.
Huna lolote wewe ! kuchana kimkakati nani asiyekujua ?
 
CCM wameishakosa kibali mbele ya Mungu cha kuwatawala watanzania. Wanatumia mabavu sasa
 
Umeambiwa subiri ushahidi,wewe unatoa hukumu kwa kusoma mashitaka?
Lema amekimbia nchi kwa ajili ya kesi hii hii au umesahau?
Mkuu, ameshitakiwa kwa kutoa fedha zitakazotumika kwenye ugaidi. Kwa mashitaka hayo unatakiwa uthibitishe katoa fedha kwa ajili ya ugaidi. Unaona inavyokuwa ngumu?

Kwa sababu aliyepewa fedha lazima uthibitishe alikuwa ndiye anaeenda kufanya huo ugaidi. Chadema wanaweza hata kuandaa concept note ya kuboresha ofisi na wakaandika waliopewa fedha ndio wangesimamia zoezi hilo. Kesi ndogo sana hii
 
Taratibu unarudi upinzani now
Dokta Slaa vipi?Nae ata join?..
Taratibu Tu mwisho utarudi kuwa think tank ya Chadema again..Hadi aje Rais wa 'taasisi' yenu mwingine ndo utarudi tena Ccm..

Tunakuelewa sana
..duh!... sidhani kama atarudi tena upinzani huyu mzee bora ajikalie kimya tu huko US ale pepo asubiri mpaka mhafidhina mwingine wa Ccm aukwae urais.
 
Ninamwomba Mwenyezi Mungu amnusuru Mh. Mbowe na matatizo ya uteswaji, kunyimwa HAKI yake kwa kubambikwa kesi ya UONGO. Mungu baba wasamehe watesaji na uwaonyeshe njia sahihi.
 
Mwendazake alifanya vibaya hadi shetani akamkana lakini hukuona.

Tuache sisi tuliozoea kwa kuuliza,kukaripia na hata kupiga kelele bila kujali dini ya mtu au kabila lake.

MMK,THE BIG SHOW Ritz Baba yenu mmoja wajomba tofauti.

Seems clearly you don't understand the degree of the fucky that I don't give,mwanakijiji amekueleza uhalisia ulivyo,Ila kwa kuwa wewe na wenzako kama mdude na wengineo hamna common sense hamuwez kuelewa
 
Ni kweli haki lazima ionekane itendeke lakini tumeona watu walioshitakiwa kwa kosa hili wakikaa ndani kwa takriban miaka minane na mwisho DPP kusema hataki kuendelea na kesi. Mimi nadhani tufike mahali mahakama iwe inazitupitilia mbali kesi zinazochukua zaidi ya mwezi mmoja kuanza kusikilizwa kwa kisingizio chochote kile na kuamuru mshitakiwa alipwe fidia.

Amandla...
Hii kesi haitakuwa hivyo na haitafika huko...

Kwa nini?

MOSI, Ni kesi very unique. Katika historia ya Tanzania huru tangu mwaka 1961 na tangu mfumo wa vyama vingi kuingia tena 1992, hakuna kiongozi wa chama kikuu cha upinzani amewahi kutuhumiwa kushitakiwa kwa kosa serious la UGAIDI (terrorism) kama analolishitakiwa nalo Freeman Mbowe..

PILI, kwa ushahidi wa kimazingira (circumstantial evidences) wa kauli na matendo ya "wanaomshtaki", maisha na historia ya mshtakiwa bila shaka hata mtoto mdogo anaweza kutambua mara moja kuwa, kesi hii ni ya kutengeneza kwa sababu za kisiasa..

TATU, ni kesi iliyobeba mstakabali wa hali ya kisiasa (utawala) na uchumi kitaifa huku mataifa wahisani na international organizations kwa Tanzania zikiwa na maslahi nayo...

Kwa kifupi sana, kwa hili CCM na serikali yao walishagundua kuwa wamefanya kosa kubwa na hata wao wanatafuta namna kulimaliza pasipo kuwaletea madhara waliyokuwa hawategemei....
 
Sabaya ni mpinzani?!
Sabaya ni wangapi kati ya msitu wa maovu ya CCM?

By the way Sabaya ni jambazi wazi wazi huhitaji hata kuanza kupoteza muda

Tazama hapo uone hata Sabaya anavyofanyiwa bado haifuti ukweli wengi wa waliobaki CCM hawaguswi huyu katolewa kama sadaka na kwa maigizo hayo naona akija kuachiwa huru !
 
Utawala wa rais aliyepita uliwabambikia watu kesi za ufisadi na kutakatisha ili wasipate dhamana, Ulikuwepo lakini hukumkosoa.
Kuna watanzania wenzetu waliitwa magaidi, wamekaa Segerea miaka 8, pia ulikuwepo na hukuinua ulimi kuwatetea.
Leo unaanza kujirudisha uraiani kwa kuwa aliye madarakani siyo yule anayemtaka.
Watu wa aina yako hawastahili kuaminika wala kuheshimika.
Walikosoa

Kama ambavyo mlimtosa slaa Kwa ajili ya lowassa

mlitema bigijii Kwa karanga za kuonjeshwa
 
Sabaya ni wangapi kati ya msitu wa maovu ya CCM?

By the way Sabaya ni jambazi wazi wazi huhitaji hata kuanza kupoteza muda

Tazama hapo uone hata Sabaya anavyofanyiwa bado haifuti ukweli wengi wa waliobaki CCM hawaguswi huyu katolewa kama sadaka na kwa maigizo hayo naona akija kuachiwa huru !
View attachment 1883769
Si ndio maana yuko ndani?

angekua chadomo mngetaka awe uraiani
 
Back
Top Bottom